Nimeelewa ni kwanini mfalume Suleiman aliomba hekima na si kitu kingine chochote

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,477
2,000
Hekima ndio kila kitu katika uongozi na si kupenda kusifiwa au kutukuzwa. Mfalume Suleiman alipoomba apewe hekima ni wazi alijua nini maana ya uongozi na kutumikia watu.

Hata katika dunia ya leo bado tunawahitaji sana viongozi aina ya Mfalume Suleiman maana wengi wao leo wamelewa madaraka na kusahau hata walikotoka!!

Inasikitisha.
 

Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,348
2,000
Akina Obama waliandaliwa kwa miaka mingi sana kuja kuwa viongozi na hawakuja kama mvua.
 

Tetty

JF-Expert Member
Jan 6, 2012
26,386
2,000
Ndiyo sababu anasema aombewe lakini hatujui aombewe nini?Alitakiwa kusema.niombeeni Busara na Hekima.

Tunapiga vita Rushwa halafu unaenda kununua Madiwani na wabunge wa Upinzani, akili ya kuku kabisa.
 

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,821
2,000
Ninaweza nikawa nakosea ila kwa upande wangu unaposema hekima unakua na maana kubwa sana kimaadili na kiutu.
Okay mfalme aliomba hekima lakin embu tujiulize hekima yake aliitumia sawa au alikosea?
Kwanza baada ya kupewa hekima mwishowe alimwacha Mungu nakuanza kuabudu miungu.
Pili alilala na wanawake wengi sana, wanawake 1000 walikua wanajulikana acha wasiojulikana.

Sasa tunajiuliza ni hekima gani huyo mtu aliyonayo? Japo hakuna aliekamili basi ni bora tujichunguze mara mbili mbili kabla ya kuanza kulaumu.

Pamoja na yote hayo mfalme suleman pia alifanya maengi mazuri tuu.
 

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,821
2,000
Kwangu mimi tatizo sio la mtu mmoja bali ni system nzima ya nchi, kwanzia watu wake, watumishi wa serikali, viongozi wa kisiasa, ulinzi yani kwa kifupi tuko hapa tulipo kwa sababu yetu sisi wenyewe.

Embu fikiria taifa kama Misri lilivyokua vizur ghafla likaingia kwenye vita ya wenyewe baadae wakarekebisha makosa na sasa hali inarudi kwenye hali yake na awali na pengine bora zaid.

Hivyo shusheni lawama kwenu wenyewe, upanzan na chama tawala sisi wote ni nuksi wala hamna lolote.

Akitokea mjanja mnaanza kumuaribu tena mwishone mwishowe hali inakua vile vile.

Nawahakikishia watanzani mkipenda Tanzania ya kisasa jitizameni mara mbili, mjitathmini muangalie wapi mnakosea na mnasahihishaje makosa vinginevyo hali itakua hivi tuu hadi Yesu atakapokuja.
 

Kumbila medi

Member
May 31, 2017
99
125
Ndiyo sababu anasema aombewe lakini hatujui aombewe nini?Alitakiwa kusema.niombeeni Busara na Hekima.

Tunapiga vita Rushwa halafu unaenda kununua Madiwani na wabunge wa Upinzani, akili ya kuku kabisa.
Anataka akawe prezida wa malaika mbinguni ndio maana anataka aombewe au umesahau ile speech yake? Anataka akawe Angel's prezida huko mbinguni.
 

Mgirik

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
12,805
2,000
Kuna watu ktk dunia hii hata ufanye jema gani lakn watazidi kukuchukia tu..
Hao tunawaita chui waliovaa ngozi ya kondoo..

Kuna kipind hata mfalme suleman alitumia maamuzi magumu ili haki ipatikane..
Mfano ni wale akina mama wawili waliokuwa wanagombania mtoto . mfalme aliamua mtoto akatwe kat kati vpande viwili ili kila mtu apate haki yake na hatmaye mwenye mtoto halisi akajulikana
 

motonkafu

JF-Expert Member
Dec 2, 2015
1,024
2,000
Ninaweza nikawa nakosea ila kwa upande wangu unaposema hekima unakua na maana kubwa sana kimaadili na kiutu.
Okay mfalme aliomba hekima lakin embu tujiulize hekima yake aliitumia sawa au alikosea?
Kwanza baada ya kupewa hekima mwishowe alimwacha Mungu nakuanza kuabudu miungu.
Pili alilala na wanawake wengi sana, wanawake 1000 walikua wanajulikana acha wasiojulikana.

Sasa tunajiuliza ni hekima gani huyo mtu aliyonayo? Japo hakuna aliekamili basi ni bora tujichunguze mara mbili mbili kabla ya kuanza kulaumu.

Pamoja na yote hayo mfalme suleman pia alifanya maengi mazuri tuu.
Aliekwambia kulala na wanawake wengi ni dhambi ni nanu, mbona adam alilala na nwanamke mmoja tu na akaadhibiwa pakubwa tu
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,933
2,000
Kama ni Kweli kuwa kulifanyika hila na siasa chafu wakati wa campaign hadi uchaguzi kiasi pengine cha kuleta Shaka Kwenye matokeo ya uchaguzi basi yanayoonekana yaweza kuwa Ni matokeo Yake ! Mwenyezi Mungu anaheshimu sana swala la upigaji kura ktk kumpata kiongozi anayekubalika na wengi! Maandiko yako dhahiri, imeandikwa Kwa kura Watu huondoa mabishano! Labda aombe Rehema na toba na wenzio! Ndo maana hata hata swala la kunia mamoja miongoni mwao ni mashaka! Kibali machoni pa wengi kinakosekana pamoja yeye mwenyewe kuona Mbona anajitahidi lakini haeleweki ? Mwenyezi Mungu ni Mkuu sana !
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,933
2,000
Halafu kanuni iko hivi haitoshi kumuomba Mungu toba na msamaha lakini yatupasa pia kuanza kuwaomba toba na msamaha binadamu wenzetu tuliowakosea hiyo Mungu anaheshimu sana, imeandikwa hata sadaka usitoe hadi upatanane na uliyemkosea!
 

Akilinjema

JF-Expert Member
Aug 9, 2016
5,933
2,000
Unakuta Mtu amemkosea Mtu lakini hatafuti kumwomba msamaha Ila eti anakazana kumwomba Mungu Rehema na toba hiyo na Sawa lakini Mungu ameagiza tuombane msamaha sisi Kwa sisi pia , imeandikwa "tafuteni kuwa na amani na Watu wote na huo utakatifu ambao hakuna atakae mwona Mungu pasipo huo" Ebr! Anaposema tutafute amani na Watu wote anamaana kubwa sana Mungu! Yani "Watu wote" yani hapo ni bila kujali dini, Rangi , Kabila , itikani za vyama, n.k
 

Mhakiki

JF-Expert Member
Dec 19, 2012
1,783
2,000
Mkuu angalia na fuata asemacho sio afanyacho.
Hawa viongozi hunena tu kama no la kudhuru back wa chini hutenda bila kujali athari zake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom