Reciprocal
JF-Expert Member
- Jan 6, 2022
- 325
- 507
Kwasasa hivi, mimi naona umrudishe kwao ili upate muda wa kutafakari ukiwa peke yako. Akili yako itakapotulia na kukubali kuwa kosa alilofanya mke wako ni la kawaida na hivyo huoni shida kuwa naye licha ya mapungufu aliyoonesha hapo unaweza kumrudisha. Kama moyo unagoma kusamehe, ni vema ukawa naye mbali.Naomba niende kwenye mada, mm na mke wangu tulioana mwaka 2015 japo tulianza mahusiano muda mrefu kidogo na mtoto wetu wa kwanza tulimpata mwaka 2013, na wapili mwaka 2018.
Nilihamishwa kikazi kutoka dar kwenda moja wapo ya mikoa ya kanda ya ziwa, hiyo ilikua mwaka 2019 ikabidi wife na watoto wabaki huko mkoa jirani na dasalamu yaliko makazi yetu ya kudumu.
Sababu ya kuibakiza familia huko ni kwamba first born wetu alikua anasoma na ukizingatia huku nilikohamia bado sijajiimarisha vyema.
Nilikua naenda kuwatembelea mara kwa mara na wao pia niliwapa fursa ya kua wanakuja ninakofanyia kazi mara tu shule zilipokua zikifungwa. Nilipanga kuihamisha familia yangu kuja kuishi na mm mara baada ya kukamilisha taratibu za kumhamisha binti yangu kipenzi na pia kumpata mtu sahihi atakaeishi kwenye nyumba yangu.
Mwaka Jana mwanzoni mwa mwezi wa sita mke wangu alinipigia cmu akanieleza kwamba anataka kuhamia huku niliko hivyo nianze taratibu za uhamisho, nami bila kufanya hiana nikaanza hatakati za kupata nafasi ktk shule nzuri za private ktk mkoa huu baada ya shule kufungwa wife na watoto wetu wawili wakatia nanga dogo akaenda akapiga paper akafaulu akapata nafasi hiyo ni mwezi wa saba 2021.
Maisha yakaendelea, mwezi wa nane wife akanambia ana mimba, tukaenda kuhakiki kweli nikadhibitisha ni mjamzito sikutaka kuhangaika na mambo ya mimba ina muda gani
Harakati za CLINIC zikaanza tukaenda tukacheki afya wote tupo sawa japo wife alinihofia Sana kua yawezekana nimeshakanyaga waya
Ilipofika mwezi wa 12 wife akaanza kunambia UNAJUA SIKU HIZI MAMBO YAMEBADILIKA SANA MJAMZITO ANAWEZA KUJIFUNGUA HATA MIEZI TISA HAIJATIMIA, mm nikawanamuuliza hayo mabadiliko yameanzia kwako au ni kwa wajawazito wote na je hiyo ni sayansi ya wapi huku nikimtania kua mbona hiyo mimba yako nikipiga hesabu ulivyofika hapa na jinsi inavyoonekana ni tofauti,(mimba ilionekana kubwa)
Ukweli ni kwamba wife alifika huku ninakoishi mwezi wa saba Kati ya tarehe 15 hadi 23 mwezi wa saba
Kwa haraka haraka kama ni mimba niliipigia hesabu za mwezi wa nane na kama nikujifungua basi itakua mwezi wa nne katikati au mwishoni kabisa
Kilichonishtua ni mke wangu KUJIFUNGUA tarehe za mwisho wa mwezi wa pili huku mimba ikiwa imemchosa Sana ( mtoto wa kiume,ambae Sasa ni mtoto wetu wa 3)
Kilichoanza kunishtua wife anakomalia mtoto apewe jina W na mm nasema kama mm ndie baba wa huyo mtoto basi ataitwa jina Q, tukaendelea kutana Sana na ikumbukwe mm nashinda Sana kazini hivyo hata wakubwa zake wakawa wanamuita jina hilo analolitaka mama yao ikabidi niwapige marufuku kumuita mdogo wao jina hilo na hadi fimbo zilitimika ndio kwa mbaali wakapunguza
Jina hili limeendelea kuitwa na kitajwa na waumini wenzake na wife hata wakija kumtembelea utasikia wanamuita jina hilo mm nakausha naamua kusepa zangu naenda kumwagilia moyo
Ikabidi nikae na wife nimuulize kinagaubaga juu ya kweli wa mimba kujifungua jina pamoja na mtoto kutokuonyesha dalili za kuwafanana wakubwa zake Wala mm Wala yy mwenyewe, wife hakusema kitu japo alionekana kuna jambo anaficha
Niliendelea kumuuliza pasipo kumpiga Wala kuhombana ndipo wife alipoamua kunichana ukweli huku akimsingizia shetani na kunilaumu mm kua nilikua mbali nae akateleza mara moja akafanya ndo ikawaimetokea hivyo, nikatulia sikumshirikisha mtu mwingine hata kidogo maisha yakaendelea lkn moyoni naumia Sana,
Na kadri siku zinavyozidi kwenda nakosa uvumilivu ukizingatia natumia kilevi hua na kua na mawazo mengi Sana nikifikiria kuilea damu isiyokua yangu
Hakika kwa umri wangu huu wa chini ya miaka 35, jamani mm hili jambo limenishinda kabisa naona sitaweza kulibeba
Jana nimemweleza kaka yake mkubwa pamoja na mama yake kua mm uzalendo umenishinda nisijefanya maamuzi mengine yakagharimu pande zote mbili nimeomba mke arudi kwao au aende kwa huyo aliezaa nae mm aniache nilee watoto wangu wawili
Naombeni USHAURI WENU wadu mwenzenu Niko dilemma
NB; matusi nisingependelea kuyaona
Ila kuendelea kuugulia moyoni na wahusika wa maumivu wapo katika mazingira yako ni hatari kwako na familia yako( hivyo ni vema ukawa nao mbali hadi pale maumivu haya ya moyo yatakapopotea) .