RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 51,719
- 107,833
Mwaka huu nimejiwekea lengo la kuwa FIT. Nimeanza mwaka kwa mazoezi sasa hivi namaliza mwezi najisikia vizuri sana. Mazoezi sio lazima uende Gym. Hata chumbani au nje ya nyumba yako unaweza kufanya mazoezi.
Kama mimi asubuhi(siku tano kwa wiki) nakimbia(jogging) kwa muda wa nusu saa kila siku kuzunguka eneo dogo tu nje ya nyumba. Jioni napiga push ups 300 siku tano kwa wiki. Hizi push ups napiga 30 mkupuo mmoja, zoezi zima huwa linachukua nusu saa.
Jogging inasaidia kuimarisha misuli ya miguu na kuimarisha moyo wakati push ups zinanisaidia kuimarisha misuli ya mikono na kiwiliwili kwa jumla. Huna haja ya kubeba machuma ili uwe fit. Jogging,sit ups,push ups zinatosha kukufanya uwe fit.