Nimechanganyikiwa mpaka nakitamani kifo nisaidieni nifanyeje mimi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimechanganyikiwa mpaka nakitamani kifo nisaidieni nifanyeje mimi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Latifaa, Jan 18, 2012.

 1. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Naombezi mawazo yenu wadau wote mtakaosoma hii thred.

  Nimekuwa na mpenzi wangu kwa muda mrefu kama miaka 2 hivi, nimekua nikijihishemu kwa muda mrefu sijawahi cheat hata siku moja kwa vile nilikuwa namuamini sana. siku zote alinionyesha karidhika na mimi mpaka kwa wazazi wangu nilimpeleka anajulikana kwetu tukiwa kwenye process za kutaka kuoana nimekuja kugundua alikua ananidanganya kwa muda wote huo kumbe ana mke kibaya zaidi nina ujauzito wake.

  Naombeni ushauri wenye hekima nifanyeje na hii mimba, sijawahi kufanya abortion naninaogopa san maana najua athari zake nawaza sijuhi ninywe sumu ya panya nijiondoe duniani?
  au nikae tuu nizae ila nisimshirikishe maana sitaki hata kumtia machoni nimemchukia chuki mbaya nasijamueleza nimegundua alikua ananidanganya maana naona ili niwe na amani ni mfute kwenye aliki yangu na sitaki kesi nayeye maana naona kayatia maisha yangu dosari kaniletea aibu ambayo sijawahi kuitegemea kwenye familia yangu.

  Kingine kuna wanaume ambao wananipenda kwa muda mrefu nilikuwa siwataki kwaajili yake hata mpaka sasahivi wanaendelea sasa nafikiria nichague mmoja nimweleze ukweli kuwa nina ujauzito wa mtu mwingine? na je kuna mwanaume anayeweza kumpenda mshichana katika hali hii?

  Naombeni mawazo yenu wadau wote
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  yes...mwambie huyo mwingine una mimba na umeshaachana na aliekupa mimba
  that is onee step
  polee saana
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Pole mwaya.

  Hauna haja ya kunywa sumu wala kutoa mimba kwasababu tu ni yake. Kaa chini jipange, futa mawasiliano nae uanze maisha yako upya. Na wala usimwambie u mjamzito asije akakuganda nao. . .
   
 4. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana The Boss itabidi nifanye hivyo ila ni rahisi mwanaume kukubali mwanamke mwenye mimba ya mtu mwingine?
   
 5. f

  fisi 2 JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,332
  Likes Received: 516
  Trophy Points: 280
  Kihere here hicho
   
 6. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole dadaangu wanaume wengi hatuko wakweli, jipange upya.
   
 7. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ahsante Lizz nafuta mawasiliano naye ila anajua nina mimba,
   
 8. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  hapa sijakuelewa Lizzy ,kivipi asimwambie mwenye mimba? Una maana unataka Latifa acheze kale kamchezo ka kutaifisha mtoto na kumpa u bin wa ujombani?sikubaliani na wewe katika hili,nashauri amwambie jamaa kuwa ana mimba yake lakini hataki mahusiano yao yaendelee ila watunze mimba pamoja in the best way possible.
  Latifa,usijiue,mambo madogo sana haya,mi mwenyewe nshawafanyia wanawake madhambi kama haya mara kibao,walizaa na leo tuko marafiki tunalea.We tulia everything will be okay,time is the ultimate healer.
   
 9. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kuna rafiki yangu alishakubali ujauzito wa mtu, maadam kuwe na mapenzi ya kweli, na la muhimu huyo muhuni usimwambie kama una ujauzito wake kama alivyokushauri da lizzy.
   
 10. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  STOP! Usiingie kwenye mahusiano mengine kwa sasa,tunza mimba,inshallah uzae salama,then baada ya hapo ndo ufikirie mambo ya mahusiano mapya,umeelewa?
   
 11. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Acha bro kuna wanaume ving'ang'anizi, mpaka atamuharibia kitumbua chake kwa mwanaume mpya, huyo jamaa mpotezeee! mtose kimya kimya hakuna kumwambia wala nini!
   
 12. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nadhani umenukuu maneno ya Rais Kikwete katika kujibu hoja ya kwa nini watoto wa shule wanabebeshwa mimba.
   
 13. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kaaazi kweli kweli.
   
 14. Loly

  Loly JF-Expert Member

  #14
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 485
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 45
  Futa mawasiliano na huyo shetani wala usitoe mimba zaa mtoto wako usimshirikishe kwa kitu chochote, wanaume wamaana wamejaa na hawakatai watoto usimuue mwanao kisa huyo pepo endelea na maisha kama kawaida wewe sio wa kwanza kufanyiwa hivyo.
   
 15. N

  Navoyne JF-Expert Member

  #15
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  Hebu tuliza akili!!

  Jaribu kuwasiliana nae kama huwezi kulea mimba na huyo mtoto, mweleze msimamo wako kuhusu mahusiano yenu.kumbuka anaweza kuwa alikuwa anakupenda kweli ingawa ana mke na watoto, wekeni utaratibu wa kulea hiyo mimba na mtoto.

  Pili, pumzika na endelea kulea hiyo mimba usifanye maamuzi ambayo utajuta maisha yako yote kila la kheri. Ingawa ni ngumu kuamini upo na mt miaka miwili na unategemea kuolewa nae na hujui kama ana mke, labda ulikuwa hutaki kuamini hadi uone.

  Pole sana hilo halikufanyi kutoa uhai wako, mahospitalini watu wanaangaika kuongeza siku za kuishi.
   
 16. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #16
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,836
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hakuna haja ya kunywa sumu ya panya! Duniani hapa jambo moja baya laweza tokea ili kufungua milango kwa mambo mema zaidi! Ni habari ya kusikitisha na ninakuonea huruma! Baada ya kujitoa kwa Bwana huyu kwa uaminifu mkubwa kakutenda kiasi hiki!! Nenda kwa huyo mwingine umweleze si kwa lengo la kutaka akuchukue, lengo lako liwe ni kumshirikisha mwombe ushauri ufanye nini na haya yaliyokukuta lengo lake ni kutaka aufahamu ukweli akiwa kama mtoa ushauri na si kama mtu anayetaka kubwagiwa zigo. Tafadhali sana usionyeshe hilo, Mpigie simu mara kwa mara na umshukuru kwa ushauri wake umelala vizuri! Trust me you will win his sympathy na in the end atakuchukua
   
 17. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #17
  Jan 18, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa hapo hata kama hamtaki huyo mtoto waka hajali anaweza akamtumia kukutumia wewe au hata kuendelea kukuharibia maisha hivyo ni ngumu kukata mawasiliano nae. Nwy. . .pole sana.
   
 18. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #18
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kila kitu kina mwanzo dada Latifaa.
  Hakuna mwenye uzoefu wa kufanya chochote bila kuanza kwanza.
  Hii yaweza kuwa ndo mara yako ya kwanza!
  Opportunity is an opportunity, take it.
  I dont want to sound harsh lakini ni ukweli.
   
 19. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #19
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  habari ndo hiyo,na sio utani its a fact,inshallah one day we will get to know each other,you will see my watoto's na ninawalea mwenyewe.
   
 20. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #20
  Jan 18, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Kama huogopi kufa huwezi kuogopa ku-abort!
   
Loading...