Nimechoka, Nataka kuchukua maamuzi magumu

Habarini ndugu, maisha yana changamoto sana kuna wakati akili inachoka na kujiuliza ni lini hizi changamoto zitaisha.

Naandika hii sms huku moyo wangu ukivuja damu na Machozi yakinilenga.

Sioni pa kushika I feel disappointed, kwa anayeweza naomba anisaidie ili niweze kusonga mbele.
Acha utoto Dogo, ujui changamoto ndo mtaji siku hizi.....pambania gemu chalii
 
Habari ndugu zangu!!
Niliandika Uzi huu nikiwa na majonzi na huzuni lakini mda huu naandika nikiwa na chembe ya matumaini.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza wale wote walioweza kunitia moyo na kunifariji NAWASHKURU SANA SANA, pia nilikwazika kwa kuzihakiwa na baadhi ya watu kwa kuniambia nikifa nikamsalimie Nyerere na Mkapa nasema kwamba nimesamehe kwa moyo wangu wote.

Naomba kumuongeza ndugu yetu mmoja humu ( sitamtaja jina) ameonyesha upendo wa dhati kabsa kwangu, hakika aliguswa sana na Uzi wangu, kwa upendo wake wa pekee ameweza kunisaidia kiasi cha pesa ili niweze kusonga mbele, NAMSHUKRU SANA SANA MUNGU AMBARIKI SANA.

Naomba niseme kwamba humu JF kuna watu watakuja na shida ya uhitaji hasa ya kiamaisha, kama utajiridhisha kuwa huyu mtu ni mhitaji na unaweza kumsaidia msaidie ila kama huwezi kumsaidia epuka kutumia maneno ya dhihaka kwake.

Kama huwezi kuweka daraja basi usiweke ukuta. Binafsi nimebarikiwa sana na huyu mtu narudia kusema Mungu ambariki sana.
Ameniachia NAFASI na mimi Nije kusaidia watu wenye uhitaji, siamini kabsa kwamba mtu ambaye hanijui ameweza kunisaidia? Nimetoa Machozi yenye furaha.

Asante pia kwa mwanzilishi wa JF na uongozi wote wa JF
 
na Mungu akubariki.
 
Bob nusu na robo ya watu humu tuna stori zetu za kutia huruma.

Lakini leo wote tuko hapa.

Graduates kama wewe.

Not employed kama wewe.

Lost business.

Lost an acre of tomatoes.

Two kids.

Broke as fvck.

Na nipo hapa.

Lost everything. 16 million debt. For 3 years been like a leper. Unaenda kujieleza kwa waliokukopesha kwamba kwa nini umeshindindwa kulipa. Hakuna wa kukusaidia. Believe me utapita tu.
 
Mimi ni graduate napatikana kilimanjaro, Nilikuwa nafanya biashara ya kutoa samaki Mwanza - Kilimanjaro changamoto ni kwamba yule ambaye nilikuwa namtumia hela ameamua kutoweka na pesa, Napiga simu yake bila mafanikio hapatikani for 5weeks now

Pole sana. Najua unavyoumia. Mtafute ila usipompata samehe tu na uanze tena.

Muhimu: usihuzunike kwamba utapata wapi hela nyingine. Utapata hela nyingi kushinda hata hiyo aliyokutapeli.

Jikaze kisabuni. Haya maisha kikubw pumzi.

Pumzi yaani afya njema ndiyo mtaji mkuu na rasilimali muhimu.

Usiwaze sana mpaka ukauchosha mwili na akili yako.

Vumilia mkuu. Pole sana. Sikujui na pia hunijui ila zingatia niliyokuasa na ninakutakia kila la heri.
 
Unataka kusaidiwa nin elezea mkuu
Maisha ni changamoto usichoke inuka jipanguse songa mbele hata sisi pia tunakomaa tu
 
Wale wote waliotoa mchango wa faraja kwangu siwezi kuwataja wote ila wanashukru sana
Kilangi masanja:
muxar:
mama D:
Fall Army Worm
Mwl.RCT
Nafaka
rr3
GENTAMYCINE

Siwezi kuwataja wote ila hao wote wamechagia mawazo mazuri sana ya kunijenga. Mungu awabariki Sana, ila kama kuna mwingine kama ataguswa kuniongezea nitashukru pia.

Asanteni sana wanaJF
Pole kijana magumu ni ya binadamu na ukiwa hai kukumbana na hizo changamoto ni lazima, binafsi nilikua nimeenda mahala jana kujarib kukopa kiasi flani nikutumie nikawa nimegonga mwamba ila tuko pamoja , aluta kontinua.
 
Ok sawa mkuu, nashukru sana kwa nasaha zako!!
Kama utafanikiwa basi utanisaidia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom