Nimechoka!

DMussa

JF-Expert Member
Sep 24, 2007
1,310
296
Jamani wana JF wenzangu,
Kama kuna kitu ambacho nimechoka kukisikia katika maskio yangu ni “UFISADI!”. Kwa kipindi kirefu sana tumekuwa tukishuhudia mambo mengi yakiibuka juu ya mikataba mibovu, matumizi mabaya ya fedha za serikali uongozi mbovu n.k.

Kwa kweli mwanzoni nilpatwa na ari ya kutaka kuiona Tanzania mpya yenye watendaji waadilifu na wenye kuithamini nchi yao pamoja na rasilimali zake. Hii ari yangu nasikitika kukiri kwamba imeisha ghafla mara tu baada ya kuona na kuamini kwamba huu ufisadi unaoibuliwa kila siku hakuna anaefanya kazi kuhakikisha wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusika katika matendo haya wanachukuliwa hatua kali za kisheria!! Naamini hivi kwa sababu kwanza haya mambo yamekua yakiibuliwa in series ili kuwafanya wananchi wasahau habari walizopata mwanzoni na kuhamia kwenye jambo jipya! Mfano. Ilianza BOT ambapo JK alimsimamisha kazi aliyekuwa gavana wa BOT Dr. Balali hili lilipamba moto sana katika wakati huo na hata suala la EPA kushikiwa bango na wananchi wengi kwa ujumla ila kabla hata ufumbuzi haujapatikana ikaibuka ishu ya Richmond ambayo pia iliitikisa nchi, serikali pamoja na chama tawala sisiem na hatimaye wale walioonekana kujihusisha moja kwa moja na hili sakata walijiuzulu kwa kudai wanachukua collective responsibility ambao ni EL, NK na IM! Hawa nao mpaka sasa hakieleweki ni kitu gani kinasubiriwa ili kuwachukulia hatua za kisheria ila ghafla anaibuka Chenge na akaunti ya nje ya nchi…. Sasa hivi kila mmoja anatega sikio kujua AC ataishia wapi na mabilioni aliyojikusanyia ktk miaka 30 ya ufanyakazi wake ndani ya serikali.

Kwa ujumla nimechoka na hizi habari maana sioni faida yake kwangu kama mtanzania kama leo EL anajiuzulu na kesho namuona akitanua wakati hastahili kufanya hivyo kwa ukubwa wa kashfa inayomkumba!! Hivi polisi, mahakama na jela zipo kwa ajili ya walalahoi?? Je ni kwa nini Balali hayuko nchini na kwa sasa yuko wapi? Je Chenge ana mabilioni nje ni vipi anayaita “vijisenti” ina maana zile ni sehemu tu ya fedha zake huko nchi za nje??? Je anastahili kuaminiwa au mali zake zitaifishwa na kutumika kwa kuletea wananchi wa Buhemba maisha bora ili waondokane na kununua maji kwa sh500/= kwa ndoo moja???

Nimechoka mimi…. Sihitaji kusikia ufisadi mwingine!! Huu nilioushuhudia unatosha kabisa kunipa picha ya huo mweingine unaokuja!!!
 
Kama wewe umechoka kuzisikia habari hizi basi epuka hizo threads zenye habari hizo. Usiwanyime uhuru wanaJF wengine wapya na wazamani kufahamu jinsi mafisadi wanavyoifisadi Tanzania. Wewe fumba macho na masikio ukija kufungua nchi imerudi katika mwaka 1800. Kila la heri katika jitihada zako.
 
Nimechoka mimi…. Sihitaji kusikia ufisadi mwingine!! Huu nilioushuhudia unatosha kabisa kunipa picha ya huo mweingine unaokuja!!!


Hitimisho lako ni kama ''ufisadi'' ni kama vile kelele za kunguru nje ya nyumba yako ambazo unaweza ziondoa just kwa kumwangalia tuu akakimbia!!

Kazi ipo mkuu tena sio ya ''kitoto''.
 
Dmussa mpiganaji hakati tamaa inabidi tuonganishe nguvu zetu zote ili kupinga na kutokomeza ufisadi kama wewe umekataa tamaa sio wote tutakaa tamaa hakuna inayependa haya mambo yatokee ndio maana kila siku tunamkoma nyani giladi mchana kweupe na jambo forums ni sehemu ambayo we dare and talk openly.Swali la kujiuliza je ukiwa umechoka je are you going to join with them?since I know if you dont like to fight with them join with them.
 
Dmussa mpiganaji hakati tamaa inabidi tuonganishe nguvu zetu zote ili kupinga na kutokomeza ufisadi kama wewe umekataa tamaa sio wote tutakaa tamaa hakuna inayependa haya mambo yatokee ndio maana kila siku tunamkoma nyani giladi mchana kweupe na jambo forums ni sehemu ambayo we dare and talk openly.Swali la kujiuliza je ukiwa umechoka je are you going to join with them?since I know if you dont like to fight with them join with them.

Mkuu heshima mbele,
You got my point... langu kubwa ni kwamba i feel like nothing is being done in all scams that have been revealed to date!!! Or may be they aren't doing enough!!

Nitaendelea kumkoma nyani giladi kama kawa ila nahitaji kujua tulicho nacho mbele yetu kimefanyiwa kazi kiasi gani??

Thread yangu haina nia ya kumkatisha mtu tamaa ila lets look at the bigger picture why are we being played???
 
kama umechoka na vita hivi kaa kimya utuachie wanaume tupambane mpaka kieleweke,hatutalala mpaka siku moja hili dudu CCM litakapong`oka na watoto wake.Ukiona kila kitu kinakuja na kuwekwa wazi basi ujue ukombozi uko njiani.Ubaya wa watu hawa usingeonekana kirahisi bila mapambano haya.Chonde kila silaha halali itumike adui yetu ametuona.
 
Usije ukakuta in one way or the other anafaidi matunda ya ufisadi iyo vita lazima aichukie
 
Ohoooo, taratibu ndugu yangu,

...nakushauri unywe maji baridi ikiwezekana tia na barafu upowe moyo, ndio kwanza majogoo, makubwa yanakuja...

ukiendekeza 'matofali' ya hapa na maskendeli ya taifa letu ndugu yangu utakufa siku si zako, muhimu familia yako inapata milo yao mitatu kwa siku basi.

Si unamkumbuka Marhum-dada Amina Chifupa na majina ya wafanyabiashara ya 'mdanga'? Tushamsahau! ...mbaya zaidi 2010 kuna ushindi mwingine wa tsunami kwa hawa hawa leo hii tunaowaita mafisadi.

Ndivyo tulivyo!
 
Nimechoka mimi…. Sihitaji kusikia ufisadi mwingine!! Huu nilioushuhudia unatosha kabisa kunipa picha ya huo mweingine unaokuja!!![/SIZE][/COLOR][/FONT][/QUOTE]

Ndugu yangu kama umechoka kiasi hicho na hutaki kusikia tena basi omba wana JF tukuandalie mahala pa kulala pema peponi, kwani wimbo wa taifa hauimbwi siku moja. Wimbo wa mafisadi ni wimbo wa kudumu hadi azaliwe rais mwenye uwezo mabegani mwake, lakini siyo hawa ambao ahadi anatungia mezani halafu kesho anakuletea utekeleze kisichowezekana. BORA MAISHA KWA KILA MTANZANIA.
 
Back
Top Bottom