Nimedisco baada ya kukamatwa namfanyia mtihani Mwanafunzi mwenzangu

Tafuta Kazi Kwa wahindi , Upate hela ya kwenda kusoma kozi za OSHA, then katafute kazi viwandan au migodini. Over
 
Mtaa unahitaji ubishi sana, kama unayo spirit ya ubishi kukubali kuchekwa na kuanza 1 huku ukitoa mawazo ya uyatima unatusua ....Elimu uliyo nayo tayar ni advantage achana na vyeti kwanza...

Tafuta club/casino au manager sehem yyt ya starehe kubwa omba nafasi pale kaunta kama mhudumu wa pale pale cheza na kuhudumia huku ukiweka uaminifu wako,kuna hela sana na sehem zile watu wa hesabu wanatakiwa sana maana kuna wakati watu wanajaa wanahitaji huduma ya chap chap...


Nenda morogoro ulizia star park ni wapi, ukifika pale mtafute manager mwambie nimeelekezwa na MD Mbabe au Mbishi.,atanipigia simu nitakusaidia....hata sisi tumekuwa kiyatima ila tukaweka mapambano mbele bila kuangalia watu.
Star Park hiki kiwanja ni noma sanaaaaa... Juzi nilikuwa pale aisee hilo nyomi si la kawaida, kaunta karibia 4 lakini bado zinazidiwa, jamaa ametega vizuri sana...
 
Habari wanajamvi,

Natanguliza samahani kwa kuwapotezea muda ila nimeandika huu uzi kwa lengo la kuomba ushauri mimi ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu ndio nilikua namaliza ila nimeshindwa baada ya kufukuzwa chuo na sababu ni kumfanyia mwanafunzi mwenzangu mtihani wa sapp huyu rafiki yangu

Nimejuana nae toka mwaka wa kwanza na changamoto yake toka mwaka ule wa kwanza alikamatwa MATHEMATICS sasa yeye katoka HGL na hakua na msingi wa hesabu aliibebea toka mwaka huo sasa mwaka huu akaona lazima agraduate na njia pekee ni kumuomba mtu amfanyie

Tulienda Kariakoo kuchongesha ID ikafika siku ya mtihani akanipa niliingia kufanya nikamuonyesha examination invigirator ID akaingalia akaniruhusu nifanye kibaya baada ya kumaliza msimamizi akapata hofu akasema nimpe ID tena aiangalie ndipo nilipokamatwa na kupelekwa admission nilipigwa na walinzi mpaka nikamtaja mwenzangu

Sasa hukumu leo imetoka nimefutwa chuo na mimi ni yatima sina wazazi yaani nimesomeshwa na serikali nilipata boom %100 na o-level ni taasisi za dini ndio zilinipa msaada wa kunilipia elfu ishirini ya ada na vifaa vya shule hapa

Nimechanganyikiwa sina hata cha kufanya nahisi dunia imenielemea naombeni ushauri wenu tafadhali
Ulipoona elimu Ni ghali ukajaribu ujinga.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom