Nimedhulumiwa MilionI 10, siku ya Tano sasa sijapata Usingizi

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,688
3,816
Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.

Huyu jamaa yangu ni kama ndugu kabisa, tulikuwa na urafiki unaovuka mipaka, the guy was so deep na alikuwa Loyal yaani ni rafiki yule wa haswa haswa, rafiki ambae tumeshibana na tunaelewana mno mno wazee.

Hapa kati wakati Project inaendelea kuna wakati tuligombana na wabongo ambao walikuwa ni mamluki kwenye kampuni ilo la wa asia, huyu mshikaji wangu ndio aliwazingua sana baadae nikaingilia kati tukali-solve ilo tatizo na tukawa peace tena.

Sasa kuna wakati nilisacrifice kazi zangu za nje kibao ili tuisimamishe hii project sababu at the end of the day tulikuwa tunapata faida ya milion 20+ na tuko mtu mbili tu, so nikiwa na vimeo vingine nje (nna kazi nyingine nje tofauti na hii) nawaachia watu wengine wanifanyie kwa niaba.

Long story short, project iliisha salama sasa tukawa tunaanda bills na documents zingine ili wa asia watulipe hela zetu, so mshikaji wangu amesomea haya mambo ya uhasibu so ikawa kazi yake kuandaa then mwisho wa siku tupeleke na tukiwa tume attach na account zetu za malipo, mie nikapata kazi (kama nilivyosema nina kazi nyingine nje ya project) ambayo ilikuwa inanilazimu niende Dodoma kuikamilisha siku hiyo.

Mazee huyu rafiki yangu ameshirikiana na wale wabongo wenzetu kwa wa asia wamempa hela yote huyu rafiki na sijui makubaliano yao au walipeana shingapi ila ndugu rafiki amekimbia na hela zote na hajulikani alipo, too sad hela alipewa cash (imagine) na mafacilitator ni hawa wabongo wenzetu wa kwa waasia. Jamaa hayupo popote ndani ya mji huu wa Dar.

Bado napambana kumpata na nimeshachukua hatua kubwa ya kumtafuta popote alipo ndani ya nchi hii, ila nimejiuliza maswali mengi sana na ambayo yamepelekea leo siku ya tano tunaenda sipati usingizi kabisaa na kila saa moyo wangu unauma na kuumwa kama vile kila siku naumizwa upya.

1. Ni kitu gani kimempata huyu ndugu yangu? Hustles zote zile tukiwa nae hakumbuki? Hakumbuki namna alivyokuwa irrelevant kwenye hii project na namna alivyochangia padogo sana kiasi hata asingekuwepo mradi ungesimama japo yeye ndio alilileta ili tenda? Why amesahau nafasi yake kwenye hili?

2. Ubongo wa mtu mdhulumati huwa unawaza nini kichwani? Yaani future yake huwa anaiona vipi? Anapata usingizi huko alipo? Is he happy? For how long?

3. Unawezaje kumsaliti rafiki yako ambae yuko loyal kwako? Hizo ni akili gani na roho ya namna gani hiyo?

4. Kwanini watu wengi wanakosa ubinadamu na haki pale hela zinapokuja? Je ukichukua haki ya mtu unadhani na yeye hato react back?

5. Nimfanye nini huyu mtu? Mbona nna haki zote hata nikiwafuata wataalam wa radi kwenye hili hawatosita kunisaidia tena bila masharti! Je mdhulumati huko aliko kama atakufa au akipata matatizo ambayo akiyaona sio kawaida atafanya nini?

Mwisho kabisa, nimeumizwa sanaa na maamuzi ya ndugu rafiki na nimekwama sanaa ktk kipindi hiki hasa nikikumbuka ile sacrifice na hustles za days and nights na ningeomba nitoe angalizo tafadhali, mtu kama hakuzaliwa na wewe usimwamini kwa namna ya aina yoyote ile sababu uliezaliwa nae atleast kuna sehemu unaweza kumkamata.
 
Mkuu kwakuwa hujajua bado kilichompata huyo rafiki wako naomba tuliza kwanza moyo..... huwezi jua, labda anaumwa, amekufa, amepata matatizo, ameibiwa hizo hela, ameuguliwa, amefiwa etc...... kwa nini tu uje na hypothesis moja tu......

Lakini kitu nachoshangaa na kukuona wewe ni MJINGA,utakuaje na rafiki ambaye hujui anapoishi, hujui wazazi wake, ndugu, jamaa na marafiki....narudia tena wewe ni MJINGA
 
Mkuu kwa kua hujajua bado kilichompata huyo rafiki wako naomba tuliza kwanza moyo.....huwezi jua,labda anaumwa,amekufa,amepata matatizo,ameibiwa hizo hela,ameuguliwa,amefiwa etc......kwa nini tu uje na hypothesis moja tu......
Laini kitu nachoshangaa na kukuona wewe ni MJINGA,utakuaje na rafiki ambaye hujui anapoishi,hujui wazazi wake,ndugu,jamaa na marafiki....narudia tena wewe ni MJINGA
Alikuwa ni kijana wa gheto tu maana alifukuzwa kazi akashuka sana kiuchumi na hii project ndio ilimpa walau nafasi ya pili, anapokaa nilifika na vitu alivyoviacha thamani yake haizidi au haifiki milioni moja.
 
Mkuu kwa kua hujajua bado kilichompata huyo rafiki wako naomba tuliza kwanza moyo.....huwezi jua,labda anaumwa,amekufa,amepata matatizo,ameibiwa hizo hela,ameuguliwa,amefiwa etc......kwa nini tu uje na hypothesis moja tu......
Laini kitu nachoshangaa na kukuona wewe ni MJINGA,utakuaje na rafiki ambaye hujui anapoishi,hujui wazazi wake,ndugu,jamaa na marafiki....narudia tena wewe ni MJINGA
Inabidi atujibu vizuri haya maswali..
 
Pole sana malipo hapa hapa duniani. Pesa mwanaharamu inaondoa ubinaadamu kwenye pesa usilete udugu, urafiki wala ujamaa, usiamini mtu na pesa isitoshe hio pesa haitomfikisha popote, karma is a bitch!

Kwanini hukuomba salio lako upewe binafsi au uwekewe kwenye account yako?
 
Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.
Pole sana.

Umemuamini sana, ulitakiwa ku verify na kuwa karibu kwenye ku finalize malipo.

Inawezekana ikawa bora umemjua mapema, usiwe naye kwenye deal kubwa zaidi.

Whether utapata au hutapata hela zako, hesabu hili kama funzo. Inaonekana wewe mtafutaji na utapata pesa nyingine tu, epuka kuamini watu sana tatizo hili lisijirudie.

Never underestimate people's greed or overestimate their virtues.
 
Mkuu angalia asije kuondoka na afya yako (ambayo ni muhimu zaidi kuliko hizo 10m)

Ndio hivyo binadamu sio wa kuamini 100%...., In short expect the worse....; Na mara nyingine hata kama ni ndugu usiwaweke katika vishawishi yaani usiwaamini sana wala kuwaaachi upenyo mkubwa wa kuweza kufanya yao hence kuvunja undugu / urafiki...

"Blessed is he who expects nothing, for he shall never be disappointed"...

NB: Tena una bahati mwingine angevuta pesa alafu akaita wadau wakampiga na kumuachia makovu alafu akakupigia kwamba ameibiwa na anaomba pesa za matibabu au kalazwa hence uende kumuangalia..... In short Dunia Sasa Imani Imekwisha...., Si kwa Watoto, Si Kwa Wazee, Kwenye watu 10 Binadamu ni Mmoja....
 
Pole sana malipo hapa hapa duniani.Pesa mwanaharamu inaondoa ubinaadamu kwenye pesa usilete udugu,urafiki wala ujamaa,usiamini mtu na pesa isitoshe hio pesa haitomfikisha popote,karma is a bitch!

Kwanini hukuomba salio lako upewe binafsi au uwekewe kwenye account yako?
Huyu na wale wabongo wengine waliniwahi walikula njama, ni kipindi ambacho tunaanda bills na mie kuchomoka kidogo tu ndio chance wakapata hapo na nilichomoka ndani ya masaa 24 tu.
 
Niliungana na rafiki angu tukaunda timu na tukafanya project na kampuni ya wa Asia, project tuliifanya kwa muda wa miezi tisa. Na hapa kati hakukua na malipo ya ziada au ya kazi zaidi tu ya malipo ya vitu vinavyohitajika wakati wa Project hasa accomodations na transports tu.

iwa na wewe usimwamini kwa namna ya aina yoyote ile sababu uliezaliwa nae atleast kuna sehemu unaweza kumkamata.
Tuwasiliane
 
Back
Top Bottom