Pambana mjasiliamali mwenzangu,kuku wa kienyeji utahitajika kuwajali dawa na msosi,japo pia msosi huwa wanajitafutia kitu ambacho hutupunguzia gharama wafugaji..
Jitahidi ujue dalili za magonjwa mbalimbali ya kuku,hii itakusaidia kupunguza vifo vya kuku..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
f
Baada ya safari ya muda mrefu wa kujibana matumizi nimefanikiwa kujenga baada pembezoni mwa nyumba yetu lenye eneo kubwa la uzio wa matofali. Nimeanza kwa kununua kuku wa kienyeji wadogo wa miezi miwili na mitatu 100 nategemea kuwa na majogoo 20 na wanaotaga 70. Malengo niliojiwekea ni kuku 50 watage kwa awamu mbili kwa mwaka huu. Kila kuku awe na vifaranga 6 kwa awamu moja, hivyo kwa awamu mbili kila kuku nategemea awe na watoto 12 nikizidisha na kuku 50 napata kuku 60 ambayo nitauza kwa Tsh 6000 kwani sitangoja wawe wakubwa sana. Hivyo kwa mwaka huu natarajia kukusanya Tsh 3000000. Soko langu limelenga sikukuu mbili kubwa. Yaani Eid na Christmas. Mungu nisaidie nifanikiwe malengo yangu. Naombeni ushauri, maoni na pia nikosolewe kama ninakosea.

Pia hela ya kununulia chakula na dawa nimeshaandaa angalau kila mwezi laki moja kwani ni kuku wa kienyeji ambao wanakula pumba tu.

Niko Muheza Tanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Good! İla umrlrkosea kitu hapo, unalenga kuuza kipindi cha sikukuu lakini kuku wadogo! Sikukuu hawalagi kuku wadogo hula kuku kamili.Kuwafungia kuku ktk uzio maana yake watakuwa hawashibi na wewe ndio itabidi ufidie chakula.Hapo itabidi uwe na ng'ombe ili kuvutia wadudu.
 
SEZARI AQUACULTURE SERVICES iliyopo ndani ya jiji la MWANZA, inakuletea Huduma bora za ufugaji Samaki( viumbe hai Wa majini), tunatoa Huduma zifuatazo: uchaguzi Wa eneo la kuchimba bwawa, uchimbaji Wa mabwawa, ujenz Wa mabwawa Na kuweka plastic sheet kama n lazima, urutubishaji wa bwawa Na kukinga magonjwa ya Samak, kupima ubora Wa Maji ya kufugia Samaki, Vifaranga bora Vya Samaki aina ya sato Na kambale, Vyakula bora Vya Samaki, utengenezaji Wa Cage( ufugaji kwenye vizimba), uzalishaji wa vifaranga bora vya samaki, utengenezaj Wa Aquariums, usafirishaji, Pamoja Na Huduma zote za ufugaji Samaki piga simu namba: 0769752665 au 0786688200Huduma zetu zinamfikia Mteja popote alipo bila shda yoyote, nyote mnakaribishwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpendwa msomaji wetu, yawezekana umekuwa ukiwaza sana nini ufanye ili uweze kufanikiwa na kuondokana na adha za umaskini. Kulalamika tu vyuma vimekaza haitakusaidia kitu kama hutaki kujiongeza ili uongeze kipato chako.

Yako mambo mengi ya kufanya ili kujikwamua kiuchumi. Usitegemee mshahara wako tu. Mimi nataka kukufungua macho kwa jambo moja tu tena kwa uchache. Jambo hili anaweza kulifanya mwenye mtaji mkubwa au mdogo.

Somo ni dogo tu lakini naamini wapo watakaopata mafanikio makubwa sana.
Unaweza kuanza kwa mtaji wa Mil.1 mpaka laki tano au hata chini ya hapo.

Mfano. Unaweza kutumia Tsh 250,000 kununua kuku 25 kwa bei ya Tsh 10,000 kwa kuku mmoja (kadirio la juu) Majogoo watakuwa 5 kwa uwiano wa 1:4.

Hii ina maana kuwa wakishaanza kutaga utakuwa na vifaranga 20 x 10 = 200 Watunze vizuri. Wale vifaranga tunakadiria kuwa majike watakuwa 150 ambao ndani ya miezi 3 au zaidi nao wataanza kutaga.

Utakuwa na kuku 200 + 25( ulioanza nao) =225 ndani ya miezi 6. Miezi 6 inayofuata 225 - (majogoo 55) = 170 Hii ina maana kuwa 170 x 10= 1,700.

Ndugu msomaji, hayo niliyotoa ni makadirio ya chini sana hivyo mpaka mwisho wa mwaka utakuwa na kuku zaidi ya 2000.

Mwaka utakaofuata utakuwa na kuku wangapi baada ya kuuza kuku baadhi ili upate fedha ya kuwalisha ????

Ukiuza kuku 1000, utabaki na kuku 1000, kati yao tuseme majike ni 750. Ndani ya Miaka 2 maanake ni 750(majike) x 10 = kuku 7500 (uza wengine upate pesa ya kutumia kuwalisha) .

Tuseme sasa utabakiwa na kuku jike 3000 x 10( jike moja ni mayai 10) = kuku 30,000.

Hao kuku 30,000 ukiwauza wote utapata; 30,000x 13000( bei ya kawaida kbsa)= 390,000,000. Je, bado utakuwa masikini? Bado vyuma vitakuwa vimekaza?

Nina uhakika, mpaka mwisho wa mwaka huo wa pili utakuwa umefanikiwa sana kuukimbia UMASIKINI.

Kwenye hayo mamilioni, hata ukitoa milioni 100 kwamba tuseme ndo zimetuka kuendeshea mradi wako, bado utakuwa ni milionea tu. Kumbuka huu ni mwongozo tu, fanya utafiti na ufuatilie zaidi.

NB: Ukiyapata hayo mamilioni ya pesa, kumbuka kutoa Zaka, sadaka na kusaidia masikini wasiojiweza ili ubarikiwe zaidi
 
Kama kuna concept wajasiriamali wengi wana overate ni hii hapa, hayo mahesabu yanavutia kuangalia lkn ukiingia kwenye practice utaambulia hasra moja takatifu.
From experience kuna vitu kma magonjwa, chakula, security na mengine. Nilijidanganya Just like mtoa mada, i lost pesa nyingi sana mainly because hatuna experts wa kutosha linapokuja kwa kuku wa kienyeji. Inshort never buy the dogma


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom