Ramon Abbas
JF-Expert Member
- May 4, 2021
- 1,964
- 3,900
Kunguni wanakera sana, unakosa usingizi wakati mwingine unadhalilika!
Basi bwana kuna hii dawa inaitwa diazinone, niliitumia mwaka 2015 na nikafanikiwa kuwaangamiza hawa wadudu korofi.
Ghafla tena naitwa nyumbani kwamba wadudu wanasumbua, njoo utupe msaada, nikaenda kweli nikakuta wamejaa kwenye neti, godoro mpaka kitandani, hadi watoto wamehamishiwa vyumba vingine.
Nilivyoona hii hali basi nikaingia mjini na sh elfu 10 tu nikiwa na uhakika hii inamaliza kila kitu.
Kweli, nikapata dawa chupa 1 sh elfu 2.5 nikachukua 2 kwa elfu 5.
Chupa ya spray nikabeba kwa elfu 4.
Chupa 1 unachanganya na lita 2 za maji safi.
Kisha unakoroga vizuri (hakikisha kama unaweza uvae gloves, barakoa kuoa suffocation, PPE ni muhimu maana hii ni sumu hatari sana)
Nikachanganya dawa vizuri na maji mpaka ikawa kama maziwa
Baada ya hapo nikaweka kwenye chupa nikaanza spray, vitu vyote lazima viwe katika sehemu ya wazi yenye hewa na mwanga wa kutosha ili mdudu aonekane vizuri na kuepuka suffocation.
Kusema kweli hii dawa ilileta matokeo mazuri sana mpaka sasa wadudu wamepungua kwa asilimia 90