Nimechaguliwa kusoma Automobile engineering ila sikuiweka kwenye machaguo yangu

Mkuu Twende skull Me nilisoma diploma kweny kitivo cha umeme lkn Nimechaguliwa Automobile Engineering, Sina Shaka nayo twende skull mkuu
Poa bro tutaonana huko now ntaenda kusoma willingly kabisa
 
Waajiri wa automobile engineers kwa hapa bongo ni wapi? Au wapi unaweza fanya kazi as an automobile engineer kwa hapa bongo
kuna brother angu yupo show room ya Mercedes-Benz analipwa dollar 2000/month.. soma iyo kitu wenzio tunaililia we aya tu
 
Nashukur wanajf kwa msaada wenu,nilikua stressed sana asee!!
 
Bwana mdogo tulia ukapige shule, Automobile Engineering ni kozi pana yenye wigo mkubwa iwe kuajiriwa au kujiajiri, Automobile Engineering kwa ufahamu wangu mdogo unaenda kusoma uhandisi wa vyombo vya moto, kuwa mhandisi ni zaidi ya kuwa fundi, Unaowaona kwenye magereji wengi tunawaita technicians, hao wana deal moja kwa moja kwa kutumia mikono yao katika kutatua matatizo katika vyombo vya moto, Katika nchi zilizoendelea mhandisi wa vyombo vya moto anafanya kazi ya kusanifu(design) muundo wote wa vyombo vya moto kuanzia engine system, gear box na makorokocho kibao, yeye anatumia kichwa kufanya analysis na kuelekeza ma technician namna ya ku solve tatizo katika vyombo vya moto. Neno engineering msingi wake ni Engine huko ndo kwenye uhandisi sasa. Na asikutishe mtu, wewe una maisha marefu kama Mungu atakupa afya njema, utajitunza na kujilinda nina maana gani? unapochagua career usiangalie hali ya leo mtaani au baada ya miaka 4 utakapohitimu, pima je baada ya miaka 10, 20 au 30 itakuwaje kwasababu kote huko wewe utakuwepo na utakuwa ni Nguvu kazi so nguvu kazi yako utailekeza wapi endapo utakuwa na miaka 30, 40 na 50. Je unachokisoma hivi sasa kitakuwa na mahitaji gani kwa jamii yetu.

Mimi ningekuwa wewe nisingekuwa na wasiwasi zaidi ya kujipanga namna ya kufaulu masomo yangu, Tunaposema huo uhandisi wa vyombo vya moto kitakwimu tunaamanisha kwa sasa Tanzania tunaagiza magari zaidi ya 50,000 kwa mwaka hii ni bidhaa ambayo hawa wote wewe na wenzio mtapigana kupata soko ili mfanye marekebisho endapo wamiliki watapata matatizo, Tunaongea tanzani ambayo sekta ya ujenzi inakuwa kwa zaidi ya asilimia 20 kwa mwaka na hawa ni watumiaji wazuri wa heavy machine ambazo repair and maintenance kama ya Grader,Crane etc haiwezi kufanywa na fundi wa gereji bubu huku, Mdogo wangu huku mjini kun wawekezaji wa kichina wana gereji za kisasa na mitambo ya kisasa ambayo fundi gereji wa mtaani hawezi kuitumia, Na kwa ukuaji huu wa teknolojia tuna miaka michache sana gereji bubu ambazo fundi hawezi kutumia software na mifumo ya kisasa kubaini tatizo la chombo cha moto zitapotea na kufa mbali kumbuka Technology ina save time,money and deliver high quality service sasa subiri uje uone hicho kiama cha ambao hata veta hawajaenda.

Mdogo wangu if you are to look in 10 years to come inawezekana kabisa tanzania ikawa na kiwanda cha ku assemble magari na vyombo vya moto, Kipo kimoja cha jeshi ila kina sua sua ila kwa hali ilivyo kidunia Africa na Asia ndio sehemu nzuri ambazo zitafaa kwa uwekezaji wa viwanda, wazungu washaharibu hali ya hewa huko kwao na misheria kibao wamejiwekea ili kukabili suala la uchafuzi wa hali ya hewa kwa hiyo kuja Africa au Asia is inevitable ni suala la muda, Usione china kakua kwa kasi sio yeye ni mimarekani baadhi imeanzisha mikampuni yao huko, sehemu nyengine nzuri itakuwa huko kwa hiyo kama Mungu atakurehemu uhai hadi miaka 20 ijayo tanzania utakayoiona si hii ya leo, Tanzania ya miaka 15 iliyopita si hii ya leo. Hiyo ni fursa tu kama utaamua kuajiriwa au kujiajiri. Sijazungumzia kabisa fursa iliyopo katika sekta ya usafirishaji ambako huko mdogo wangu hiyo fani yako hulali njaa.

Am on my mid 20's ila natamani ningekuwa na on my 10's ningeweka juhudi kuji brand internationally, Mdogo wangu nina maana gani, kwa kuwa ndo unaenda kusoma basi kaza kweli kweli, jua vitu jifunze kadri uwezavyo kila uchao jifunze vitu vipya jua dunia iko wapi kwenye career yako jua dunia inahitaji nini kwa sasa kwenye career yako, Tumia muda wako vizuri once you become smart you can go and work anywhere, Wapo huko watanzania wenzetu weusi ka ngozi ya t*ako ila wazungu wanaweheshimu kutokana na mzigo wanaoupiga yes hata wewe unaweza kama utawahi kuchukua hatua mapema na muda bado unao, ukiwa smart kwenye hiyo kozi sitashangaa kusikia unapiga mzigo Volkswagon, Mercidez Benz, Toyota, Volvo na kampuni yeyote ile duniani unayoijua ina deal na vyombo vya moto ili mradi tu uwe smart na uweze ku deliver kile ambacho wengi hawawezi. Usi limit ubongo wako kufiria tu hapa hapa tu, fungua ubongo maisha popote muhimu unapata maslahi unayoyahitaji. Nenda kasome acha kusikia majungu ya watu mdogo wangu acha kabisa watanzania asilimia kubwa ni watu wenye wivu, husda, wasiofanya tafiti, wenye kufuata mkumbo na wasiofikiria mbali go and chase your dream buddy. samahani kwa kukuchosha kuandika hobby yangu.
Umemaliza Mkuu asipokuelewa leo hatokuelewa tena
 
Sasa si bora ningeenda veta tu nilipomaliz form4,yani mtu una degree mkuu then uende kufanya kazi pamoja na artisans wa veta.Sasa si itakua nimepoteza muda bure au si bora tu niingie veta sa hv kuliko kwenda kupoteza miaka 4 kizembe
Mfano umefanya MD au BAF ile uwe Dr au mhasibu nani anafanya hizo kazi?,jibu unafanya mwenyewe katika level yako,kuwa na degree ya Automobile sio lazima ushike supana,unakua una vijana chini yako unawaelekeza/simamia kwa kuwa wewe unauelewa mpana juu ya hayo mambo
 
Sasa si bora ningeenda veta tu nilipomaliz form4,yani mtu una degree mkuu then uende kufanya kazi pamoja na artisans wa veta.Sasa si itakua nimepoteza muda bure au si bora tu niingie veta sa hv kuliko kwenda kupoteza miaka 4 kizembe
Una kasumba. Tatizo umri
 
Habr zenu wanajamv,nimechaguliwa hiyo kozi pale NIT lakini sikuiweka katika machaguo yangu niliyoweka TCU.Yani nahisi kuchanganyikiwa maana huku mtaan naambiwa kwamba naenda kua fundi garage,nataka nihame chuo lakini naogopa kuja kukosa mkopo maana now mkopo nishapata first batch.Nahitaji ushaur wenu wakuu nifanye nini hapo maana naona nishapoteza muelekeo wa maisha yngu
Vipi mkuu ushahitimu hapo NIT,na tupe mrejesho baada ya kumaliza chuo ..michongo vipi?
 
Vipi mkuu ushahitimu hapo NIT,na tupe mrejesho baada ya kumaliza chuo ..michongo vipi?

Mm n muhitimu ie Automobile Engineer. N course Nzur sana, Kwenye suala la michongo commitment zako tuh ila am really enjoying my professional. Huwez kufikiria kuajiriwa
 
Back
Top Bottom