Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.

Huyu jamaa angu ni kama ndugu kabisa, tulikuwa na urafiki unaovuka mipaka, the guy was so deep na alikuwa Loyal yaan ni rafiki yule wa haswa haswa, rafiki ambae tumeshibana na tunaelewana mno mno wazee.

Hapa kati wakati Project inaendelea kuna wakati tuligombana na wabongo ambao walikuwa ni mamluki kwenye kampuni ilo la wa asia, huyu mshikaji wangu ndio aliwazingua sana baadae nikaingilia kati tukali-solve ilo tatizo na tukawa peace tena.

Sasa kuna wakati nilisacrifice kazi zangu za nje kibao ili tuisimamishe hii project sababu at the end of the day tulikuwa tunapata faida ya milion 20+ na tuko mtu mbili tu, so nikiwa na vimeo vingine nje (nna kazi nyingine nje tofauti na hii) nawaachia watu wengine wanifanyie kwa niaba.

Long story short, project iliisha salama sasa tukawa tunaanda bills na documents zingine ili wa asia watulipe hela zetu, so mshikaji wangu amesomea haya mambo ya uhasibu so ikawa kazi yake kuandaa then mwisho wa siku tupeleke na tukiwa tume attach na account zetu za malipo, mie nikapata kazi (kama nilivyosema nina kazi nyingine nje ya project) ambayo ilikuwa inanilazimu niende Dodoma kuikamilisha siku hiyo.

Mazee huyu rafiki angu ameshirikiana na wale wabongo wenzetu kwa wa asia wamempa hela yote huyu rafiki na sijui makubaliano yao au walipeana shingapi ila ndugu rafiki amekimbia na hela zote na hajulikani alipo, too sad hela alipewa cash (imagine) na mafacilitator ni hawa wabongo wenzetu wa kwa waasia. Jamaa hayupo popote ndani ya mji huu wa Dar.

Bado napambana kumpata na nimeshachukua hatua kubwa ya kumtafuta popote alipo ndani ya nchi hii, ila nimejiuliza maswali mengi sana na ambayo yamepelekea leo siku ya tano tunaenda sipati usingizi kabisaa na kila saa moyo wangu unauma na kuumwa kama vile kila siku naumizwa upya.

1. Ni kitu gani kimempata huyu ndugu yangu? Hustles zote zile tukiwa nae hakumbuki? Hakumbuki namna alivyokuwa irrelevant kwenye hii project na namna alivyochangia padogo sana kiasi hata asingekuwepo mradi ungesimama japo yeye ndio alilileta ili tenda? Why amesahau nafasi yake kwenye hili?

2. Ubongo wa mtu mdhulumati hua unawaza nini kichwani? Yaani future yake hua anaiona vp? Anapata usingizi huko alipo? is he happy? for how long?

3. Unawezaje kumsaliti rafiki yako ambae yuko loyal kwako? Hizo ni akili gani na roho ya namna gani hio?

4. Kwanini watu wengi wanakosa ubinadamu na haki pale hela zinapokuja? Je ukichukua haki ya mtu unadhani na yeye hato react back?

5. Nimfanye nini huyu mtu? Mbona nna haki zote hata nikiwafuata wataalam wa radi kwenye hili hawatosita kunisaidia tena bila masharti! Je mdhulumati huko aliko kama atakufa au akipata matatizo ambayo akiyaona sio kawaida atafanya nini?

Mwisho kabisa, nimeumizwa sanaa na maamuzi ya ndugu rafiki na nimekwama sanaa ktk kipindi ichi hasa nikikumbuka ile sacrifice na hustles za days and nights na ningeomba nitoe angalizo tafadhali mtu kama hakuzaliwa na wewe usimwamini kwa namna ya aina yoyote ile sababu uliezaliwa nae atleast kuna sehemu unaweza kumkamata.
Duh!! Hongera sana hela zote lakini bado una nguvu hata kuandika, mimi nilidhulumiwa laki moja na nusu niliweweseka karibu mwezi wote...
 
Huyu na wale wabongo wengine waliniwai walikula njama, ni kipindi ambacho tunaanda bills na mie kuchomoka kidogo tu ndio chance wakapata hapo na nilichomoka ndani ya masaa 24 tu.
Huwezi kuwa na Rafiki wa milele wala adui wa milele, am sure huwezi kumkosa hata mmoja kati ya walioshiriki, tafuta mbongo mmoja unayehisi amekula nae njama mtie ndani mpe tu askari buku 5, jamaa ataeleza yote na ziada juu na kibongo bongo unaeza kukuta wanawasiliana bado.....
 
Huwezi kuwa na Rafiki wa milele wala adui wa milele, am sure huwezi kumkosa hata mmoja kati ya walioshiriki, tafuta mbongo mmoja unayehisi amekula nae njama mtie ndani mpe tu askari buku 5, jamaa ataeleza yote na ziada juu na kibongo bongo unaeza kukuta wanawasiliana bado.....
Fuata huo huo ushauri.

Pia Kama una usongo Sana hela yako tafuta mtu awe private investigator wako amsake Jamaa Hadi ampate mumfanyie ambush
 
Alikua ni kijana wa gheto tu maana alifukuzwa kazi akashuka sanaa kiuchumi na hii project ndio ilimpa walau nafasi ya pili, anapokaa nilifika na vitu alivyoviacha thamani yake haizidi au haifiki milioni moja.

What makes you think amekudhulumu? Je hudhani kuwa wale waswahili mliokuwa nao kwenye hiyo project wanaweza kuwa wamemdhuru? Jaribu kutafuta ukweli pengine hayupo duniani!!!
 
Aise pole, fanya kupeleleza kwa ndugu zake, ujue nini kimempata au yuko wapi, naamini wao ni rahisi kujua alipo. Usifanye maamuzi yeyote kabla. Ila Kama utapata uhakika jamaa yupo mzima wa afya tele, Ila ameamua kukuzingua, ua free ku take any action u thn it's okay for u! Ova
 
PI unataka kuingia kazini
666 chata nimekuita lakini hujaitika.

Hawa matapeli wanadhibitika vizuri tu
Screenshot_20210702-201435.png
 
Kuna mwamba humu aliwahi kutoa tangazo la kulaani kunyimwa haki na hakimu mmoja halafu akatoa na siku kadhaa za matazamio.......The rest is the subject which deals with past events.....
 
Hukusoma injili?
Samehe 7 mara 70...
Bado ana nafasi 489 za kusamehewa na wewe
 
Mkuu kwa kua hujajua bado kilichompata huyo rafiki wako naomba tuliza kwanza moyo.....huwezi jua,labda anaumwa,amekufa,amepata matatizo,ameibiwa hizo hela,ameuguliwa,amefiwa etc......kwa nini tu uje na hypothesis moja tu......

Lakini kitu nachoshangaa na kukuona wewe ni MJINGA,utakuaje na rafiki ambaye hujui anapoishi,hujui wazazi wake,ndugu,jamaa na marafiki....narudia tena wewe ni MJINGA
Sawa... Ila ndo apatwe na hayo matatizo baada ya kupokea pesa?
 
Back
Top Bottom