Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.

Nilihamishwa kikazi kutoka Dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikuwa mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na Dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.

Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikuwa anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.

Nilikuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kuwa wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokuwa zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mimi mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.

Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia simu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.

Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kuwa yawezekana nimeshakanyaga waya.

Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)

Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba.

Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama ni kujifungua basi itakuwa mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa

Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana (mtoto wa kiume, ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)

Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mimi nasema kama mimi ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mimi nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitumika ndio kwa mbaali wakapunguza.

Jina hili limeendelea kuitwa na kutajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo, mimi nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo.

Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kufanana na wakubwa zake Wala mimi Wala yeye mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha.

Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kugombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawa imetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lakini moyoni naumia Sana.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi, huwa nakuwa na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokuwa yangu.

Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mimi hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba.

Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kuwa mimi uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili, nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mimi aniache nilee watoto wangu wawili

Naombeni USHAURI WENU wadau mwenzenu, niko dilemma.

NB: Matusi nisingependelea kuyaona
Na inshu ni kuanzia Sasa mtakuwa wanaume wawil mke mmoja hpo ndo Kazi Sasa, huyo alishaamua kuzaa Kabsa inaonekana hta Jina la mtoto ni la Hyo mme. Hpo ni kaz. Kwanin umewaambia ndugu zake yee hujamuambia Kuwa asepe?? Fanya maamuz magumu Kwa afya yako
 
Dodoma leo: huyu kwangu keshatoka na atasepa tuu, nisikufiche iwe nilichepuka akajua au hakujua kuniletea DAMU YA UKOO MWINGINE KWANGU NA KUTAKA MM NILEE ALAFU BAADAE UNIGEUKE UIPELEKE ULIKOITOA BORA HIZO PESA NIWAPELEKE WATOTO WANGU MAPUMZIKONI HUKO mikumi national park au tarangire
Nimelea mimba nimehudumia mtoto kuzaliwa na hadi Sasa anamiezi zaidi sita basi itoshe kusema basi matibabu maana cku hizi wanazaliwa na magonjwa
 
Inshu ya yeye Kuondka na watoto anaitumia Kama fimbo but najua hta akiondka nao ukifuata taratibu Hyo mkubwa Unaweza umchukua. Na hta mdogo pia. Na Kama akienda Kwa hyo mwanaume nakuhakikishia hayupo mwanaume anapenda kulea dam si yake utawapta tu ukae nao.
 
Bro kwa Sasa acha tu waende wakikua watakuja kama kuna mjomba wao anakili timamu basi atawarudisha maana Dada yake kazaa Kijiji alafu hakuna future nilikua nabebeshwa mizingo mingine mara unakomaliwa mtafutie kazi huyu wa darasa la saba acha waende aiseee
 
Yeye anaweza akaenda nje na akaoa kabisa,je huyo unayamtetea anaruhusiwa kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja?
Kwahiyo Swali lako hili ndiyo justification ya Wanaume Kuwasaliti Wake / Wachumba / Wapenzi wao?

Huna / Hamna Akili.
 
Hapana mkuu nimemuwezesha kwa jinsi alivyoomba na Sasa Yuko huko kwa wachungaji wake sijui baba wa kiroho wake anajishauri aanzie wapi maana kwenda kwao ni mtihani maana anaujua mziki wa kwao kwa maana ya life la pale, kwa mzinzi mwenzake ndo cjui anawaza nn
Ila nimepiga makufuri mapya yote kuanzia kwenye Geti la kuingilia,mlango wa kuingilia hadi milango ya vyumba vyote sihitaji kusikia jambo lolote aiseeee
Big up
 
Wewe ni Mwanaume au una jinsia ya kiume?

Nimekuuliza tu mkuu dah!!!

Kumbuka Kuna kitu kinaitwa Utamaduni, unapochangia usisahau na hili.
Mpaka utamaduni uje kuna sababu zilikuepo si ndio? Mf: utamaduni wa wanaume kuwa na manzi wengi ni kwa sababu ya maumbile, kutotosheka na mmoja ndo maana yakatokea haya ya watu kuoa wake wengi..na siku hizi updated version ni michepuko.

So hata haya ya wanawake kuzaa nje na kusingizia waume ndo tamaduni mpya imeanzishwa. Yani this is the beginning.
Jokajeusi aliemphasize purity mkamuona limbukeni lakini aliona haya kuja kutokea. Sasa kama mnaoa kwa vigezo vya pisi kali, sijui anajua kutuma salamu mtaacha kusingiziwa watoto. Tena huyo dada mshamba hajajua kulipanga game dadeekkk wengne game linachezwa na mwanaume hujui kitu mzee..

Na mnavyopenda wanawake sijui fighter, mara msomi, mara pisi kali...kumbe wenzenu wana teknolojia ya makombe na visomo, mnaingiza ndani mnafikiri mmepata watoto wanne kumbe watatu sio wako.

Kama wewe mwanaume hutataka kumtafuta Mungu akupe mke mwema hesabu chenga. Yani iko ivi. Kwenye kupata mke okoka kwanza. Mafunuo upewe na mbingu ndo utaelewa. Lakini kama hutaki ok. Sisemi kuwa ambao hawajaokoka hawana wake wazuri ila ili ukwepe hii tamaduni mbaya inayotaka kuanza....be on the safe side.

#itsyourchoiceanyways#
 
Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.

Nilihamishwa kikazi kutoka Dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikuwa mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na Dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.

Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikuwa anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.

Nilikuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kuwa wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokuwa zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mimi mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.

Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia simu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.

Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kuwa yawezekana nimeshakanyaga waya.

Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)

Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba.

Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama ni kujifungua basi itakuwa mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa

Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana (mtoto wa kiume, ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)

Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mimi nasema kama mimi ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mimi nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitumika ndio kwa mbaali wakapunguza.

Jina hili limeendelea kuitwa na kutajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo, mimi nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo.

Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kufanana na wakubwa zake Wala mimi Wala yeye mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha.

Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kugombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawa imetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lakini moyoni naumia Sana.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi, huwa nakuwa na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokuwa yangu.

Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mimi hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba.

Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kuwa mimi uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili, nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mimi aniache nilee watoto wangu wawili

Naombeni USHAURI WENU wadau mwenzenu, niko dilemma.

NB: Matusi nisingependelea kuyaona
Nakushauri ufanye maamuzi ya msingi Ili uwe na amani kama alikuwa anakuja kwako unampa mgegedo au wewe unasafari kwenda iweje afanye hivyo na kama alibaini kapata Mimba alishindwa kutumia njia ya kuitoa?
 
Tuje kwa mleta mada. Binafsi naona kiukweli una majeraha sahivi. Ila trust in time. Kwa ushauri wangu huyo dada arudi kwao tena na watoto wake wote kama anawang'ang'ania. Na wewe huku baki mwenyewe tafuta kitu cha kukupa furaha ila isiwe mwanamke( maana hapa utachuma matatizo mengine mara umtie mimba akati hukupanga).

Kaa kwa miezi unayoona inafaa tuliza akili, kula vizuri actually live healthy. Then utapata ukweli what you really want. Incase ikitokea unataka kumsamehe ili mkae sawa huyo dada asije na mtoto hapo kwako (atajua kama atamuacha kwa mzazi wake au atampeleka kwa baba ake).

Nashauri ivi ili isiendelee kukuumiza wewe na kukutesa. For the safety of your family. Ila ukikaa ndani ya mwaka ukaona hutaweza kumsamehe basi ni wewe. Though i believe ana a good side huyo mwanamke.

Though kitendo cha mama ake kujibu mbovu..huyo mama hana busara hata hivyo. Huna mkwe hapo. Na huyo dada nae haonyeshi kujuta that is very wrong yan hapo pana kichef². Atleast wanaume huwa wanajuta na kuomba misamaha kwa wake zao. Kiukweli maamuzi unayo wewe ila kwa sasa dada aende tu.
 
Daaaaaah kuna wanaume wenzetu wanapitia matatizo na tabu nyingi mnooo sana sana hizi tabu ni zakujitakiaa tuu
 
Tuje kwa mleta mada. Binafsi naona kiukweli una majeraha sahivi. Ila trust in time. Kwa ushauri wangu huyo dada arudi kwao tena na watoto wake wote kama anawang'ang'ania. Na wewe huku baki mwenyewe tafuta kitu cha kukupa furaha ila isiwe mwanamke( maana hapa utachuma matatizo mengine mara umtie mimba akati hukupanga).

Kaa kwa miezi unayoona inafaa tuliza akili, kula vizuri actually live healthy. Then utapata ukweli what you really want. Incase ikitokea unataka kumsamehe ili mkae sawa huyo dada asije na mtoto hapo kwako (atajua kama atamuacha kwa mzazi wake au atampeleka kwa baba ake).

Nashauri ivi ili isiendelee kukuumiza wewe na kukutesa. For the safety of your family. Ila ukikaa ndani ya mwaka ukaona hutaweza kumsamehe basi ni wewe. Though i believe ana a good side huyo mwanamke.

Though kitendo cha mama ake kujibu mbovu..huyo mama hana busara hata hivyo. Huna mkwe hapo. Na huyo dada nae haonyeshi kujuta that is very wrong yan hapo pana kichef². Atleast wanaume huwa wanajuta na kuomba misamaha kwa wake zao. Kiukweli maamuzi unayo wewe ila kwa sasa dada aende tu.
Suala la kusamehe HALIPO HILO ......keshavunja agano na zaidi kazaaa ....HAIPO ASEEE ABAKI HUKOHUKO..... akitaka na watoto sawa tu.....
 
Pole sana najua kakukosea. Na umefanya vizuri kumpeleka kwao. With time utaheal na utamrudisha nyumbani.
Kuna baba mmoja alifungwa jela miaka mitano. Alivyotoka jela alimkuta mkewe kazalishwa mtoto mmoja. Nae alichukia sana (Which is normal)Ila baadae vikao vya familia na mke kuomba msamaha. Alimsamehe mkewe wakarudiana na wakazaa watoto watoto watatu. Kumbuka kabla ya kufungwa walikuwa wamezaa mmoja ,ndo mkewe akazaa nje mmoja tena.Sasa wanaishi na watoto wao 5 including yule wa mke .Samehe na inawezekana kabisa.
Acha kumuingiza chaka mwenzio. Maamuzi aliyofanya ni sahihi.
 
Sijawahi na Wala ckuwahi kufikiria kutokana na migogoro ambayo nimekua nikishuhudia
Na hata yy mwenyewe alikua akinambia ni bora uchepuke lkn sio kuzaa nje ya ndo huyo mtoto cku ukimleta kwangu namwagia maji ya moto bora nikafungwe lkn sio wewe kuleta mtoto hapa kwangu, sitakubali kile tulichotafuta wote mwingine aje akifaidi

Daaaah hii kauli nikiimbuka namwagizia bia kila mtu niliekaa nae kwenye hii meza inauma Sana tena Sana
Ni mtihani hapa. Ila follow your heart. Take time kwanza. Hivyo akiwa kwao wewe endelea kuchapa kazi. Ila msamehe ili uheal. Msamehe kwa ajili yako. By the way kumsamehe sio lazima mrudiane. Ukitulia wewe ndo utaona sasa kama utamrudia ama la.
But samehe ili urelease pain otherwise utakuwa na uchungu hata kama ukioa mwanamke mwingine. Ule uchungu utakuwepo mpaka unaingia kaburini.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom