Nimeelewa kwanini baadhi ya nchi katika janga hili la corona wamepunguza mishahara na marupurupu ya viongozi wa kisiasa

Itoye

JF-Expert Member
Sep 29, 2017
531
1,024
Wakuu Salaam,
Baadhi ya nchi waliamua kupunguza mishahara ya viongozi wa kisiasa ktk nchi hizo, mara ya kwanza sikuelewa vizuri hiyo 'move' nilijiuliza hawa viongozi wako wachache sana hiyo fedha inayopatikana baada ya wote kukatwa mbona ni kidogo sana.

Lakini sasa nimeanza kuelewa pamoja na sababu za wazi walizotoa pia lengo jingine ni kuwapatia hawa viongozi 'first hand experience' ya madhara ya janga hili, ili wanapomsikia mtu analalamika hali imekua ngumu, mahitaji hayapatikani kama hapo kabla basi waelewe vizuri maana na yeye limempata mfukoni kwake, hivyo hata matamko wanayotoa au maelekezo yatakua yanaeleweka na hata utendeji wao hata baada ya corona utakua wa uhakika ili hali irudi kuwa normal haraka.

Jaribu kupiga picha kwa kiongozi ambaye tangu janga limeanza anapata mshahara na maposho na marupurupu yake kama zamani yaani maisha yake yako vile vile kilichobadilika ni yeye kuvaa barakoa tu, hivi ukimwambia masuala ya 'stimulus package' kwa biashara au sekta flani hadi aje achukue hatua au aelewe kwa nchi zetu za dunia ya 3, itachukua miaka.
 
Back
Top Bottom