Nimeanza safari yangu ya ufugaji wa kuku wa kienyeji Rasmi kwa Mwaka 2019,Nahitaji ushauri wenu.

  • Thread starter Mkulima na Mfugaji
  • Start date
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
115
Points
225
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined Apr 10, 2011
115 225
Hivi inakuwaje kuku analalia mayai 10 mwisho vinatoka vifaranga v2 shida iko wapi
Shida yaweza kuwa kwenye mayai, kuku anayeatamia au mazingira yanayomzunguka kuku anayeatamia (management yako mfugaji).

Mayai sharti yawe bora. Yawe yamerutubishwa vema na jogoo. Hapo ratio sahihi ya tetea/jogoo ndiyo suluhisho. Tetea 10 wawe na jogoo 1.

Pia mayai yasikae muda mrefu. Mwisho siku 14 tangu yatagwe. Mayai yasiwe na nyufa, mawimbi, umbo dogo au kubwa sana, na pia yasiwe na unyevu/uchafu.

Kuna kuku si waatamiaji wazuri. Hatulii kwenye kiota. Huyo lazima aharibu mayai.

Kuhusu mazingira, hakikisha kuku anayelalia ametengwa peke yake asisumbuliwe na kuku wengine. Pia maji na chakula viwe jirani na vitosheleze. Avipate on demand! Acha kumsumbua sumbua ikiwa unafanya hivyo.

Kazi kwako.
 
King mkucha

King mkucha

Member
Joined
Oct 14, 2016
Messages
47
Points
125
King mkucha

King mkucha

Member
Joined Oct 14, 2016
47 125
Kaka kuku kuchi huwa sio wazuri sana kama utahitaji kufuga kwa biashara labda ujifurahishe tu... maana huwa sio watagaji na majogoo wake hupenda kuendekeza ngumi hadi wanajisahau kupanda na uzito wao huwa unachangia....
Hata Mie nimeanza kufuga kwa kuku kuchi 2 na dume lake 1 sasa Nina vifaranga vya kuku kuchi 13 vya mwezi 1 matarajio yangu hadi mwezi wa sita mtakua nao wengi kwa kuuza biashara
 
King mkucha

King mkucha

Member
Joined
Oct 14, 2016
Messages
47
Points
125
King mkucha

King mkucha

Member
Joined Oct 14, 2016
47 125
Nunua vifaranga hao wakubwa utapata hasara sana
Kuna binadamu hawana huruma kabisaa mwaka 2017 mwisho december nilinunua kuku kutoka mbeya jumla majike na majogoo kama 70 ila mpaka hivi hela hawajaongeza kabisaa zaidi naona wamebakia 30 kila siku mfanyakazi anasema wanaumwa na kufaaaaa
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
19,731
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
19,731 2,000
Msaada Wandugu... Kuku wanaokula mayai, dawa Yao NI nini ili waache..??
 
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2014
Messages
1,591
Points
2,000
Escrowseal1

Escrowseal1

JF-Expert Member
Joined Dec 17, 2014
1,591 2,000
Mkuu niruhusu tuwasiliane DM tubadirishane mawazo kwa kuwa na mimi niko kwenye maandalizi ya kufuga
 
BenKaile

BenKaile

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2014
Messages
307
Points
250
BenKaile

BenKaile

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2014
307 250
Baada ya safari ya muda mrefu wa kujibana matumizi nimefanikiwa kujenga baada pembezoni mwa nyumba yetu lenye eneo kubwa la uzio wa matofali. Nimeanza kwa kununua kuku wa kienyeji wadogo wa miezi miwili na mitatu 100 nategemea kuwa na majogoo 20 na wanaotaga 70. Malengo niliojiwekea ni kuku 50 watage kwa awamu mbili kwa mwaka huu. Kila kuku awe na vifaranga 6 kwa awamu moja, hivyo kwa awamu mbili kila kuku nategemea awe na watoto 12 nikizidisha na kuku 50 napata kuku 60 ambayo nitauza kwa Tsh 6000 kwani sitangoja wawe wakubwa sana. Hivyo kwa mwaka huu natarajia kukusanya Tsh 3000000. Soko langu limelenga sikukuu mbili kubwa. Yaani Eid na Christmas. Mungu nisaidie nifanikiwe malengo yangu. Naombeni ushauri, maoni na pia nikosolewe kama ninakosea.

Pia hela ya kununulia chakula na dawa nimeshaandaa angalau kila mwezi laki moja kwani ni kuku wa kienyeji ambao wanakula pumba tu.

Niko Muheza Tanga

Sent using Jamii Forums mobile app
MWENYEZI MUNGU AIBARIKI KAZI YA MIKONO YAKO, NDUGU YANGU. HEKO!!
 
Sanchez magoli

Sanchez magoli

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2015
Messages
2,688
Points
2,000
Sanchez magoli

Sanchez magoli

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2015
2,688 2,000
Wakate midomo ile ya juu iliochongoka Nenda maduka yanayouza madawa ya wanyama wanauza hiyo mikasi yake
Tokana na adhaa hizi kuna haja ya kuwa na muhudumu wa karibu
 
U

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2017
Messages
279
Points
250
U

UMUNYU

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2017
279 250
Baada ya safari ya muda mrefu wa kujibana matumizi nimefanikiwa kujenga baada pembezoni mwa nyumba yetu lenye eneo kubwa la uzio wa matofali. Nimeanza kwa kununua kuku wa kienyeji wadogo wa miezi miwili na mitatu 100 nategemea kuwa na majogoo 20 na wanaotaga 70. Malengo niliojiwekea ni kuku 50 watage kwa awamu mbili kwa mwaka huu. Kila kuku awe na vifaranga 6 kwa awamu moja, hivyo kwa awamu mbili kila kuku nategemea awe na watoto 12 nikizidisha na kuku 50 napata kuku 60 ambayo nitauza kwa Tsh 6000 kwani sitangoja wawe wakubwa sana. Hivyo kwa mwaka huu natarajia kukusanya Tsh 3000000. Soko langu limelenga sikukuu mbili kubwa. Yaani Eid na Christmas. Mungu nisaidie nifanikiwe malengo yangu. Naombeni ushauri, maoni na pia nikosolewe kama ninakosea.

Pia hela ya kununulia chakula na dawa nimeshaandaa angalau kila mwezi laki moja kwani ni kuku wa kienyeji ambao wanakula pumba tu.

Niko Muheza Tanga

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera kwa wazo zuri
 
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
115
Points
225
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined Apr 10, 2011
115 225
Msaada Wandugu... Kuku wanaokula mayai, dawa Yao NI nini ili waache..??
Pia tatua tatizo la msingi. Kuna virutubisho wanakosa kwenye chakula unachowapa. Madini &/ protein. Rekebisha chakula. Usipofanya hivyo hawaachi hata uwakate vipi.
 
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2009
Messages
19,731
Points
2,000
Ngalikihinja

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2009
19,731 2,000
Pia tatua tatizo la msingi. Kuna virutubisho wanakosa kwenye chakula unachowapa. Madini &/ protein. Rekebisha chakula. Usipofanya hivyo hawaachi hata uwakate vipi.
Asante kiongozi, unaweza nitajia aina ya vyakula inayoweza ondoa shida hiyo?
 
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
115
Points
225
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined Apr 10, 2011
115 225
Asante kiongozi, unaweza nitajia aina ya vyakula inayoweza ondoa shida hiyo?
Vyanzo vizuri zaidi vya madini ni mifupa na chokaa chokaa. Vyote hivi vinapatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Pia waweza tumia DCP au Premix.

Chanzo kizuri zaidi cha protein ni soya. Ila kumbuka protein yoyote itokanayo na mimea hukosa elementi mbili za Lysine na Methionine. Hivyo utalazimika kutumia premix yenye hivyo viwili ndani yake.

Hakikisha pia chakula chako kinawekwa virutubisho kwa uwiano sahihi. Mfano, protein yapaswa kuwa 16% - 22% ya chakula chote. Angalia kwenye desa la uandaaji chakula cha kuku lifuatalo.
 
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
115
Points
225
EZZ CHEZZ

EZZ CHEZZ

Senior Member
Joined Apr 10, 2011
115 225
Vyanzo vizuri zaidi vya madini ni mifupa na chokaa chokaa. Vyote hivi vinapatikana kwenye maduka ya vyakula vya mifugo. Pia waweza tumia DCP au Premix.

Chanzo kizuri zaidi cha protein ni soya. Ila kumbuka protein yoyote itokanayo na mimea hukosa elementi mbili za Lysine na Methionine. Hivyo utalazimika kutumia premix yenye hivyo viwili ndani yake.

Hakikisha pia chakula chako kinawekwa virutubisho kwa uwiano sahihi. Mfano, protein yapaswa kuwa 16% - 22% ya chakula chote. Angalia kwenye desa la uandaaji chakula cha kuku lifuatalo.
Nimeshindwa kuki-attach. Ingia google download kitabu cha UTENGENEZAJI CHAKULA CHA KUKU cha LRDC
 
kalagabaho

kalagabaho

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
4,838
Points
2,000
kalagabaho

kalagabaho

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
4,838 2,000
Safi sana, mimi nimeanza kufuga kuku 6, jogoo mmoja mitetea 5, sasa hivi wote wanataga nnatarajia mda siyo mrefu nitakuwa na vifaranga siyo chini ya 60, ambao nitawachukua kutoka kwa mama yao, baada ya hapo kazi yangu itakuwa kula mayai na nyama wakipungua nazalisha wengine, sifanyi kwa ajili ya biashara, ila nimegundua kufuga wanyama/ndege inakufanya uwe active sana, furaha na stress vyote vyako, kuna kuku mmoja namkubali sana sana sijui kama nitakuja kumla kwa kweli, actually hawa kuku wote nilioanza nao sitawala
Kweli kiongozi kufuga ni raha na sometimes karaha ..Mi nina kuku wangu mmoja namkubali sana mwenyewe namuitaga straika huyu akiniona ananikimbilia na kisha anaruka ruka kama vile anataka kupiga story na mimi.. dah huyu siwezi kumchinja.. kuna mwingine bwege kweli akiniona ananidonoa bila sababu na kukimbia halafu hatagi sana hata akitaga anataga viyai vidogoo huyu hana siku nyingi za kuishi .. ila kiujumla na enjoy sana kufuga hasa ktk zama hizi ambazo binadamu ni wanafiki na wambea ni bora kutumia muda wako kucheza na kuku tu
 
Forum statistics

Threads 1,315,050
Members 505,131
Posts 31,846,482
Top