Nimedanganywa mara tatu!

mama kubwa

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,411
8,394
Ndugu zangu naomba msaada katika maisha yangu nimedanganywa mara nyingi lakini mara tatu nimefanywa mjinga hadi najiona sifai

1.nilidanganywa na mwanaume akanizalisha akaniacha

2.nilipata mwanaume mwingine akanitapeli kumbe ana mke na watoto

3.nilikutana na mume aliyenizalisha akaahidi kunisaidia kutunza mtoto kibaya mazingira yalinifanya nishirikiane nae kanitosa tena
chonde naomba msaada wa mawazo lakini msinitukane mtazidi kuniumiza
 
Mwe....kwani mwenzetu akili zako kazishika nani jamani mpaka uwe wa kuumizwa tuuuu!
 
Pole sana,ila umewapa kweli kweli,punguza mwendo kasi.
 
Njoo kwangu, mimi sitakudanganya nitakuambia ukweli daima. Ukweli wangu ni kwamba nina wake 5 na watoto 30, wewe utakuwa bimdogo wa 6. Naomba uweke kumbukumbu sahihi usije ukasahau na kudai nilikudanganya sina mke.
 
wanaume ndivyo walivyo wasamehe wote hao waliokudanganya songa mbele mlee mwanao atakuja wa ukweli mpaka hao wataona aibu na wakati mwingine uwe makini
 
ooh pole sana mpendwa, kwa sasa achana kabisa na wanaume pambana na ajira ili uwalee wanao na pia ikiwezekana wapeleke baba wa watoto wako ustawi wa jamii ili upate msaada wa matunzo ya wanao. KUZAA SI KAZI, KAZI KULEA MWANA
 
okay girl u gat fake nailz,fake eyez,fake hair,fake ass.....n u expect to get a real man!!!!!!dream ova!!!!
tubadilike na sie, tusilalamikie sana wanaume
 
ndugu zangu naomba msaada katika maisha yangu nimedanganywa mara nyingi lakini mara tatu nimefanywa mjinga hadi najiona sifai

1.nilidanganywa na mwanaume akanizalisha akaniacha

2.nilipata mwanaume mwingine akanitapeli kumbe ana mke na watoto

3.nilikutana na mume aliyenizalisha akaahidi kunisaidia kutunza mtoto kibaya mazingira yalinifanya nishirikiane nae kanitosa tena
chonde naomba msaada wa mawazo lakini msinitukane mtazidi kuniumiza

Mama mkubwa karibu kwa Bujibuji mfariji wa ajabu.
 
jamani mama Kubwa kwa vile umeshajifunza kupitia haya yote next time fanya evaluation kwanza kabla ya kutoa maamuzi yoyote ..
Pole sana
 
Ndugu zangu naomba msaada katika maisha yangu nimedanganywa mara nyingi lakini mara tatu nimefanywa mjinga hadi najiona sifai

1.nilidanganywa na mwanaume akanizalisha akaniacha

2.nilipata mwanaume mwingine akanitapeli kumbe ana mke na watoto

3.nilikutana na mume aliyenizalisha akaahidi kunisaidia kutunza mtoto kibaya mazingira yalinifanya nishirikiane nae kanitosa tena
chonde naomba msaada wa mawazo lakini msinitukane mtazidi kuniumiza

haya ndo matatizo sasa mama kubwa..................

siku zote sumu haijaribiwi kwa kuonja>>>>>>>>>>>>>>
 
okay girl u gat fake nailz,fake eyez,fake hair,fake ass.....n u expect to get a real man!!!!!!dream ova!!!!
tubadilike na sie, tusilalamikie sana wanaume

hiyo ya fake ass ndo imeniacha hoi kabisa..........................
 
Wewe dada angu, una bahati kwani umeleta JF ndo penyewe. Kuna wengine hawajui pa kukimbilia wala wa kumueleza kwa hiyo tuliza moyo. "Acha mawazo ya kujisikia maisha bila mwanaume hayawezekaniki". Sasa ndo muda wako wewe kuonyesha kuwa umekomaa kifikra. Pigana kwa njia sahihi, ondoa hayo mawazo ya kujilaumu kwa mambo yaliyopita, songa mbele.

Jitahidi tu kuweka mipango yako vizuri, nenda kanisani kila jumapili au msikitini kila ijumaa au jumamosi sali na rudi nyumbani jipange kwa kazi zako.

Wanaume wapo wengi tena sana, atakuja atakayematch nawewe. Onyo, usifanye haraka kumpata kisa umemiss mambo fulani, vumilia jiweke sawa kila idara. Nakuhakikishia ndani ya mwaka mmoja utakuwa unawaza vitu vingine kabisa kama kufungua mradi wa ..... maeneo fulani.

Nakutakia kila kheri, najua hutapuuzia kuchukua mchele na kuacha pumba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom