Nimechaguliwa kusoma vyuo viwili kimoja ni cha 14 na kingine ni cha 122 duniani kwa ubora vyote ni "fully funded scholarship"

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
5,975
7,731
Nipo njia panda ni mwezi sasa, sijui niende chuo gani. Usiku na mchana nachakata ubongo wangu kisha nalala.

Katika kufanya application za vyuo mbalimbali duniani nimebahatika kuchaguliwa vyuo viwili.

Chuo kimoja ni cha 14 kwa ubora duniani, ila nikiwa nasoma chuo hicho nitakua nikilipwa kama milioni 2 na nusu kwa mwezi kama fedha ya kujikimu.

Hiki kingine nicha 122 kwa ubora duniani ila nikiwa hapo nitakua nalipwa milioni tatu na nusu kwa mwezi pamoja na marupurupu mengine.

Nipo hapa jamani, kuomba ushauri nifuate njia ipi. Je niende hicho cha 14 kwa ubora duniani au niende hicho cha 122?
 
Achana na kukagua majina ya jamii forum au kutaka kumpeleleza mtu kwa sheria za jamii forum ni kosa. Sheria ya confidential ikivunjwa kuna adhabu zake. Nakusisitiza uwe unasoma tu mada zinazoandikwa chukua maarifa au toa michango.
Tutolee upuuzi huku...
 
Sweden ndio chaguo sahihi kwa upande wa gharama rafiki za maisha.... hakuna ubaguzi... watu wa Scandinavia wanamioyo myeupe sana
 
Achana na kukagua majina ya jamii forum au kutaka kumpeleleza mtu kwa sheria za jamii forum ni kosa. Sheria ya confidential ikivunjwa kuna adhabu zake. Nakusisitiza uwe unasoma tu mada zinazoandikwa chukua maarifa au toa michango.
Kumbe wewe ni kijana mpuuzi kwa comment hiyo
 
Hizo funds zinakuwaga almost the same kulingana na gharama za maisha za nchi husika. Chuo cha 12 kinaonekana ni very reputable, kama course ni unayoipenda basi nenda hicho
 
Hizo funds zinakuwaga almost the same kulingana na gharama za maisha za nchi husika. Chuo cha 12 kinaonekana ni very reputable, kama course ni unayoipenda basi nenda hicho
Waswahili nimewashindwa kwa kubadilisha taarifa, mleta mada kwenye kichwa cha mada kaandika chuo ni cha 14 lakini ndani ya habari yenyewe kaandika ni cha 15.
Mkuu na wewe umekuja na chuo cha 12
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom