Hahaha.Utasikia 'Hebu fanya mpango wa ten hapo'
Kwanini uombe ombe hovyo unampa kazi ya kukunyima mwombaji.Wanyime..
Kwanza naomba niseme uzi umenihuzunisha sana kwasababu mimi ni mmoja wa vijana katika umri huo...
Lakini ngoja nikuvunjie hapa ukweli wa hali halisi....
Kizazi chetu kimeathiriwa na vitu vifuatavyo:-
MFUMO WA ELIMU umetufanya tuwe tegemezi wa ajira sana kuliko ubunifu binafsi na ujasiriamali yaani nakumbuka hata tukiwa shule kiutaniutani mwalimu anakwambia EGM maana yake ni Expected General Manager tena wanakupa story za makampuni makubwa so unasoma ukiwa na fikra fulani tegemezi kwa ajira......
UKOSEFU WA AJIRA: baada ya mfumo wa elimu kukuandaa kutegemea ajira sasa unamaliza shule unakuja mtaani unakutana na kisanga kingine kabisaaa cha ukosefu wa hizo ajira na ubaya zaidi watanzania wengi hatuna transparency so kuambiana ukweli ni shida.. Utaanza kudanganywa na ndugu, marafiki na wengi watakwambia lete cheti huku! Lete CV huku! na ww unakaa kusubiri tu muda unazidi kwenda.. Bila ya kuwa na plan B ndio unaishia kupiga vizinga na kushinda mitandaoni hopelessly....
UGUMU WA MAISHA KATIKA AWAMU YA TANO YA UONGOZI:- hapa naomba tuwe wawazi jamani awamu hii ya uongozi imeleta changamoto sana ya maisha kuliko iliyopita ndio maana hata issue ya upungufu wa ajira haikusikika sana awamu iliyopita kutokana na unafuu wa maisha... Mfano sasa hivi unaona watanzania hawazungumzii tena siasa au kushiriki uchaguzi kwa wingi tofauti na awamu iliyopita kwasababu ni ngumu kuongea ukiwa na njaa tumboni yaani hii stlye ya kubana maisha ili watu wawe busy na vitu vingine imefanikiwa... Jamani familia nyingi zina maisha magumu sana kwa sasa na hii ni hatari sana kwa nchi na uongozi mzima inaweza ibua matatizo mbeleni huko.... (Mtoa uzi naamini awamu iliyopita hukuwahi pata vizinga sana)
UTANDAWAZI:- hapa naomba nicheze na social networks.. Kutokana na ugumu wa maisha na ukosefu wa ajira vijana wengi wakakimbilia kwenye mitandao ili kupunguza makali na kupoteza muda kidogo.... Wasichokijua mitandao ina addiction kama dawa za kulevya yaani ukisha ingia inakuchanganya akili haswaa (wahanga wananielewa, yaani ukiingia mtandaoni unajikuta unapoteza muda mrefu bila kutegemea hii ni kwa sababu ubongo unapigwa na butwaa kwa kukuta taarifa nyingi kuliko uwezo wa ku process) na wakuu wa dunia wanaitumia kufanya Mass control kwa kupenyeza ajenda za kipuuzi ambazo vijana tunazikuta na kuzibeba bila kujua purpose yake... (JAPO MITANDAO INA POSITIVE SIDE YAKE)
Natamani kuendelea lakini let me jump to solutions:-
AJIRA:- Kuna trick mimi huwa napenda kuwaelekeza watu "Katika mazingira magumu ya ajira kama una degree bhasi tafuta kazi za form6 au diploma au form4 kwanza then piga show hapo huku unaangalia channels zingine maana ni rahisi sana kupata kazi ukiwa kwenye kazi kuliko ukiwa nje ya kazi maana inaweza tokea ukapandishwa cheo hapo ulipo au kutokana na utendaji wako wa kazi ukapata shavu sehemu nyingine" TATIZO vijana hatupendi kujishusha.
UJASIRIAMALI:- Hapa unatakiwa kuwa mbunifu sana, tumia mitandao ya kijamii, usiwe muoga wala aibu kwenye kutafuta pesa.
Ikiwezekana hama mtaa au mji kabisa tafuta sehemu ambayo utakuwa comfortable kufanya mambo yako..
Ahsanteni..
VIJANA TUACHE UVIVU NA UJINGA NDIO CHANZO CHA VIZINGA.