DMussa
JF-Expert Member
- Sep 24, 2007
- 1,310
- 296
Jamani wana JF wenzangu,
Kama kuna kitu ambacho nimechoka kukisikia katika maskio yangu ni UFISADI!. Kwa kipindi kirefu sana tumekuwa tukishuhudia mambo mengi yakiibuka juu ya mikataba mibovu, matumizi mabaya ya fedha za serikali uongozi mbovu n.k.
Kwa kweli mwanzoni nilpatwa na ari ya kutaka kuiona Tanzania mpya yenye watendaji waadilifu na wenye kuithamini nchi yao pamoja na rasilimali zake. Hii ari yangu nasikitika kukiri kwamba imeisha ghafla mara tu baada ya kuona na kuamini kwamba huu ufisadi unaoibuliwa kila siku hakuna anaefanya kazi kuhakikisha wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamehusika katika matendo haya wanachukuliwa hatua kali za kisheria!! Naamini hivi kwa sababu kwanza haya mambo yamekua yakiibuliwa in series ili kuwafanya wananchi wasahau habari walizopata mwanzoni na kuhamia kwenye jambo jipya! Mfano. Ilianza BOT ambapo JK alimsimamisha kazi aliyekuwa gavana wa BOT Dr. Balali hili lilipamba moto sana katika wakati huo na hata suala la EPA kushikiwa bango na wananchi wengi kwa ujumla ila kabla hata ufumbuzi haujapatikana ikaibuka ishu ya Richmond ambayo pia iliitikisa nchi, serikali pamoja na chama tawala sisiem na hatimaye wale walioonekana kujihusisha moja kwa moja na hili sakata walijiuzulu kwa kudai wanachukua collective responsibility ambao ni EL, NK na IM! Hawa nao mpaka sasa hakieleweki ni kitu gani kinasubiriwa ili kuwachukulia hatua za kisheria ila ghafla anaibuka Chenge na akaunti ya nje ya nchi . Sasa hivi kila mmoja anatega sikio kujua AC ataishia wapi na mabilioni aliyojikusanyia ktk miaka 30 ya ufanyakazi wake ndani ya serikali.
Kwa ujumla nimechoka na hizi habari maana sioni faida yake kwangu kama mtanzania kama leo EL anajiuzulu na kesho namuona akitanua wakati hastahili kufanya hivyo kwa ukubwa wa kashfa inayomkumba!! Hivi polisi, mahakama na jela zipo kwa ajili ya walalahoi?? Je ni kwa nini Balali hayuko nchini na kwa sasa yuko wapi? Je Chenge ana mabilioni nje ni vipi anayaita vijisenti ina maana zile ni sehemu tu ya fedha zake huko nchi za nje??? Je anastahili kuaminiwa au mali zake zitaifishwa na kutumika kwa kuletea wananchi wa Buhemba maisha bora ili waondokane na kununua maji kwa sh500/= kwa ndoo moja???
Nimechoka mimi . Sihitaji kusikia ufisadi mwingine!! Huu nilioushuhudia unatosha kabisa kunipa picha ya huo mweingine unaokuja!!!