Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

Baada ya kusoma comments za huu uzi nimegundua kuwa wanaume ni maselfish kupindukia. Naomba niwe noted siko hapa kumtetea huyu mwanamke infact mko busy mnamshauri huyu jamaa mwenzenu kafinyiwa kwa ndani hana mpango wa kumfukuza huyu mwanamke angekuwa ana mpango asingekuja kuuliza humu ni vitendo tu dhidi ya maneno.

Ok mimi naangalia wanaume mlivyong'aka humu aisee. Yani kati yenu mliocomment humu mkute nusu mna watoto wa nje ya ndoa (kwa wale married men) na mmewaleta nyumbani wake zenu wawalee. Na wengine michepuko mmeijengea nyumba, na kuinunulia magari in the name of utamu. Halafu wake zenu wanaganga njaa tu na watoto wenu wanaishi under-standard life ukilinganisha na kipato chako. Pesa zenu msowekeza kwenye familia zenu mko busy kuhonga kisa puthee inafinyia kwa ndani.

Mmeumia, wengine mna hasira kweli. Sasa ndo muone jinsi wanawake huwa wanajisikia. Wanaume mliofadhaika na hili suala mjirekebishe na nyinyi msiumize wake zenu. Muwaheshimu na kuwapenda. Msijikute nyie ndo mna nyege mshindo, wanawake wawe watakatifu kisa we ndo mwanaume. Mbadilike au la...mambo kama haya ndo kwanza yanaanza hayataisha. Mtapata mnayostahili.

#stakibakahehekwenyecommentyangu#
Yaani sana. Hapa umesema kweli. Wao wamezaa nje .Ila mwanamke kuzaa nje ni kama kaua vile.
 
Kaka mtu kasema hata yy ni mwanaume hawezi kukubaliana na mke wake kuzaa nje ya ndoa ni bora angefanya mapenzi tu kama kweli alikua amezidiwa ikaisha lkn sio kuzaa nje hiyo ni dharau akanambia nimpeleke kwao

Mama mkwe yy anamtetea mtoto wake ananiuliza wakati anazaa nje wewe ulikua wapi nikakata cmu sikutaka kuendelea kumsikiliza
Tatizo jingine huyu wife analazimisha kua ataondoka ila lazima aondoke na watoto wake wote,
Mwache aondoke tu, hao watoto itafahamika mbele ya safari la ukithubutu kusamehe hilo kosa utajuta milele
 
Mkuu umeandika mengi na mazuri Sana
Jamii yangu Niko nayo vzr Sana
Kuhusu kujisimamia najisimamia vyema Sana, hua sipendi Shari na wife wangu labda itokee bahati mbaya
Sina mengi mkuu yakuandika
Huyo mwanamke bado yupo kwako tu?
 
Na hapo mimba iliingia mapema kabla ya kusafiri kwenda mwanz. Kama angedinywa kipindi kile cha safari na Mshikaji naye akafika anashindilia Hakika 100% asingeshtukia mchezo na angetulia.

Hapa ndio mhone wanaume tunapigwa sana
Kwakweli 'nahona' na mtapigwa sana tu km hata kuandika hujui sasa ije kuwa kubambikiwa mimba,,
 
Huyo mwanamke bado yupo kwako tu?
Hapana mkuu nimemuwezesha kwa jinsi alivyoomba na Sasa Yuko huko kwa wachungaji wake sijui baba wa kiroho wake anajishauri aanzie wapi maana kwenda kwao ni mtihani maana anaujua mziki wa kwao kwa maana ya life la pale, kwa mzinzi mwenzake ndo cjui anawaza nn
Ila nimepiga makufuri mapya yote kuanzia kwenye Geti la kuingilia,mlango wa kuingilia hadi milango ya vyumba vyote sihitaji kusikia jambo lolote aiseeee
 
Samehe msonge mbele. Hayo mawazo mengi ndo yanazalisha chuki .You only live once.
Nakuelewa Dada ila kwa Sasa nikikumbuka tulikotoka na jinsi niliswaga ng'ombe kwenda kwao na jinsi niko napambana kwa ajili yake, na nimekua nikimwambia yy ndie ndugu yangu japo ninao ndugu kibao niliozaliwa nao namwambia tulia uhakikishe wanao wanapata elimu bora na mazingira mazuri ya maisha hasa baada ya kumaliza masomo taarifa zangu zote za kitumishi nimempa kipaumbele alafu leo ANATAFUNWA kizembe namna hii pengine alikua anavizia watoto wangu wamelala analiingiza ndani kwangu hilo BALOBALO lake nyumba niliyojinyima kuijenga

Hapana,,,, ninazijua hasira zangu ndio maana hata hua naogopa kumpiga hata wanangu najitahidi kutumia diplomasia zaidi ktk kuwajenga najua nikinyanyua mkono kumuadhibu aiseee hata mama yake mwenyewe ANAWEZA kimbilia polisi
 
Pole sana najua kakukosea. Na umefanya vizuri kumpeleka kwao. With time utaheal na utamrudisha nyumbani.
Kuna baba mmoja alifungwa jela miaka mitano. Alivyotoka jela alimkuta mkewe kazalishwa mtoto mmoja. Nae alichukia sana (Which is normal)Ila baadae vikao vya familia na mke kuomba msamaha. Alimsamehe mkewe wakarudiana na wakazaa watoto watoto watatu. Kumbuka kabla ya kufungwa walikuwa wamezaa mmoja ,ndo mkewe akazaa nje mmoja tena.Sasa wanaishi na watoto wao 5 including yule wa mke .Samehe na inawezekana kabisa.
 
Pole sana. Ni kweli mkeo kakukosea. Binafsi nilizaa nje ya ndoa na hii ilisababishwa na hasira zangu baada ya mme wangu kuzaa nje ya ndoa na wanawake wanne tofauti. Baadae akasema hanitaki akahama na nyumbani. Mimi sasa nikatulia na nikajihesabu ni mjane. Tulikuwa na watoto watatu mimi na yeye. Baadae nikaamua tu kubeba mimba ya mwanaume mwingine (Hii ni baada ya mme kusema hanitaki na akaondoka home) alikaa miaka 5 hayupo home wala hatuwasiliani kabisa .Mara siku ya siku akaja akanikuta tumbo hilo.Salale alilia kama mtoto🤣.Nyie wanaume bwana tokea siku hiyo nikajua kumbe wanaume ni wa binafsi sana. Yaani alisahau kuwa yeye ana watoto nje ya ndoa. Mimi kuzaa kamoja tu tena baada ya yeye kunikataa.
Ila hapa naona mkeo ndo kakosea sana. Maana wewe hauna hata watoto nje. Pole ila still waweza msamehe.
 
Pole sana najua kakukosea. Na umefanya vizuri kumpeleka kwao. With time utaheal na utamrudisha nyumbani.
Kuna baba mmoja alifungwa jela miaka mitano. Alivyotoka jela alimkuta mkewe kazalishwa mtoto mmoja. Nae alichukia sana (Which is normal)Ila baadae vikao vya familia na mke kuomba msamaha. Alimsamehe mkewe wakarudiana na wakazaa watoto watoto watatu. Kumbuka kabla ya kufungwa walikuwa wamezaa mmoja ,ndo mkewe akazaa nje mmoja tena.Sasa wanaishi na watoto wao 5 including yule wa mke .Samehe na inawezekana kabisa.
Sawa asante

Nawashukuru wadau wote kwa ushauri mlionipa, na kwa wale mliotoa ushauri kua nisamehe na kwa jinsi mlivyowasilisha nimewaelewa ( ILA MMENIFANYA NISEME HIVI KAMA HAMTOJALI NITALETA MKASA MZIMA KUANZIA NAKUTANA NA HUYU BINTI NILIYOMVUMILIA AMBAYO BADO YANAFANANA NA HILI NA PENGINE NAWAZA YULE MTU ALIEKUA ANACHATI NAE NDIE HUYU PIA NA MAPUNGUFU YANGU MAANA SIWEZI SEMA MM NILIKAMILIKA NA TABIA YA FAMILIA NZIMA HASA MAMA MKWE AMBAE SIKUTAKA KUMZUNGUMZIA SANA)

Episode hazitazidi 3 na hii AMBAYO ilitakiwa kua ya mwisho maana nilivumilia Sana lkn ktk hili yamenifika shingoni ndio maana nikaleta nipate mawazo ya wadau
 
Naomba nikuulize. Na wewe umezaa nje ya ndoa ?I mean mkiwa tayari mmeoana. Be honest please.
 
Naomba nikuulize. Na wewe umezaa nje ya ndoa ?I mean mkiwa tayari mmeoana. Be honest please.
Sijawahi na Wala ckuwahi kufikiria kutokana na migogoro ambayo nimekua nikishuhudia
Na hata yy mwenyewe alikua akinambia ni bora uchepuke lkn sio kuzaa nje ya ndo huyo mtoto cku ukimleta kwangu namwagia maji ya moto bora nikafungwe lkn sio wewe kuleta mtoto hapa kwangu, sitakubali kile tulichotafuta wote mwingine aje akifaidi

Daaaah hii kauli nikiimbuka namwagizia bia kila mtu niliekaa nae kwenye hii meza inauma Sana tena Sana
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom