Nimebaini mke wangu amezaa nje ya ndoa na amekiri, naombeni ushauri

dada ukitaka ushindane na mwanaume hutoweza,eti yeye anachepuka nami ngoja nichepuke,mwanaume ni ngumu kuvumilia usaliti mi binafsi nakaa mbali na familia lakini suala la mchepuko nshakataa kwanza unajitunzia heshima
Hivi Kuna mahala nimesema nashindana na mwanaume,, watu wengine bhana,,
 
Pole sana ndugu kwa hili, lakini mtu hupewa jaribu analolimudu. Mm nna amini utalimudu.

Japo kwa umri uliokiri kua chini ya miaka 35 jaribu laweza kua zito, giveni mazingira tunayoishi sasaivi. Ndugu mm nnakwenda kinyume na wengi waliokushauri hapa, kuna mchangiaji mmoja alisema "Iko namna wazee wa zamani walikua wanahandle matatizo kama haya". Nnaunga mkono hoja ya huyu mchangiaji kwa 100%.
Kuna siku nlipata wasaa wa kupiga story na mzazi wangu basi katika maongezi nlikuja kugundua kua ndugu zake kadhaa kwa mama yake mdogo (Baba yake alikua na wake wawili) hawakua watoto wa Baba yake. Babu yetu alilipokea na hao watoto wamekua wa kwake na kurithi vya kwake.

Basi tena siku moja nikiwa safarini, nikapata kuskia story nyingine iliwahi kutokea Bukoba. Hii ilikua mbaya zaidi maana kwenye ndoa hii mama wa familia alichepuka na padre, tena padre wa kizungu. Akamzaa mzungu kwenye familia ya wahaya weusi tiii. Kila mtu akajua, jamiii ikajua. Bahati nzuri au mbaya yule padre wa kizungu muda wake ukawa umeisha akarudi kwao Ulaya.

Basi katika familia hio yenye Mzungu chotara, maisha yaliendelea as if nothing happened. Basi kwasababu jambo lilikua dhahiri sana, wazee wenzake na Baba wa familia hio wakawa wanamtania sana kilabuni, "Unakaa kaa kibwege mpaka mkeo anakuzalia mzungu na unaendea kuishi nae. Yule mzee aliyapokea yote akayabeba akalea familia yake kwa upendo mkubwa.
Amini usi amini, unaambiwa katika familia ile watoto wote walisoma ila yule wa kizungu ndo alikuja kutoboa kimaisha. Amewajengea wazazi wake nyumba kijijini na anawasaidia ndugu zake. Yaani yy ndo amekuja kua mkombozi wa hio familia.
Sasa naskia sikuhizi Mzee akienda kilabuni anatamba kweli kweli kwa fedha ya mwanae huyo mzungu, na hakuna anaeinua mdomo. Si unajua wahaya tena na tambo zao.

Kaka, ww sio wa kwanza na wala hautakua wa mwisho kutokewa na jaribu la namna hii. Kuna mchangiaji mmoja hapo juu amesema, "Jaribu kuangalia na mazuri ambayo Mungu amekujalia, wale watoto wawili wa mwanzo". Angalia pia na mazuri mengine ambayo mkeo amekufanyia amekubali kua mkeo na kukuzalia watoto, amekubali kuishi na wewe.

Usiangalie sana majibu anayokupa mkeo au mama mkwe sasaivi, na yeye yupo katika hali ya taharuki na kujihami hawezi kua perfect. U perfect wake mm nnaupima kwa matendo aliyofanya mwanzo baada ya kuteleza. kwanza hakutoa mimba, pili alifanya jitihada muishi pamoja tena. Mkeo ni mtu mwema sana ni kuteleza kibinadamu tu. Ww ndie mwenye hatma ya maisha yake ya ndoa usijiweke kwenye thinking level moja na yeye (Lead/Ongoza).

Kaka unadhani ni akina mama wangapi kwenye ndoa wanazini na hawapati mimba, au wanapata mimba na kuzitoa, au wanapata mimba na kuzizaa bila waume zao kujua. Au wanapata mimba na kuzaa na waume zao wakajua ila wakakaa kimya. Au wakapata mimba wakazaa, mume akajua na jamii ikajua ila wakaendelea na maisha.

Ndio maana kukawa na msemo kitanda hakizai haramu, lkn pia ndoa maanake ni kua mtoto yyte anayezaliwa na mkeo ni wa kwako ni mali yako na atarithi jina la ukoo wako.

Ww ndie mwenye hatma ya huyo mtoto pia. Unaweza kusema apelekwe kwa baba aliyemzaa. Je kama nae ni mume wa mtu..! Huyo mtoto ni wako na unapaswa kumlea vizuri. Tena uji control asijue na wale wengine wasijue, mtunzie heshima mkeo na usilete taharuki kwa watoto wako wale wawili. Mpende mkeo muishi kwa amani, huo ndio uanaume.

Ili sasa uweze kujiepusha na stress na kuwaza sana hilo tafuta vitu vya kukuliwaza kama mchepuko, pombe na marafiki ila utumie akili pia wakati unaingia huko. Kumbuka mwenye hatma ya ndoa yako ni ww na ww ndie unaepaswa ku lead hio hatma.

Kaka trust me ukifanya hivyo mkeo atakupenda sana, atakupambania na kukuheshimisha siku moja. Atakua tayari kuipambania familia yenu kwa jasho na damu.

Asante
Kwahio jamaa awe mlevi na mchepukaji kama njia ya kujiliwaza kwa maumivubya kuchapiwa.? Unaona hayo ndio yatakua maisha sahihi?
Na mke hajamuheshimu angemuheshimu asingelazimisha jina la mtoto alilotoa mchepuko ndio aitwe mtoto.
 
Hana ubavu wa kuondoka na watoto wote komaa nae Tena hata Sheria zitambana sio mama mzuri kwanza,anataka aondoke na hao ili umhudumie na huyo mwingine ukute baba ake marioo tuu!!Hana mbele wala nyuma
Hivi ndio mpaka azae kweliii ukishaona mpaka mwanamke kaamua kuzaa nje ni kadhamiria huyu mwanamke aliamua tu kwa maksudi yake

Halafu jamaa anaonekana mpole sana na mstaarabu na mkewe amempanda kichwani na kingine usikute baba mtoto kweli marioo kashamchanganya mwanamke wa watu

Maamuzi aliyofanya mleta mada naungana naye
 
Msamehe mkeo kama ni mtoto wa kike akikua chakata mbususu babuu , unafukuza utamu wa badae , enyi mabaharia jiwekeeni akiba ya baadae kama ndondo wafanyavyo.
 
Kumfukuza mkeo haiwezi kubadilisha historia zingatia haya;
1. Kama hujawahi kumsaliti una haki kumfukuza lakini kama umewahi potezea hiyo huitwa ngoma droo 1:1

2. Unawapenda wanao?
Unajua kuwa wanao wanahitaji malezi ya wazazi wote wawili? Jali furaha ya watoto wako.

Potezea tu
Mkuu hata kama nimechepuka ndio yy akachepuke na kuzaa kabisa sina tatizo na yy kuchepuka ila tatizo kuvuruga amani ya familia yangu kwa kuleta mtoto wa nje
Ni bora baba ulete mtoto wa nje lkn sio mama aiseee hiyo haina heshima kabisa
 
Acha wewe unaongea na watu waliopeleka watoto....

Mtoto amefanya mtihani Tena sio seven Four years of age... Anapigwa paper. Na asipofikisha 80 hapati nafasi.
Shule gani hiyo itaje jina?

Tuone ukweli wako,maana kuna members humu wanaijua huenda unadanganya vile vile!

Itaje tu-verify hapa kwamba enrolment ya mtoto wa 4 years anapewa "academic examination"!
 
Ni kweli kabisa kiongozi, ndio maana Kwa usalama wa mleta mada ni Bora atemane na huyo mke wake.
Sababu mahusiano ya mkewe na mchepuko hayataisha tena kazalishwa na mchepuko daaah. Ila inauma sana Aisee.
Mtoa mada pole Sana aisee hili jambo lisikie tu kwa mwenzako
 
Hivi ni kwanini wanandoa wakichepuka matumizi ya condom huwa bonge la changamoto
 
Tena nmekumbuka kama jamaa mleta Uzi Hana wazifa. Basi atulie awe mpole.

Wanamama ukiwa Huna kitu. Maaanina kabisa
Mkuu mm ni mtumishi ktk MOJA ya taasisi yenye jukumu la kudhibiti ubora wa bidhaa zinazoingia na kuzalishwa nchini pesa ya kubadili mboga na kusomesha watoto shule nzuri na kuwapa mahitaji yote wanayohitaji siwezi kukosa, hata mwaka huu nilipanga kumnunulia wife ka usafiri ili akiwa anaenda kanisani na watoto wake basi anajiachia kwenye ka ist kake lkn Sasa ndo hivyo
Na anasema mwamba aliemzalisha anaishi kwa mjomba wake, cjui kama ni kweli ama laaa
 
Ni kweli kabisa kiongozi, ndio maana Kwa usalama wa mleta mada ni Bora atemane na huyo mke wake.
Sababu mahusiano ya mkewe na mchepuko hayataisha tena kazalishwa na mchepuko daaah. Ila inauma sana Aisee.
Mtoa mada pole Sana aisee hili jambo lisikie tu kwa mwenzako
Asante mkuu
 
Naomba niende kwenye mada, mimi na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wa pili mwaka 2018.

Nilihamishwa kikazi kutoka Dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikuwa mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na Dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.

Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikuwa anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.

Nilikuwa naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kuwa wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokuwa zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mimi mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.

Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia simu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.

Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kuwa yawezekana nimeshakanyaga waya.

Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mimi nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kuwa mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti, (mimba ilionekana kubwa)

Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba.

Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama ni kujifungua basi itakuwa mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa

Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana (mtoto wa kiume, ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)

Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mimi nasema kama mimi ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mimi nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitumika ndio kwa mbaali wakapunguza.

Jina hili limeendelea kuitwa na kutajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo, mimi nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo.

Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kufanana na wakubwa zake Wala mimi Wala yeye mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha.

Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kugombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mimi kuwa nilikuwa mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawa imetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lakini moyoni naumia Sana.

Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi, huwa nakuwa na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokuwa yangu.

Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mimi hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba.

Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kuwa mimi uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili, nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mimi aniache nilee watoto wangu wawili

Naombeni USHAURI WENU wadau mwenzenu, niko dilemma.

NB: Matusi nisingependelea kuyaona
Umefanya maamuzi sahihi...usiutese moyo.Maisha lazima yaendelee ndugu. Usije fanya mambo ya ajabu maana shetani anaweza kupitia hapo hapo. Let it go!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom