EZZ CHEZZ
JF-Expert Member
- Apr 10, 2011
- 1,230
- 1,352
Nimeshindwa kuki-attach. Ingia google download kitabu cha UTENGENEZAJI CHAKULA CHA KUKU cha LRDCVyanzo vizuri zaidi vya madini ni mifupa na chokaa chokaa. Vyote hivi vinapatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Pia waweza tumia DCP au Premix.
Chanzo kizuri zaidi cha protein ni soya. Ila kumbuka protein yoyote itokanayo na mimea hukosa elementi mbili za Lysine na Methionine. Hivyo utalazimika kutumia premix yenye hivyo viwili ndani yake.
Hakikisha pia chakula chako kinawekwa virutubisho kwa uwiano sahihi. Mfano, protein yapaswa kuwa 16% - 22% ya chakula chote. Angalia kwenye desa la uandaaji chakula cha kuku lifuatalo.