Hivi inakuwaje kuku analalia mayai 10 mwisho vinatoka vifaranga v2 shida iko wapi
 
Baada ya safari ya muda mrefu wa kujibana matumizi nimefanikiwa kujenga baada pembezoni mwa nyumba yetu lenye eneo kubwa la uzio wa matofali. Nimeanza kwa kununua kuku wa kienyeji wadogo wa miezi miwili na mitatu 100 nategemea kuwa na majogoo 20 na wanaotaga 70. Malengo niliojiwekea ni kuku 50 watage kwa awamu mbili kwa mwaka huu. Kila kuku awe na vifaranga 6 kwa awamu moja, hivyo kwa awamu mbili kila kuku nategemea awe na watoto 12 nikizidisha na kuku 50 napata kuku 60 ambayo nitauza kwa Tsh 6000 kwani sitangoja wawe wakubwa sana. Hivyo kwa mwaka huu natarajia kukusanya Tsh 3000000. Soko langu limelenga sikukuu mbili kubwa. Yaani Eid na Christmas. Mungu nisaidie nifanikiwe malengo yangu. Naombeni ushauri, maoni na pia nikosolewe kama ninakosea.

Pia hela ya kununulia chakula na dawa nimeshaandaa angalau kila mwezi laki moja kwani ni kuku wa kienyeji ambao wanakula pumba tu.

Niko Muheza Tanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera kwa maamuzi mazuri na huu ni ushauri kwako,
Nianze kwa kuweka wazi kwamba zoizi hili nilishalifanya na nilifanikiwa sana japo kwa sasa nahangaika na michakato tofauti,

Tofauti yangu na wewe ni kwamba wewe utaanza na kuku wengi wakati mimi nakumbuka nilianza na tetetea 12 na jogoo moja na ndani ya mwaka kuku hawakupungua 300.
Mimi niliwatumia wazazi kwa kuatamia lakini walipototoa vifaranga niliwapokonya na kutunza kwenye vibanda vidogo(bruda) na mama zao nilifungia kwenye mabanda ya pembezoni wasiweze hata kusikia milio ya vifaranga vyao huku nikiwalisha hawa wazazi vyakula vizuri.Kwakufanya hivi kama watachanganywa na jogoo hutaga kwa haraka sana ndani ya wiki tatu.

Changamoto kwako wewe unaanza na kuku wengi.Kwakawaida kuku wanapokuwa wengi ni rahisi kuanza kutaga pamoja na hapa ndipo kunahitaji umakini.

Kuku ili aatamie vizuri anahitaji awe kwenye sehemu isio na bugudha jambo ambalo idadi inapokuwa kubwa huwa ngumu kidogo.Ni rahisi sana ukakuta sehemu kuna kuku anaatamia huku wengine wakamsumbua wakitaka kutaga hapohapo.Hii hupelekea kushusha ufanisi wa uanguaji kwani Mayai mengi huharibika.

Jitahidi sana kuwa makini pindi hali hii itakapojitokeza ukabiliane nayo vizuri vinginevyo itakusumbua.

Nakutakia kila la kheri na Mungu akutangulie.
 
Hivi inakuwaje kuku analalia mayai 10 mwisho vinatoka vifaranga v2 shida iko wapi
Shida yaweza kuwa kwenye mayai, kuku anayeatamia au mazingira yanayomzunguka kuku anayeatamia (management yako mfugaji).

Mayai sharti yawe bora. Yawe yamerutubishwa vema na jogoo. Hapo ratio sahihi ya tetea/jogoo ndiyo suluhisho. Tetea 10 wawe na jogoo 1.

Pia mayai yasikae muda mrefu. Mwisho siku 14 tangu yatagwe. Mayai yasiwe na nyufa, mawimbi, umbo dogo au kubwa sana, na pia yasiwe na unyevu/uchafu.

Kuna kuku si waatamiaji wazuri. Hatulii kwenye kiota. Huyo lazima aharibu mayai.

Kuhusu mazingira, hakikisha kuku anayelalia ametengwa peke yake asisumbuliwe na kuku wengine. Pia maji na chakula viwe jirani na vitosheleze. Avipate on demand! Acha kumsumbua sumbua ikiwa unafanya hivyo.

Kazi kwako.
 
Kaka kuku kuchi huwa sio wazuri sana kama utahitaji kufuga kwa biashara labda ujifurahishe tu... maana huwa sio watagaji na majogoo wake hupenda kuendekeza ngumi hadi wanajisahau kupanda na uzito wao huwa unachangia....
Hata Mie nimeanza kufuga kwa kuku kuchi 2 na dume lake 1 sasa Nina vifaranga vya kuku kuchi 13 vya mwezi 1 matarajio yangu hadi mwezi wa sita mtakua nao wengi kwa kuuza biashara
 
Nunua vifaranga hao wakubwa utapata hasara sana
Kuna binadamu hawana huruma kabisaa mwaka 2017 mwisho december nilinunua kuku kutoka mbeya jumla majike na majogoo kama 70 ila mpaka hivi hela hawajaongeza kabisaa zaidi naona wamebakia 30 kila siku mfanyakazi anasema wanaumwa na kufaaaaa
 
Mkuu niruhusu tuwasiliane DM tubadirishane mawazo kwa kuwa na mimi niko kwenye maandalizi ya kufuga
 
Baada ya safari ya muda mrefu wa kujibana matumizi nimefanikiwa kujenga baada pembezoni mwa nyumba yetu lenye eneo kubwa la uzio wa matofali. Nimeanza kwa kununua kuku wa kienyeji wadogo wa miezi miwili na mitatu 100 nategemea kuwa na majogoo 20 na wanaotaga 70. Malengo niliojiwekea ni kuku 50 watage kwa awamu mbili kwa mwaka huu. Kila kuku awe na vifaranga 6 kwa awamu moja, hivyo kwa awamu mbili kila kuku nategemea awe na watoto 12 nikizidisha na kuku 50 napata kuku 60 ambayo nitauza kwa Tsh 6000 kwani sitangoja wawe wakubwa sana. Hivyo kwa mwaka huu natarajia kukusanya Tsh 3000000. Soko langu limelenga sikukuu mbili kubwa. Yaani Eid na Christmas. Mungu nisaidie nifanikiwe malengo yangu. Naombeni ushauri, maoni na pia nikosolewe kama ninakosea.

Pia hela ya kununulia chakula na dawa nimeshaandaa angalau kila mwezi laki moja kwani ni kuku wa kienyeji ambao wanakula pumba tu.

Niko Muheza Tanga

Sent using Jamii Forums mobile app
MWENYEZI MUNGU AIBARIKI KAZI YA MIKONO YAKO, NDUGU YANGU. HEKO!!
 
Hongera kwa wazo zuri
 
Msaada Wandugu... Kuku wanaokula mayai, dawa Yao NI nini ili waache..??
Pia tatua tatizo la msingi. Kuna virutubisho wanakosa kwenye chakula unachowapa. Madini &/ protein. Rekebisha chakula. Usipofanya hivyo hawaachi hata uwakate vipi.
 
Pia tatua tatizo la msingi. Kuna virutubisho wanakosa kwenye chakula unachowapa. Madini &/ protein. Rekebisha chakula. Usipofanya hivyo hawaachi hata uwakate vipi.
Asante kiongozi, unaweza nitajia aina ya vyakula inayoweza ondoa shida hiyo?
 
Asante kiongozi, unaweza nitajia aina ya vyakula inayoweza ondoa shida hiyo?
Vyanzo vizuri zaidi vya madini ni mifupa na chokaa chokaa. Vyote hivi vinapatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Pia waweza tumia DCP au Premix.

Chanzo kizuri zaidi cha protein ni soya. Ila kumbuka protein yoyote itokanayo na mimea hukosa elementi mbili za Lysine na Methionine. Hivyo utalazimika kutumia premix yenye hivyo viwili ndani yake.

Hakikisha pia chakula chako kinawekwa virutubisho kwa uwiano sahihi. Mfano, protein yapaswa kuwa 16% - 22% ya chakula chote. Angalia kwenye desa la uandaaji chakula cha kuku lifuatalo.
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom