Nimefanikiwa kumjengea mama yangu nyumba kabla ya birthday yangu ya miaka 24 mwaka huu

Heading ya story yako ni very inspiring. Ila maudhui yake, SIO POA. Mi nilihani ulipiga zile husstling za kibabe sana mpk at that age ukatoboa na kumjengea maza mjengo..!! Kumbe ni shortcut ya FOREX bana...!!!

Ingekuwa umeendeleza hustling za kilimo, nafaka, ukauza ukatoboa, ningesema daaah, kweli dogo umetoboa kichizi na umepambana sn. Ila kumbe umepambana na smartphone??

Nway, KUTOBOA NI KUTOBOA TU, but, story yako sio nzuri sana kwa vijana wanaokomaa kutafuta maisha now. Unaweza ukawatamanisha kuingia FX wakapigwa mpk wakajuta.

All the best..!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Utafutaji kila mtu ana njia yake chamsingi ni legal
 
Mkuu wewe ni scalper, swinger au day trader?
Mkuu mimi huwa nafanya scalping yani nikipata faida tu nafunga

Tokea nianze kufanya trading ninadili na pair mbili 2 hizo profit zote nikikuonyesha screenshot ni eu na gu

Huwa na trade mara moja moja gold inapofika point nzuri

Kwa maana hiyo pair zoote, commodities, indices sizigusi sina utaalamu nazo, ndio maana kumuelekeza mtu inakuwa vigumu

Nimemasta pair mbili tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niseme tu haya maisha nilianza kuyaona machungu sana punde tu nilipo anza darasa la kwanza, nakumbuka ilikuwa 2003 . Mara ya mwisho kumuona baba yangu mzazi ilikuwa ni siku aliyonipeleka kuniandikisha shule hadi leo naandika hapa sijawahi kumuona tena.

Huyu baba yangu aliondoka kwenda nchi za njee kutafuta maisha ,safari yake alianzia nchini kenya lakini hadi leo hatujui alizamia nchi gani maana hakuwahi kurudi tena.

Wakati anaondoka aliacha amekorofishana na ndugu zake karibia wote hadi na mama yake mzazi ambaye ni bibi yangu kisa cha ugomvi ni kuhusu mama yangu kwani alikuwa ni mke wa pili na ndugu zake hawakutaka mama yangu aolewe.

Sasa baada ya baba kuondoka ikapita miezi kadhaa ndugu zake pamoja na bibi yangu wakaja wakatufukuza kwenye nyumba tuliokuwa tunakaa wakisema mama yangu sio mke halali. Na huyu huyu Bibi yangu ndio alienda weka kipingamizi kanisani kuwa ndoa haiwezi fanyika kwani baba tayari anawatoto kwa mke mwingine

Baada ya kufukuzwa tulihamia kwenye kiwanja kingine lilikuwa ni shamba tukajenga kijumba kidogo sana cha matofali mabichi juu tukaweka majani. Wakati huo tulikuwa mimi , mama na dada yangu ,kiukweli maisha yalikuwa magumu sana kwani mama yangu alikuwa hana kazi yoyote ni mama wa nyumbani tu

Yaani naposema maisha magumu yalikuwa magumu kweli kiasi kwamba tulikuwa tunakosa hata pesa ya chakula, madaftari, nguo za shule,. Viatu yaani mtaani Sisi ndio tukawa tunaonekana hoe hae. Kuna siku njaa ilitupiga ikabidi nitoroke kisiri siri hadi kwa baba mkubwa atupe msaada asee alinitimua na matusi ya kutosha ila sikuwahi mwambia mama

Baada ya hapo nikachukia shule sii kwamba nilipenda ila ilifika mahali nguo za shule zikachakaa hadi bukta ikatoboka makalioni, viatu vikaisha nilikuwa na mfuko flani hivi wa daftari unaitwa sport ulizeeka ukachanika vibaya.

Nakumbuka kulikuwa kunamwalimu mkali balaa alikuwa anapiga fimbo hatari kunasiku alinidaka kwenye kosa wakati nimelala chini anichape bukta ikawa imechanika ikabidi aniambie dogo inuka uondoke .

Tokea kipindi hicho nilikuwa na kaa utoro hadi miezi 3 ni barua zilikuwa zinakuja nyumbani wakati wa mitihani za wito wa mzazi .

Katika kipindi hicho chote hakuna kibarua ambacho sikuwahi fanya kuanzia kufyatua matofali yale ya udongo kipindi hiko tofali moja unalipwa sh 30 , kuchota mchanga ndani ya mto
Mpaka mjaze gari yaani hakuna kazi ya kipuuzi kama hiyo unazamisha Koreo ndani ya mto unajaza koreo ukitaka kutoa umwage njee maji yote yanapeleka mchanga,

Kunazile kazi za kupakia mawe kwenye tipa nilikuwa mdogo ila nilikuwa nakomaa hadi kunasiku boss alikuja kutembelea pale ikabidi anihamishe kitengo cha kwenda kutengeneza baruti.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya graduation ya darasa la saba nilikuwa sijalipia sh 1500 kabla ya kwenda ukumbini tulianzia shuleni kuna mwalimu alikuwa ananifahamu akaniambia saidiana na wale jamaa mbebe hizo spika muweke kwenye gari mpeleke ukumbini ndio nikapata chance ya kuingia ,Muda wa kucheza mziki kwa mavazi niliyokuwa nimevaa hakuna hata aliyetaka kunisogelea

Katika kipindi cha hapa katikati niliwahi hadi kurubuniwa tukaenda kuiba kuku kwenye nyumba ya mtu nusu nichomwe moto na raia bila vijana wa mwenyekiti kuwa wababe sijui siku ile ingekuwaje hapo nilikuwa fm2. Toka siku hiyo nione mafuta yanaletwa kuniteketeza sijawahi tamani au kushika kitu cha mtu au kusogea mahali mwizi anapigwa.

Kipindi Niko advance nilikutana na jamaa flani akanipeleka kwa mganga kutafuta utajiri yaani kwenye safari ya kupigana na umaskini nimesha pitia mengi siwezi kuandika hapa yote.

Kunakipindi mama aliniambia kunapesa anatarajia kupata anataka ajenge nyumba nyingine ndogo. Basi kwa kua tulikuwa na eneo kubwa ikabidi nianze kupiga tofali maana nilikuwa nimeshakuwa mtaalamu, nikamuita rafiki yangu tukapiga tofali kama buku 4 ,kisha tukazichoma, kisha tukaanza kusomba mchanga wa barabarani ule ambao mvua ikinyesha inausomba waliokaa kijijini watanielewa.

Daa nilipomaliza kumbe mama alikuwa na 130000 tu fundi alipokuja akasema hii pesa inatosha mifuko 3 ya cement na mawe hata pesa ya ufundi haitoshi. Ikabidi fundi aseme msingi watajengea matope. Wakimaliza kwenye kuweka matofali ndio watumie mchanga na cement na ili cement itoshe inabidi mfuko mmoja waweke karai za mchanga 100.

Hiyo nyumba ilijengwa haikufika hata katikati resources zikawa zimeisha
Ukweli kwa msoto na kazi nikizokuwa nimefanya lakini hakuna kinachobadilika nikaona bora nijaribishe shuleni hiyo ndio sababu iliyonifanya kuvuka kidato cha 4.

Mwaka 2016 ndio nilianza mwaka wa kwanza chuoni nakumbuka hapo nilikuwa sina ndugu yoyote au rafiki aliyeko dar nakumbuka nimefika ubongo terminal pale nililala siku mbili kwenye lile jengo la wageni. Sometimes unakuta mtu anapiga story alienda kutafuta maisha sehemu fulani akafikia kwa ndugu anaanza kulalamika mala shemeji anamtesa , huwa na shangaa sana angejua kuna watu hawana hata mahala pakufikia

Niseme tu toka nimeanza masomo hiyo 2016 sikuwahi kukanyaga home japo kiukweli nilikuwa na fight kila njia pesa na tuma home nilikuwa nawatumia pesa mfululizo hadi nikawa nawaza kiukweli hapa nyumbani shida zile ndogo ndogo hazitokuwepo tena.

Nakumbuka mwaka jana baada ya kumaliza masomo baada ya kuangaika Ilala boma kuuza karoti, kufanya vibarua kadhaa nilipiga dili flani nikapata million 10 niliandika uzi humu nilipata ushauri kwa watu tofauti tofauti pia kukutananao jinsi gani nitazalisha hiyo pesa mmoja aliniasaidia eneo la biashara kubwa tu store ya nafaka japo nilimlipa kiasi flani lakini ilikuwa ni kunisaidia tu.

Kuna rafiki yangu anaitwa J4 aliniongezea kama million 3.5 maana pesa ile ilikuwa haitoshi kuleta mzigo wa kutosha. Baada ya hapo mwaka huu mwezi wa kwanza niliongea na jamaa flani hivi alikuwa anatokea kanda ya ziwa akaniambia ndio msimu wa kupanda mahindi pia maharahge nikamwabia jamaa yangu J4 tuchange pesa kidogo tukalime maharage hata heka 5 yakikomaa tunaleta town.

Basi kweli nilifanikiwa kwenye store nilimuacha J4 aangalie mimi nikaenda shambani japo sikulimaa kitaalam lakini nilikamilisha kila kitu. Wakati namaliza ndio Covid 19 ilikuwa imeshika kasi.

Nilimpigia mama tukaongea akaniambia kabla hujarudi dar upite nyumbani utusalimie kwani hapo ulipo ni karibu sana asee siku nimefika nyumbani ndio nilijua kwanini wachaga wanaongoza kujenga kwao.

Yaani nilikuta hakuna kilichobadilika sisemi kama niliwalaumu lakini nilikuta hali ni ileile getto nililokuwa na kaa liko vilevile mdogo wangu mdogo wa kiume ndio analala japo baba tofauti.

Sinaga maisha ya kujilinganisha lakini ile sehemu watu walikuwa wamejenga sii majumba ya kifahari lakini nyumba za kawaida umeme wa rea mji wote usiku unawaka kasoro kwetu lile jambo lilininyima raha nikiangalia mfukoni sina kitu nilikuwa kama na 220000 pesa zote ziko kwenye mzunguko.

Kesho yake nikampigia J4 simu nikamwabia katika mauzo yote msiagize mzigo mwingine tusikilizie kwanza hili janga la corona halafu kwenye pesa hizo unitumie Million 1

Kiukweli ndani ya nafsi yangu nilikuwa nimeshaingiwa na tamaa tena yenye uchungu mkubwa ndani yake kwa nini mama anakaa kwenye nyumba kama banda la kuku .kweli ndani ya dakika chache jamaa akanitumia hiyo pesa.

Ukweli ndani ya moyo wangu hata baadhi ya wadau humu baada ya kupata ile million 10 waliniambia achana na maswala ya forex na gambling lakini kwa ile akili na mazingira ya pale home nilisema hakuna sehemu nitapata pesa za fasta fasta kama kwenye forex nikajikuta tayari nimeshavunja masharti niliokuwa nimejiwekea kuwa sitrade tena forex.

Mawazo yangu nilisema naweka dola 100 napandisha hadi 500 kisha naanza kununua material ya ujenzi kidogo kidogo kweli niliweka dola 100 kama 240000 kupitia safaricom asee kutokana na tamaa siku ile ile pesa yote ikaenda nikipigwa.

Nilihisi kuchanganyikiwa ikabidi niweke tena dola 200 kama 500000 yaani siku moja ile million niliotumiwa Mpesa ikabaki inasoma kama 250000 daa nikaendelea kutrade zile dola 200 zikaenda hadi negative 120 nikataka nifunge loss nibaki na dola 80 nikasema kama yote inaenda iendee.

Nifupishe tu ile dola 200 ilirudi kwenye profit niliendelea kutrade zikafika hadi dola 1000 ,zilivyofika 1000 nikasema chochote nitakachopata faida zaidi ya hapo hata kama ni dola 2 natoa nanunua kifaa.

Nilinunua mabati 50@18500=925000
nikanunua mbao 50,3x2@2500=125000
mbao 40,4x2@3500=140000
Misumari ya bati+ mbao 60000
Cement 50@19000=950000
Chokaa 10@12000=120000
Mchanga 3@75000=225000
Mawe 2@70000=140000
Nondo 10@18000=180000
Nyavu mita 10@150000
Vifaa vya umeme 450000
Gharama kuvuta umeme rea 160000
Ufundi +kibarua 270000
Fremu za milango +madirisha 320000
TV +Dstv 280000+70000=350000
Milango =380000
Jumla inakuja kama 5000000 lakini ni zaidi ya hapo
Kuna vitu vingine vidogo vidogo nimesahau maana vitu vingi nilikuwa nafata nusunusu mfano gharama ya ubebaji
Kiukweli nilikuwa sijui kama ujenzi unakula pesa hivyo maana nilikuwaga sijui gharama hata ya kipende cha msumali


Kutokana na kubana matumizi ilibidi nifanye kazi na mimi kama kibarua yaani nilipiga kazi kweli kweli sikutaka utani wala kuangalia mtu

Siku ya maumivu kwangu tulikuwa tunajenga mimi napiga kibarua kisha naenda kuangalia simu asee kidogo tu account iungue ila nashukuru mungu trade zote zilikuwa zinakuja upande wangu.

Siku ya mwisho tuliokuwa tunamaliza ujenzi nilipata profit ya dola 300 zaidi ya laki 6 nikafunga trade nikatoa pesa nikabaki na mtaji kama dola 1000 nataka nikuonyeshe forex ilivyohatari usiku kwenye saa mbili nikaopen trade ilikuwa ijumaa nakumbuka nikalala na neg 700 j3 soko kufunguliwa pesa yote ikachomeka.

Nikarudisha tena ile dola 300 niliyokuwa nimewithdraw ndani ya hiyo wiki nikapata faida ya dola 900 .

Hadi muda huu bado na hiyo account inadola 1000 naendelea kutrade ikiungua basi maana mwezi huu nimeingiza faida ya dola 22000 kama million 5

Sishauri mtu atrade kwa kufata mkumbo eti kisa mimi nimepata faida fulani unaweza ingiza dola 1000 zikaungua siku hiyo hiyo
Ninamengi ya kusema ila ngoja niishie hapa

Hapa chini ni picha za ukuta wa nyumbani hapo awali ulikuwa umechakaaa tukabomoa wote, nikiwa kibarua, baadhi ya vifaa nilivyonunua, Profit nilizotengeneza, loss nilizopata, account ninayotrade sasa hivi,
View attachment 1456772View attachment 1456776View attachment 1456778View attachment 1456780View attachment 1456781View attachment 1456782View attachment 1456786View attachment 1456790View attachment 1456791View attachment 1456792View attachment 1456793View attachment 1456796View attachment 1456805View attachment 1456806View attachment 1456807

Sent using Jamii Forums mobile app
Tangazo limekata vizuri
 
Wabongo bwana, hawaishiwi maneno

Jamaa kaleta uzi wake wa kuonesha achievement yake aliyokuwa anaitamani maishani mwake na akaweka na source ya income alikoipata lakini mnaona kama anajipigia promo

Angeleta huu uzi bila kuonesha katoa wapi pesa wakati bado kinda tuu najua mngemuuliza mshiko katoa wapi wakati kamaliza chuo juzi tuu

Forex sio illegal business. Hata angekuwa anajipigia promo kwani tatizo liko wapi? Forex sio mbaya ila wabaya ni watu wanaoitumia kuwatapeli watu!

Hivi mnadhani kwa situation ya maisha ya bongo sasa jamaa asingekomaa na forex biashara gani ingemsaidia? Ajira zenyewe hamna, na hata angekuwa na ajira pia angesubiri miaka kadhaa ndipo ange-accomplish hiyo goal yake!

Acheni mawazo mgando wabongo, open your brains ili muwe na exposure ya mambo mengi.

Mkuu jooohs we komaa na life lako achana na snitches wa humu ndani
Unforgetable

Manners Maketh Man
 
Wabongo bwana, hawaishiwi maneno

Jamaa kaleta uzi wake wa kuonesha achievement yake aliyokuwa anaitamani maishani mwake na akaweka na source ya income alikoipata lakini mnaona kama anajipigia promo

Angeleta huu uzi bila kuonesha katoa wapi pesa wakati bado kinda tuu najua mngemuuliza mshiko katoa wapi wakati kamaliza chuo juzi tuu

Forex sio illegal business. Hata angekuwa anajipigia promo kwani tatizo liko wapi? Forex sio mbaya ila wabaya ni watu wanaoitumia kuwatapeli watu!

Hivi mnadhani kwa situation ya maisha ya bongo sasa jamaa asingekomaa na forex biashara gani ingemsaidia? Ajira zenyewe hamna, na hata angekuwa na ajira pia angesubiri miaka kadhaa ndipo ange-accomplish hiyo goal yake!

Acheni mawazo mgando wabongo, open your brains ili muwe na exposure ya mambo mengi.

Mkuu jooohs we komaa na life lako achana na snitches wa humu ndani
Unforgetable

Manners Maketh Man
Ndio maana hapo juu kabisa nikasema ukiishi kwa kuangalia eti nani anasema nini umekwisha wewe fanya unaloona kwako ni sahii . Kikubwa huwa na heshimu sana muda ndio unatoa majibu sahii

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom