Nimeanza na kudeposit 100,000, nataka ninunue gari

Kujichanga kwa 10 years afu uje ufanikiwe unaingia tuh barabarani unakutana na dereva machachari wa boda boda au daladala anasababisha uipeleke gar gereji tena ..tabu yote ya nn we nunua gar ukiwa na hela maana kupata gari wanasema ni rahis ila matunzo ndio tabu
 
Leo nimeweka laki moja kwene acc maarumu kwa ajili ya kununua gari

Gari ninayoitaka ni Rav4 new model black

Bei zake nimechek cheki kwenye mitandao ni milion 23-24

Sijui itabichukua muda gani kufikia lakini nimeona bora nianze kujichanga naipenda sana hiyo gar!

Ebu mnishauri mliofanikiwa kununua gar yeyote kwa kujichanga kidogo kidogo AU KAMA KUNA NJIA NYINGINE NZURI YA KUTIMIZA MALENGO JISHAURINI
Hiyo laki (100000/=) una isave kwa siku, kwa wiki au kwa mwezi? Jibu la hili swali ndio utakuwa msingi wa ushauri wangu. Nasubiri.
 
Sio kwangu tu, imagination inafanya kazi kwa mtu yeyote.
Kupitia imagination unaweza kupata sio gari tu chochote kile.

in a battle between imagination vs will power
Imagination always win
Imagination aka image +formation.
 
Tafuta namna upate mkopo,au hiyo laki ingia namna uanze kucheza mchezo na wenzio,then uchukue pesa kubwa, au jiunge na saccoss zipo nyingi unWeza kopa hata maratatu ya pesa yako. Achana na wanaosema kukopa ili kununua gari ni big mistake.Wengi tuna magari ya mikopo
Kopa ununue gari la biashara,liingize fedha,lilipe mikopo lenyewe,usikope kununua gari ya kutembelea tu labda uwe na vyanzo stable vya upataji fedha
 
Tatizo watu wanaanza tu na kukukatisha tamaa. Hao ndio watu hawajui uwezo wa mtoa mada, pengine anauwezo wa kuweka laki kila siku,lakini wamekimbilia kwamba haiwezekani. Mkuu inawezekana hata ikikuchukua miaka kumi,ujue tu inawezekana,we focus tu.
 
Imarisha /ongeza vyanzo vyako vyaapato zaidi , ili uweze kisave pesa nyinhi zaido.. na malenho yako yatimie haraka!!
 
Back
Top Bottom