Nimedokezwa na jirani kuwa mume wangu anatembea na mdogo wangu. Nianzie wapi?

Benokolongokonongose

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
213
0
Habirini za jioni.

Mimi ni mjasiriamali ambaye kazi zangu za kutafuta zinanifanya kuzunguka sana vijijini. Nyumbani mara nyingi napatikana jumanne na alhamisi tu. Tunaishi na mdogo wangu. Leo jirani yangu amenidokeza kuwa nichunguze kwa makini kwani mdogo wangu anatembea na shemeji yake. Naomba msaada kwani nimechanganyikiwa na hata sielewi nianzaje kuchunguza swala hili.

Hivi kwa akili ya kawaida mtu unathubutuje kumfanya shemeji yako?Dunia hii! Wenu BENOKOLONGOKONONGOSE
 

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,739
2,000
Dunia imebadilika dada yangu wala jambo hilo siyo la ajabu kama unavyofikiria ila kwa sababu ni mara yako ya kwanza kukumbwa na hii dhahama basi piga moyo konde!!

Kuthibitisha maneno ya Jirani yako basi uwe tiyari kuachana na huyo mmeo kama kweli kafanya hivyo,.

Pia jihoji maswali yafuatayo kabla hujamchukulia hatua!

1.Unampatia haki yake ya ndoa ipasavyo?

2.Je una mgogoro wowote na mumeo?


Jibu haya kwanza,..
 

Hornet

JF-Expert Member
Apr 29, 2013
19,620
2,000
Kwanza pole sana..binafsi sipendi kumchunguza sana mtu..
Ila nakushauri kama una moyo wa uvimilivu panga safari kama kawaida kisha uondoke na ufunguo mmojawapo..na urudi kabla ya siku uliyohaidi kurudi..kisha ufungue mlango hasa mda wa usiku kama yapo utayaona tu..
 

gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
8,853
1,500
Pole sana kwa yaliyokukuta...kama walivyosema wadau wengine panga safari kisha uzuke tu ghafla...wachunguze pia wakiwa pamoja wanabehave vipi kama kama chemistry utaona tu kuwa hawa wanakulana!!
 

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,808
2,000
BENOKOLONGOKONONGOSE..................

Aisee ID yako ndefu sana, hebu jaribu kuifupisha basi.

Kuhusu tatizo lako, chunguza naamini kwa mtu makini anaweza kugundua haraka maana mapenzi hayana siri, na ukigundua uje hapa kuomba ushauri tutakusaidia,

Anza na hilo kwanza.
 

mutant gene

JF-Expert Member
May 18, 2014
876
0
mkuhu pole sanah. hunatakiwa huhangalihe kwa huzuri sanah time hingine wanahongeha huhongo, hope humenihelewa mkuhu.
 

Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
37,502
2,000
Pole sana ila punguza presha,tulia utaharibu mambo.Chukua simu ya mdogo wako kwa kumshtukiza utajua ukweli;Kingine jitahidi kuongeza siku za kukaa nyumbani kulea familia.Siku mbili mme hazimtoshi utaibiwa kila siku.
 

Mkare_wenu

JF-Expert Member
Mar 11, 2011
1,716
1,500
Pole sana ila punguza presha,tulia utaharibu mambo.Chukua simu ya mdogo wako kwa kumshtukiza utajua ukweli;Kingine jitahidi kuongeza siku za kukaa nyumbani kulea familia.Siku mbili mme hazimtoshi utaibiwa kila siku.

wanakulana humohumo ndani sidhan kama hata simu inahusika
 

Mashaxizo

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
6,712
1,225
1 Usikurupuke na hata usioneshe kustukia chezo!

2 Hakikisha ukiingia mwezini (period/hedhi) uweko nyumbani! (Zuga unaumwa hautokwenda mihangaikoni) Usiondoke hadi ikaribie kuisha!

3 Hakikisha unaaga unaondoka kabla ya kumpa mbunye mmeo!

4 Usiondoke kweli, jitege japo kwa jirani! Hakikisha unaaminiwa umeondoka!

5 Timba home kimya kimya mida kama saa tano or sita usiku!
...
Hapo utathibisha yaliomo yamo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom