Nimedukua simu ya mke wangu, Simu zetu zina siri nzito, nakufa mimi

KAFA.cOm

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
1,301
2,000
kuna application unadownload tu, kama unatumia android au ios, zinaweza kukuletea sms zote, call logs, zingine zinarecord mpaka calls unaweza kuskiliza baadaye, inakupa geolocation ya simu kwa wakati husika, unaweza kuwasha microphone ya simu yake hata kama ameiweka mezani ukaskiliza maongezi yanayoongewa offline bila yeye kujua, unaweza kuwasha camera ukaona kila kitu, unaweza kuangalia picha alizopiga, unaweza kukamata login details za kwenye mitandao ya kijamii na sehem zingine, kiufupi simu yake unakuwa na access nayo wakati wowote inapokuwa on bila yeye kujua, na hiyo application wala haionekani ukishaiweka inapotea kabsa!
uongo hmna app ya aina hii
 

shija jr

Member
May 21, 2016
54
125
kuna application unadownload tu, kama unatumia android au ios, zinaweza kukuletea sms zote, call logs, zingine zinarecord mpaka calls unaweza kuskiliza baadaye, inakupa geolocation ya simu kwa wakati husika, unaweza kuwasha microphone ya simu yake hata kama ameiweka mezani ukaskiliza maongezi yanayoongewa offline bila yeye kujua, unaweza kuwasha camera ukaona kila kitu, unaweza kuangalia picha alizopiga, unaweza kukamata login details za kwenye mitandao ya kijamii na sehem zingine, kiufupi simu yake unakuwa na access nayo wakati wowote inapokuwa on bila yeye kujua, na hiyo application wala haionekani ukishaiweka inapotea kabsa!
Ndo app gani hiyo mkuu hebu tujuzane
 

kweleakwelea

JF-Expert Member
Nov 29, 2010
3,058
2,000
6.ukiona mke wako anamhurumia saana mwanaume fulani apatapo tatizo yani yupo tayari kumsaidia hata fedha za ndani kulitatua tatzo lake ujue anampenda kimapenzi huyo mtu.....hii ilitokea pia katika huu mchakato.


DAH MKUU HII UKWELI.TUPU....YAANI WE ACHA RU
 

Simuchi

JF-Expert Member
Jun 24, 2016
275
250
Unajua nilikuwa natizama post tuu nikaona hii post unanifanya nisilale daah ila pole sana mitihan tumeumbiwa binaadamu kaka kama mm huyo mke ningemuacha hafai maana hao watu wasaliti ukija ktk dini ya kiislam watu kama hao hukumu yao kifoo kwasababu walidhamiria na sibahat mbaya ila uamuzi unao ww kama umeamua kumsamehe msamehe kwa moyo wote ningekushauri uhame hiyo sehemu ulipo kama unakaa temeke amia kinondoni itakusaidia kusahau maana hiyo itakuwa kashfa mtaan upitapo
Aisee Mimi nilitafuta hii thread siku 3 mpaka nikaikuta mwanzoni nili subscribe kumbe nilikua sija login nilivyofungua nikakuta aipo. Pole sana kaka
 

Bulah

JF-Expert Member
Aug 19, 2011
234
225
kuna application unadownload tu, kama unatumia android au ios, zinaweza kukuletea sms zote, call logs, zingine zinarecord mpaka calls unaweza kuskiliza baadaye, inakupa geolocation ya simu kwa wakati husika, unaweza kuwasha microphone ya simu yake hata kama ameiweka mezani ukaskiliza maongezi yanayoongewa offline bila yeye kujua, unaweza kuwasha camera ukaona kila kitu, unaweza kuangalia picha alizopiga, unaweza kukamata login details za kwenye mitandao ya kijamii na sehem zingine, kiufupi simu yake unakuwa na access nayo wakati wowote inapokuwa on bila yeye kujua, na hiyo application wala haionekani ukishaiweka inapotea kabsa!
Nipe jina la hii application
 

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
10,669
2,000
Habari ya leo wakuu

Leo napenda kuwapa kilichotokea kwenye ile thread kuhusu kufanya udukuzi kwenye simu ya mke wangu.

Tujikumbushe kidogo kwa wale ambao hawakupata ile thread. Ni hivi mimi nipo DSM na mke wangu yupo korogwe Tanga.

Tulikuwa tunaishi wote hapa DSM kabla hajapata kazi kisha akapata kazi na kuelekea huko.

Kabla hajaelekea huko Tanga hapa jirani kuna baba mmoja ni mlokole anavojiweka mwenywewe na ana mke na watoto wakubwa wa kwanza yupo chuo.

TULIVYOISHI
Huyu jamaa akawa yupo jiran na mke wangu, yan kumpigia simu na kushauriana mambo kadha wa kadha hasa ya kanisa kwa vile nilimwamini mke wangu sikuwa na wasi wasi...na kikubwa zaidi akawa anampigia wakati wowote akiwa na suala hasa kikanisa...
ikafika stage wife akaondoka akaenda kikazi tanga...
akiwa tanga nilinunua smart phone na kumpelekea....
kwenye ile smart phone nikaweka program ya kunitumia taarifa zake ikiwemo msg na calls zote ziingiazo na kutoka kwenye ile simu...


ILIVYOANZA

Huyu jamaa alikuwa anajifanya mpole na kuhitaj kuwa karibu na kumchukulia kama family friends....yan familia yangu ikiwa na shida gari lake linatumika na familia yake ikiwa na shida kama wakilihitaj gari linatumika.

Tukiwa pamoja na huyu jamaa namheshimu sana as family friend na naye akawa anaonyesha heshima ya juu sana nikamuona ni mtu mwema kwa kizazi na maisha ya watu leo kumbe anakuja kunitenda kwa kutembea na mke wangu na kuniachia kovu ambalo sijawahi kuhisi maumivu yake.

Ni bora utendwe na mtu alie mbali nawe kuliko yule uliemwamini na kumheshim sana halafu anakuja kumvua mkeo chupi, hiki ndo nikikumbuka nalia kidume mimi.

Hapa nitaeleza dalili za mwanzo kati na hadi mwisho wa kuja kukamatwa kwa huyu alieniliza kidume mimi.

Lengo la hii thread nitaomba ushauri wenu nitarudije normal na pia nimfanyeje hawa wezi wote mke na mme.

Nilivyompa ile simu ikiwa tayari ina hiyo application nikalala asubuhi yake nikaondoka kurudi DSM
ile nipo kwenye dar express mida ya saa tano nikaletewa notification kwamba kuna mu anangea na wife.

Kucheki namba ni jirani yangu, nikapotezea nikaendelea na mambo mengine mida ya saa saba mchana notification simu inatumika kucheki ni jamaa jirani, saa kumi notification kucheki ni jamaa saa kumi na mbili notification kucheki ni jamaa saa moja na saa mbili notification kucheki ni jamaa tu.

Machale yakanikuna kuwa kuna kitu hapa.

Asubuhi yake mapema jamaa kampigia tena ilipofika saa 4 wife alienda church kwa hiyo alikuwa amezima simu jamaa kamwandikia messge mbona hupatikan nimekumiss sana.
Hapo alarm ya kichwa ikapiga kwamba kuna jambo sio dogo hapa.

Ile wife ametoka kanisani akawasha simu basi muda huo huo nikaletewa notification kwamba jamaa anaongea na wife.

Walivomaliza kuongea wife akanipigia simu akanipa hai tukaagana akakata simu.

Baada ya kukata simu wakapigiana tena na tena yani jamaa anampigia wife kila baada ya saa moja au mbili.

*****TUENDELEE*TULIVYOISHI
Huyu jamaa akawa yupo jiran na mke wangu, yan kumpigia simu na kushauriana mambo kadha wa kadha hasa ya kanisa kwa vile nilimwamin mke wangu sikuwa na wasi wasi...na kikubwa zaidi akawa anqmpigia wakat wowote akiwa na suala hasa kikanisa...
ikafika stage wife akaondoka akaenda kikazi tanga...
akiwa tanga nilinunua smart phone na kumpelekea....
kwenye ile smart phone nikaweka program ya kunitumia taarifa zake ikiwemo msg na calls zote ziingiazo na kutoka kwenye ile simu...

hapa mwanaume nimeamua kuweka ukweli wangu kama yamenikuta yaweza kukuta na ww naomba mzahamzaha sipendezwi wakuu

*************

basi vile nilivokuwa napata zile notifications mara kwa mara za meseji na calls kwa jamaa kwenda kwa mke wangu nikashindwa kuvumilia ikanibidi niende korogwe kwa wife...nikampigia simu kwamba nakuja tanga, wakati nakata simu ikaingia notification kwamba jamaa anaongea na wife kumbe wakatumia wakati huu kuambizana kwamba nipo njiani naekekea tanga, hivo zile notification za mawasiliano yao zikapungua kuja kwangu....

Nimefika tanga nikamkuta wife yupo normal tu na simu yake ipo loose tu juu ya meza....basi akanipokea pale kwa bashasha yani full tabasamu (dont trust a woman) akaandaa chakula tukala tukalala....
usiku mida ya saa 3 usiku ikaingia txt kwenye simu yangu nikaichukua ile msg nikaisoma ilikuwa ya kikazi nilivomaliza kuisoma nikairudisha simu kwenye dressing table...hapo nikaona wife amenyanyua kichwa akaniuliza msg ya nan nikamjib ya kazini akanyanyuka kuichukua simu yangu nikaidaka na kukataa aiguse sababu kubwa nina hasira za kimia kimia moyoni kwamba najua nn kinaendelea ila najipa muda. .akanituhumu pale kwamba msg ya mwaamke ndo maana nakatalia aione.

akanijibu jibu moja kwamba mm sio mwaminifu ndo maana nakatalia simu akadai kwamba mbona yeye simu yake ipo free na kama nataka nikae nayo hata siku nzima hamna kibaya kitakachoingia (hili jibu hutolewaga na wasichana na nilitumia kuliamini sana kumbe sio) kuweni makini utakaa na simu ya mkeo au mchumba na still akakucheat....basi tukakwaruzana pale kidogo kisha tukalala.


asubuh nikaamka nikarejea dsm
hii siku nzima ilipita sikupata notification ya mawasiano yao.
kesho kutwa yake nikaendelea kupata notification za mara kwa mara kwamba wanaongea na msg za hapa na pale yaani wanaongea hadi saa 4 usiku sometime.
nikashndwa uzalendo nikaanza michakato kila anapomaliza kuongea nampigia simu namuuliza ulikuwa unaongea na nani akawa anataja ndugu zake na anakupa hata sababu walichokuwa wanajadili.....nikawa namkubalia kwa shingo upande kwan notification za txt zote na calls zote anazopata nazipata..
ipo siku tena nikaamuliza akawa mkali sana kwamba iweje anipe taarifa za kila anaempigia je mbona mm simpi.
nakumbuka ilikuwa jumatano nikaletewa txt as notification toka kwa jamaa anamtaka wakutane ijumaa wasex.....jamani jamani jamaniiiiiii inauma asikuambie mtu.....nilivuja jasho sijapata kuona nikakabwa na kitu kooni nikavumilia.
wife akamjibu sawa karibu hata mm nimemiss mambo yako...

.hiii jumatano sikulala kabisaa kwan walizidisha muda wa kuongea walichati sana msg za kawaida na kijinga......kipindi hiki wanaendelea wife alikuwa ananipigia sim kama kawaida tunaongea ila alinote sipo sawa akaniuliza kuna nn nikamjib hamna shida...niliamua kuondoka dar saa 11 jioni alhamisi kwenda korogwe ili kuliwah siku ya tukio yani ijumaa wanapokutana.
nimefika korogwe ilikuwa kama saa 3 usiku niliwaza sana kabla sijaenda nyumbani kwa wife
niliwaza nijifiche ili kesho niwakamate
niliwaza je nikiwakamata kesho nn kitatokea
niliona jibu lepesi ni kuwaua wote
*******************************

hiyo alihamisi jioni nikakodi chumba korogwe nilale...ila usiku saa 4 hivi nikahisi sipo sawa kabisaa kila kitu nakiona kichungu..
nikawaza bunduki sina, panga sina, je hawa hiyo kesho nitawauaje? je wakishaingia gest mi nae nikaingia afu nikakute wamemaliza kufunga mlango itakuaje? je zikianza purukushani za kutaka kubomoa mlango na mhudumu akawaomba watu msaada kwa kupiga kelele si watanishika na jamaa atakimbia..
m
niliwaza sana pale gest nikiwa kitandani, wazo likanijia kwamba sitapata hata tone la usingizi pale ni bora nimfuate wife nianze nae kwanza kupata ukweli...ile saa tano usiku nikapata tena notification wanaongea hasira zikazidi nikaamka kumfuata nyumbani kwake hapo korogwe saa 6 usiku nagonga kwa wife na inaonekana alikuwa hajalala..

NILIPOFIKA KWA WIFE
kwanza alishangaa iweje umekuja usiku hivi...nikamwambia nilikumiss na ni suprise yangu kwako.....nikajikaza sana kidume nisioneshe hasira.

NOTABLE EVENTS
Nilipofika ndani nikakaa kitandani nikavua viatu na soksi nikapanda kitandani sikuvua suruali wala shati coz nilijua hapatalalika,
cha kwanza wife akaonyesha kuhamaki kidigo afu akapotezea
simu yake ilikuwa juu ya dressing table tena kwenye chaji kabla hajaenda kuniandalia maji ya kuoga bafuni nikaona anaichomoa kwenye chaji na kuihamishia kwenye begi la nguo juu lilikuwa mwisho wa kitanda upande wa pili....
nikaamuliza mbona unatoa simu chaji akajibu imejaa..
nikamuuliza mbona unaihamisha akajib nimeweka vibrate kwa hiyo hapo inaweza vibrate ikakudisturble na pia ikadondoka.
nikamwambia wakat unaenda kuniandalia maji naomba niicheze chezee hapa hizo games zake.
akanipa ila hana aman akaelekea bafuni.

KWENYE SIMU
Cha kwanza nilicheki txt zote zimefutwa japo mm ninazo kwenye simu yangu.
cha pili calls zote zinafutwa akishamaliza kuongea nae hivo kwenye simu yake hakuna evidence yoyote japo mm ninazo kwenye simu.

Kamata mke wa huyo mchungaji na wewe!! Akileta ubishi mwanzoni mwaga ushahidi wote. Huyo mke wa mchungaji akigoma kabisa pamoja na ushahidi wote cheza na zile 18 na 12 zote zilizokuwa zinajilengesha kwako wakati ukitunza heshima ya mkeo. Au anza na housegirl, na kumpa promotion ya kufa mtu, mfano, kumfungulia akaunti benki na kujaza mifedha na ma-deposit slips kuyatuma kwa mkeo kama umekosea vile!! Achana na huyo mchungaji na huyo mkeo. Kuwaua ni kutaka murder case bila faida yeyote, na kuijiharibia maisha yako na kuwatia uzuni ndugu zako ambao wengine labda wanakutegemea na wanakupenda na wanataka uendelee kuwepo duniani kwa mujibu wa life expectancy yako.

Hesabu mkeo kama fedha uliyoporwa na majambazi - tafuta fedha nyingine.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom