Nimechanganyikiwa, mwanaume akinipa hela ananiomba tena hela

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
Mpaka kuandika natetemeka...

Nina mpenzi wangu tuna 5 au 6 month yeye ana kazi anapokea kama 1m hivi kwa mwezi. Mimi nina biashara napata kama laki 3 hivi kwa mwezi.

Nimepanga chumba, kula, kodi ya kibanda na nyumba ni juu ya hiyo laki 3 ambayo ndio faida katika biashara yangu.

Lengo la kuomba ushauri ni juu ya huyu mpenzi wangu.

Iko hivi, mwisho wa mwezi wa 10 alinipa laki 1 niongezee mtaji dukani na tangu kanipa hiyo hela hahusiki na matumizi yoyote yanayonihusu mimi.

Anaweza kuja kula na kulala kwangu, kodi halipi, bills zote mimi, salon, kuvaa yaani matumizi yote yeye hahusiki.

Hata vocha jamani tangu tumeanza uhusiano kaninunulia mara 1 tu.

Yote nimeyavumilia tu nikaona labda ile laki aliyonipa ndio matumizi. Leo ananiomba nimpe elfu 30 kati ya ile laki; jamani na anajua juzi nimelipa kodi laki na 80 na nilimuomba aniongezee akasema hana.

Leo wa kuniomba elfu 30 kweli?

Na mwezi uliopita kabla hajanipa laki aliniomba elfu 30 nimkopeshe lakini mshahara ulipotoka hakunirudishia badala yake akanipa laki leo tena anaomba hela.

Buyu mtu anakuja kulala kwangu hata mia haachi asubuhi. Akiamua ananiambia pika nakuja kula anakuja hata nyanya tu hamna.

Da! Nimeshindwa kumuelewa.
 
I
Tatizo nyie watoto wa kike ukipata bwana tu tena awe pedeshee ndo unahamishia vita yote kwake Yale mabom wanayofanyia Korea kaskazin majaribio unataka yote uyalipulie kwake!
Imebidi nicheke tu,,,
Mi sijampa mzigo kabisa tatizo nikwamba pamoja na majukum niliyonayo sio wa kuniomba hela jmn sawa inawezekana ka kwama lkn nimemwambia sina kachukia sasa nifanyeje?
 
Nilileta Mimi hapa leo kuna vitu vimetokea imebidi nianze moja kueleza ili mtu naelewa ndio maana kuna baadhi ya maneno yanafanana
Okay pole.. Mchane jamaa ukweli, mwambie aache kuwa kama marioo.

Mwambie ukweli ukija kulia lia huku utaishia kukejeliwa tu na watu wenye stress zao.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom