Nimechoswa na kuombwa pesa kila siku na vijana

Kamundu

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2006
Messages
2,746
Points
2,000

Kamundu

JF-Expert Member
Joined Nov 22, 2006
2,746 2,000
Najua nasemea wengi 70% ya Watanzania ni chini ya miaka 25. Mpaka 35 itakuwa karibu 85%. Kumekuwa na utamaduni wa vijana kuombaomba pesa kila siku nimevumilia lakini inabidi niseme ukweli nimechoka.

Yaani tuna wazazi wa miaka 60-80 halafu tunatumia pesa badala ya kusaidia wazazi kila siku vijana wanatafuta mbinu za kutubomu. Wamekuwa wepesi kushinda kwenye mitandao zaidi kujua kila aina ya siasa na wasanii lakini hakuna kazi, kipato wala hata

Kibaya zaidi wengi hawana hata ubunifu wala maamko. Ugumu wa maisha haujaanza leo wakati nikiwa kijana zaidi miaka ya mwisho ya 90’s na 2000’s tulikuja na mwamka wa wakati ule kutafuta shule nyingi kwa shida bila mitandao lakini Watanzania walienda Dunia nzima miaka ile sio kwa kupenda lakini kulikuwa na uhaba wa vyuo.

Hatukuwa ombaomba tulitafuta mbinu. Siku hizi hata na mitandao ukiuliza ni wanavyuo wangapi wametafuta scholarship utapata wachache pamoja na kuwa na simu na kila kitu online. Yaani kwenye maendeleo hata kumsaidia kijana wa siku hizi wewe ndiye umuombe na kumuuliza kuhusu maendeleo yake mwenyewe na wanasiriki hata kukukwepa ukikazania sana kuongea mambo ya maendeleo. Sisi mbona hatukusubiri serikali miaka ile siku hizi ni kusingizia na kushabikia tu lakini hamna utekelezaji.

Vijana wanaoa wakati hawana kazi wala chochote halafu baada ya mwaka ni matatizo tu. Wengine wanasubiri wazee wao wafe ndiye wapate nyumba au hata kupigana kwa vitu vya wazazi. Hii generation ya vijana waliozaliwa kuanzia miaka ya 1985-2000 ni zero na kama wasiikobasilika wanashida maana wanashindana na Dunia nzima siku hizi. Nitaandika zaidi lakini nimeamua kama siku kitu cha kujiendeleza si saidii kijana

Yanni hata diaspora watakuambia ukienda TZ watu wakwanza kukucheka ni hawa vijana kwanini hujajenga, umepoteza muda wakati wenyewe wanakuomba pesa wewe! Nimekuwa frustrated sana na hawa vijana kuomba omba pesa kila siku. Binadamu tunaomba misaada lakini kwa wakati wa shida kama misiba au harusi sio kila wakati.
 

Forum statistics

Threads 1,344,244
Members 515,354
Posts 32,812,521
Top