Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

Mkuu mm ni mtumishi ktk MOJA ya taasisi yenye jukumu la kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia na kuzalishwa nchini pesa ya kubadili mboga na kusomesha watoto shule nzuri na kuwapa mahitaji yote wanayohitaji siwezi kukosa, hata mwaka huu nilipanga kumnunulia wife ka usafiri ili akiwa anaenda kanisani na watoto wake basi anajiachia kwenye ka ist kake lkn Sasa ndo hivyo
Na anasema mwamba aliemzalisha anaishi kwa mjomba wake, cjui kama ni kweli ama laaa
Kwa kweli mrudishe huyo mama kwao! Usije fanya maamuzi mabaya! Huyo muongoo Ana hitaji huruma kuwa Kazaa na kapuku jiuluze kwanini awe Ana ng'ang'ania Jina La mtoto liwe analo pendekeza yeye? Wewe ni mpole aisee Angekuwa mwana ume mwingine Angekuwa Hana meno
 
Kaka mtu kasema hata yy ni mwanaume hawezi kukubaliana na mke wake kuzaa nje ya ndoa ni bora angefanya mapenzi tu kama kweli alikua amezidiwa ikaisha lkn sio kuzaa nje hiyo ni dharau akanambia nimpeleke kwao

Mama mkwe yy anamtetea mtoto wake ananiuliza wakati anazaa nje wewe ulikua wapi nikakata cmu sikutaka kuendelea kumsikiliza
Tatizo jingine huyu wife analazimisha kua ataondoka ila lazima aondoke na watoto wake wote,

Ungekuambia Kwa hiyo Binti Yako amerithi kutoka kwake? Umsikilize atakavyosema
 
Hii ni kweli 100% . Nimeamua kuwa na mtu mmoja why nihangaike na wengine. Hata uje kwa gia gani siwezi msaliti mume au mpenzi wangu. Yaani badala kuwa busy na familia yako uko busy na kuchepuka. Hivi hata hamu inakuja kweli kutembea nje ya mahusiano yako? Wanawake tujiheshimu, tunatia aibu jamani
Ngoja nimpigie simu sangoma wangu wa kinole anipe mchakato wa kuja kukutongoza nione kama utabaki njia kuu🤣🤣🤣
Mambo vipi mrembo
 
Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.

Nilihamishwa kikazi kutoka Dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikuwa mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na Dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.

Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikuwa anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.

Nilikuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kuwa wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokuwa zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mimi mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.

Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia simu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.

Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kuwa yawezekana nimeshakanyaga waya.

Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)

Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba.

Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama ni kujifungua basi itakuwa mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa

Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana (mtoto wa kiume, ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)

Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mimi nasema kama mimi ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mimi nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitumika ndio kwa mbaali wakapunguza.

Jina hili limeendelea kuitwa na kutajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo, mimi nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo.

Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kufanana na wakubwa zake Wala mimi Wala yeye mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha.

Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kugombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawa imetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lakini moyoni naumia Sana.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi, huwa nakuwa na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokuwa yangu.

Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mimi hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba.

Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kuwa mimi uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili, nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mimi aniache nilee watoto wangu wawili

Naombeni USHAURI WENU wadau mwenzenu, niko dilemma.

NB: Matusi nisingependelea kuyaona
Nashauri ukae mbali nae hili suala halitakuja kuisha moyoni mwako hasa ukiwa unawaona hao wawili,

Chamsingi achana nae ikibidi aende akamlee huyo mtoto na baba yake aliyezaa nae.

Lakini pia nikupongeze kwa kuw mpole na mtulivu kwa kipindi hicho wakati unatafuta ukweli na baada ya kuujua ukweli,, maana yahitaji moyo saana.
 
Sasa hivi atakuwa mpole na kujiliza akionyesha kujutia alichofanya, sasa fanya ujinga wa kujifanya ngoja niamue tu yaishe, atasahau kila kitu na mwisho wa siku utashangaa kukuta msg za mapenzi wanawasiiliana na lijamaa lake...

😂😂😂

Kuna mambo hayahitaji ushauri wala mjadala
 
Pole sana mkuu kwa jambo zito lililo mbele yako, unahitaji utulivu sana wa maamuzi juu ya hatima yako,Mungu akusimamie na kukupa hekma katika kipindi hichi

Ushauri wangu kabla hujaamua kuchukua maamizi ya jumla kawapime D. N. A hata haya watoto wawili unaodhani ni wako ili uweze kujua ukweli ni upi, coz najiuliza maswali machache.

Kama mwanamke anajua kabisa amecheat juu ya ujauzito kwanini asingekuwa mtulivu na mwenye busara hata kutokulazimisha jina ambalo wewe hulipendi kwa mtoto aliezaa nje ya ndoa.

Huenda ana uzoefu na alichofanya, kwa mwanamke mwingine asingepata hata nguvu ya kuanza kubishana juu ya jina la mtoto, baada ya majibu ya D.N.A utajua nini cha kufanya.
Uko sahihi Mkuu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom