Nimechoka baada ya kushudia ajali hii alasiri ya leo Jiji Arusha.

LiverpoolFC

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
11,348
3,216
Ni dk kidogo kijana wa umri kati ya 16-17 alipogongwa na gari aina ya toyota Rv4 T 553 AVE eneo la Technical College Arusha na kupoteza maisha hapo hapo ni machungu kweli kweli lakini hayana budi kwani yameshatokea.

Huyu marehemu alikuwa anatokea upande wa juu kama kuelekea huko kusini yaani kwa wanaojua hapa ninapopazungumzia ni kwamba anaelekea kuliko pub ya Narok sasa kukawa na gari tajwa hapo juu inakuja na inaendeshwa na mama mmoja na kijana wake kwa ujumla ni kama anafundishwa mama gari na ndipo gari likamzidi nguvu huyu mama kwani alikuwa kwenye mwendo wa spidi kama 50 hivi na ndiyo hawa vijana kuhamaki gari karibu inawafikia na ndipo mmoja akamshtua marehemu naye akashindwa la kufanya na ndipo gari likamkandamzia kwenye mti na mauti ikamfika pale pale!

Kwa kifupi ndivyo ajali ilivyokuwa!

Picha ninazo lakini kimeo ninayotumia inashindwa kubandika nayo!

Bwana ametoa na Bwana ametwaa!
 
R.I.P kijana!
hizo picha wala usiziweke,maana sina uhakika kama unayo consent ya mhusika kuzitumia ktk machapicho yako!!
 
Zamaulid; Kwa kweli haina haja kwani marehemu amepata mkandamizo na kuvuja damu mpaka masikioni!

Haina hata mana nikiweka hizi picha kwani wengi tutaumia kinafsi sana!

Alale kwa Amani yake Bwana wetu!


R.I.P kijana!
hizo picha wala usiziweke,maana sina uhakika kama unayo consent ya mhusika kuzitumia ktk machapicho yako!!
 
Last edited by a moderator:
Na hapo anaenda kulipishwa faini ya tshs 20,000 au jela miezi 6.
Pole kwa familia.
 
usiweke picha my dear!
r.i.p marehemu kijana!
so sad kwa kweli !
 
Duh!...nakumbuka miaka ya tisini mwishoni maeneo hayo hadi huku Mianzini, njia panda ya Ilboru hadi Sanawari lilikua ni eneo la ajali sana...
 
so saaad...nguvu kazi imeondoka.... may his soul rest in eternal peace
 
Duh!maisha ya mwanadamu ni kama maua.Asubuhi huchanua jioni hunyauka.
Mungu ailaze roho ya marehemu peponi.
 
Preta; yani we acha tu! Imenitouch sana kwani mtu anakuwa na pesa yake anajichukulia maamuzi ya kujifunzia gari mwenyewe na ingali shule zipo lakini hawataki. Na ndiyo yanatokea madudu ya uzembe kama haya ya leo.


nimeishuhudia hiyo ajali....ila sikujua kama imeua....RIP mpiganaji.....
 
Last edited by a moderator:
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom