Nimechukizwa na kitendo cha Rais Magufuli kujigamba hadharani kuwa anawatukana mawaziri wake!

Status
Not open for further replies.
Naamini hujawahi kukaa usukumani mimi sioni jambo la ajabu na amesema hayo katika nia njema kuwa hata yeye na mawaziri wake huwa inafikia hatua wanaambiana maneno makali ili kazi iende. Hakuwa na maana ya kuwatukana kama ulivyojikalilisha wewe
Pumbavu...mambo ya usukumani usihusishe na taasisi ya Urais...Udhaifu wa mtu mpuuzi ni upuuzi wake mwenyewe
 
Ukiangalia kwa makini na kutafakari sana utagundua kuwa Rais Magufuli amekuwa Rais wa pekee duniani kuongea maneno ambayo kimsingi anapozungumza basi miongoni mwake yanakuwepo maneno ya HOVYO kupita kiasi. Unaweza kujiuliza sana kama Rais Magufuli ana utimamu kiuongozi na jibu ukalipata vizuri sana kutokana na anavyozungumza.

Wapi katika dunia hii umewahi kusikia Rais mwingine mbali na Magufuli akijinasibu kuwatukana wengi wa mawaziri wake? Wapi umewahi kusikia? Ukishaona hilo utagundua kuwa tuna Rais wa kipekee kama ambavyo wana CCM wasemavyo kwa kumpamba.

Akiwa mkoani Kilimanjaro alimpa za uso RC Meck Sadick hali iliyomfanya aamue kujiondokea, akamfanya Kinana akimbilie kusiko julikana. Alitaka kuleta sintofahamu kwa mama Samia bahati nzuri wakaokoa jahazi. Sasa hao waliotoka "Majalalani" wanaona sawa tu kutukanwa. Huwa najiuliza sana! Lakini mwenye shida ni Rais mwenyewe. Ukiona tayari una madaraka makubwa kiasi cha kuweza kuamua chochote basi ni bora sana ukatawaliwa na busara.Usijikweze kwa kumtukana mtu mzima mwenye familia huku ukiona hana ujanja kutokana na maisha, mbaya zaidi ni pale unapomtangaza hadharani.

Kiukweli kitendo cha Rais kujigamba hadharani kuwa anawatukana mawaziri wake si cha kuchukuliwa kikawaida. Ameongea hivyo ili baadaye aanze kuwatukana sasa hadharani. Anapima upepo na kutokana na ilivyochukuliwa basi tutarajie watu kuanza kutukanwa hadharani. Yani tumekuwa waoga-wajinga mpaka tunakera. Inakuwaje? Ni ufukara wetu? Ni unyonge tulio nao ambao wanajivunia?
Mkuu, WAACHE WAFU WAWAZIKE WAFU WAO...!!!
YEYOTE ANAYEDHALILISHA ELIMU NA KUTOIPA THAMANI YAKE KWA AJILI YA MLO MMOJA NI "PUMBAVU TU" HASTAHILI JINA JINGINE ZAIDI YA HILO. WANAPATA HAKI YAO
 
Naye pia Ni binadamu Kama walivyo binadamu wengine,,ana madhaifu yake.
Hana mpangilio mzuri wa Nini akiseme na Nini asiseme...
Yote kwa yote ndio Rais wetu tuliyemchagua

Ukipitia upadri unakuwa shaped,Na kuifaa jamii.Utakuwa Na self confidence, public speaking, hekima Na busara,utulivu wa nafsi,uwezo wa kujenga Hoja Na ushawishi utu Na huruma juu ya wengine, kinywa chako hakitoyanena machafu,nk.
 
Hujawahi kufanya kazi chini ya mtu ambaye anakudhalau ,ndo maana huwezi kujua maumivu yake.
Hao wala usidhani wanajali hiyo kudharauliwa. Wenyewe wako peace tu, bora mkono uende kinywani.
Kuna methali inasema 'mtumikie kafiri upate mradi wako'
 
Yule bos wa TIC aliulizwa na Magu"hukunipigia simu nikakutukana wewe?"

Jamaa akabaki anacheka cheka tu,achana na utamu wa V8 na allowances lazima uwe mpole tu.
 
Kama ni wapumbavu kweli ulitaka atumie msamiati gani? Wenyewe wanakiri kuwa wameokotwa jalalani, sasa kuna kosa gani?
 
Kama nimekukuta ukiwa unaishi jalalani na wewe ni profesa tena wa sheria kwa nini nisikuite mpumbavu. Safi sana mtukufu, endelea kuwaita wapumbavu hao wapumbavu uliowaokota jalalani!
 
HAKUNA , WATANZANIA MNANYUMBURISHA MANENO SANA , YEYE HAKUSEMA ANAWAAMBIA WAPUMBAVU,HIVI NYIE MBONA MNAMLISHA MANENO RAIS,
pambafu zenu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom