Nimechaguliwa kusoma Clinical Medicine, nijiandae vipi wakuu?

lelulelu

JF-Expert Member
Dec 8, 2017
401
366
Wakuu habari za muda,mm ni kijana ambae nilikuwa na ndoto za kuwa daktari tokea muda,maisha nikayaharakia baada ya kumaliza shule nikaoa ndoto zikapotea.

Nikajicjanganya na kazi za ufundi katika sehemu mbalimbali hasa mahotelini kwa muda usiopungua mwaka.

Mwanaka jana nikasema naenda kutimiza ndoto yangu nika apply nikapata chuo private, nimecjaguliwa kusoma Clinical Medicine ambayo nimefuatilia nimeambiwa nikikomaa na GPA ya 3.5 naweza kusoma MD moja kwa moja.

Sasa je, wakuu nijiandae vipi ili nifaulu?

Maana natishwa naambiwa ni kozi nguvu hasa kwa mm niloishia form four bora ingekuwa japo form six,ikoje hii wakubwa?

Nijiandae vipi ili kozi isiwe mogumu kwangu mwadau wangu?
 
Jiandae kifikra, kifedha na kimwili; na uwe na utayari wa kujifunza na kuelewa yale yote yanayofundishwa darasani na wakufunzi wako.
Amani ya moyo uwe nayo ya kutosha wakati wote na mambo yataenda sawa na miaka mitatu au semester 6 kwako itakuwa kama wiki 4 unaukwaa u-clinical officer ambapo kujiajiri/kuajiriwa kuko nje nje.
 
All the best usiogope hakuna kinacho shindikana chini ya jua ajira nje nje usikatishwe tamaa na walimwengu.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Jiandae kifikra, kifedha na kimwili; na uwe na utayari wa kujifunza na kuelewa yale yote yanayofundishwa darasani na wakufunzi wako.
Amani ya moyo uwe nayo ya kutosha wakati wote na mambo yataenda sawa na miaka mitatu au semester 6 kwako itakuwa kama wiki 4 unaukwaa u-clinical officer ambapo kujiajiri/kuajiriwa kuko nje nje
Sanste sana kaka.

Vp kuna haja ya kujiandaa kusoma labda baadhi ya mambo kwa muda huu ili iwe rahisi kuelewa mambo huko darasani?
 
Wakuu habari za muda,mm ni kijana ambae nilikuwa na ndoto za kuwa daktari tokea muda,maisha nikayaharakia baada ya kumaliza shule nikaoa ndoto zikapotea.

Nikajicjanganya na kazi za ufundi katika sehemu mbalimbali hasa mahotelini kwa muda usiopungua mwaka.

Mwanaka jana nikasema naenda kutimiza ndoto yangu nikahonga honga nikapata chuo private,nimecjaguliwa kusoma clinical medicine ambayo nimefuatilia nimeambiwa nikikomaa na GPA ya 3.5 naweza kusoma MD moja kwa moja.

Sasa je wakuu nijiandae vipi ili nifaulu ?
Maana natishwa naambiwa ni kozi nguvu hasa kwa mm niloishia form four bora ingekuwa japo form six,ikoje hii wakubwa ?

Nijiandae vipi ili kozi isiwe mogumu kwangu mwadau wangu ?
Nani anakutisha?Mkuu hakuna kisichowezekana katika maisha.Wewe Tayari ni MD unachohitaji ni kukamilisha utaratibu.SOMA kwa Bidii
 
Kwanza hongera.
kozi zote ngumu kama hautasoma kiufupi jitahidi tu usome kwa bidii na kwa kuelewa.
Semister huwa fupi na mambo mengi tunza mda wako
aliyepita form 6 na wewe wote mko sawa maana mnaaza wote certificates na hakuna tofauti yoyote kati yenu zaidi kitachowatofautisha umri,jinsia,uelewa,rang nk ila elimu ni ile ile.
mwisho kwa kua ada ya private ni kubwa nakushauri soma kwa mwaka mmoja kisha anagalia pumzi yako kama ngumu hamia gvt.

Kila la kheri
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom