Nimeanza kuogea Omo baada ya harufu mbaya kwenye korodani kukataa kutoka mwilini mwangu

Paramagamba

Member
May 12, 2017
85
129
Wadau mwenye kujua madhara endapo nitaogea sabuni ya Omo hasa katika korodani anijuze.

Korodani zangu zinatoa sana harufu nimeanza kuogea Omo baada ya sabuni nyingine zote kudunda kuanzia detol, protex na kadhalika.

Korodani langu linatoa sana harufu huu ni mwaka wa 18 harufu haitaki kutoka. Mwanzo nilidhani labda ni fangus ambazo ni chronic lakini hakuna cha fangus wala nini nimepaka sana cream za fangus na kumeza dawa zake moja inaitwa zocon lakini hakuna kitu sio fangus bana.

Shuleni nilikuwa na tabia ya kuvaa chupi hata kama haijakauka vizuri kambani inakuja kukaukia mwilini. Ninahisi hicho ndiyo chanzo cha haya mateso yote. Nikikaa karibu na mtu hata kwa dakika mbili anaugua mafua pale pale na kupiga chafya za kutosha. Kabla sijanunua gari nilitesa watu wengi sana kwenye hizi daladala. Kila mtu alikuwa anahama siti yangu endapo atapata fursa ya kuhamia kwenye siti ya abiria mwingine aliyeshuka kwenye daladala. Hili ni janga ndugu zangu.

Kazini kuna AC za kutosha na huwa ninavaa boksa za pamba 100% lakini hakuna kitu. Korodani zangu hazina majira ya kiangazi, vuli, kipupwe wala masika iwe joto iwe baridi harufu ipo pale pale. Naogopa kukutana na watu. Ningekuwa nimeisha oa mpaka sasa lakini baada ya muda wanakimbiaga ninahisi labda ni sababu hii.

Ninakwenda kukata tamaa kwa sababu nikienda mahospitalini huwa naonana na madaktari bingwa wa ngozi wanaitwa dematologists hawaoni fangus wala nini wanasema nina matatizo ya kisaikolojia. Mbaya zaidi kuna ambao wanasema ninanuka kweli na wengine wanasema sinuki lakini baada tu ya kuwaambia tatizo. Ubongo wa mwanadamu ni tanuru la giza. Mtu nimekutana naye hana hata mafua baada ya kukaa naye dakika mbili automatically anaanza kupiga chafya za kutosha mpaka kamasi zinamtoka anaziba na pua kabisa bila kujua chanzo ni mimi lakini baada ya kumwambia tu hali yangu basi ubongo wake ghafla unaziba mlango wa fahamu wa kunusa harufu anasema sina harufu na mafua pale pale yanapona na chafya zinakoma.

Mpenzi wangu aliwahi kuniambia ninanuka. Mama yangu aliwahi kuniambia nina nuka. Rafiki zangu wa karibu sana ambao tupo nao kila siku ofisi moja ni kama wamezowea harufu yangu imekuwa sehemu ya maisha yao kwa miaka sasa kwa hiyo pua zao ni kama zimeisha jeruhiwa kwa harufu yangu kwa hiyo ni sawa tuvlabda siku izidi sana ndiyo unaona wanateseka lakini kwa wafanyakazi wengine nilishawabamba wananiteta kuhusiana na harufu yangu.

Wengine walishauri nisuuze kwa maji ya ugali, wengine tumia mafuta ya nazi, vyote nimejaribu harufu iko pale pale. Jana kwa mara kwanza nimepata wazo la kuogea sabuni ya Omo ila cha moto nimekiona.

Naombeni msaada ndugu zangu.
 
Hivi nitajie mwanamume yule ambaye Korod** zake hazinuki!!!, kwani wewe zako zina nukaje??-- kama kitu kilichooza au ???--

Halafu kumbuka humu kuna jinsia ya KE pia.
 
Duuu, polee mzee...
Inaonesha hali si nzuri, Nahisi ni fungus,

Huna PE? Ukiwa maeneo ya joto sana Epuka kusunda nguo nyingi Na za kubana huko chini kibiti....,
Jitahidi kuoga, Mafuta haina ulazima wa kupaka,
Vaa boksa za Cotton, Ukilala ziache zipunge upepo, Zioshe kwa maji baridi, Unaweza nyunyizia Powder, Ukiwa katika mazingira Binafsi au Yasio na taharuki/vishawishi/watu wengi hasa KE, vaa nguo za ku relax, Kama track hivi...
Ukishajizoesha, na mwili uka adapt, basi itafika hatua mwili utazoea na hutatumia nguvu sana kupambana na hio harufu..,

Katika hali ya kawaida korodani hutoa harufu usipooga, siku nzima katika mazingira ya joto kali, Na sio ghafla tuu, mwanzo utaisikia mwenyewe labda baada ya hapo uzidishe,
Kwenye mazingira ya Baridi hata week hazitoi harufu kiasi hicho.
 
PE unamaanisha nini?
 
Pole sana kwa unayopitia hayo.Hili swala watu wengi wanalichukulia rahisi lakini kiukweli ni mateso makubwa mno.Mimi pia ni mhanga wa jambo kama lako kwa miaka 14 sasa kitu ambacho kimeniharibia utu na maisha yangu kwa ujumla.Naishi kama mnyama asiweza kujiswafi licha ya hali ya usafi ninayo kuwa nayo mda wote.

Hali hii kwangu ilianza october 2006 wakati nipo form one kuna siku tu nikahisi kiharufu kizito na chepesi kinatokea sehemu zangu za siri,lakini jioni nilipojiangalia maeneo sikuona tofauti yoyote nikajua labda ni mambo ya usafi tu kumbe nisijue ndio ukawa mwisho wa maisha ya furaha kwangu kama mwanume kamili.

Baadae form two hali ilizidi kuwa mbaya hususani baada ya saa nne(hali ilikuwa inachachamaa sana ukitoka juani kiasi cha ku paralyse pua zangu huku wenzangu wakikiona cha mtema kuni kwani harufu inakuwa ni nzito sana na wakati mwingine ni kama ile ya kiatu kinachonuka).NImeenda ma hospitali naambiwa sina fangasi yoyote lakini msoto bado upo pale pale.Maombi,waganga,limao,ma ukoko ya ugali,baking powder,mafuta ya nazi vyote ni vimedunda.

Yaani kwa hali niliyopo sasa siwezi hata kurudia suruali kwa siku mbili,Yaani nateseka sana na hii hali alafu pumbu huwa zinachemka sana huku harufu nzito ikitoka huko.Yaani nikiwa na safari nisipopata siti ya dirishani basi jirani ana hali mbaya safari nzima.
NILISHALETAGA UZI HAPA JAMII FORUM JAPO MODS WALIBADILISHA HEADING TOFAUTI NA MALENGO YANGU MAAANA ILIKUWA KU CAPTURE ATTENTION YA WACHANGIAJI WENGI.
Nimekata tamaa na maisha yangu kwa hali hii.Zaidi soma hapa chini.
Msaada: Natokwa na harufu mbaya sana sehemu za siri
 
Wadau mwenye kujua madhara endapo nitaogea sabuni ya Omo hasa katika korodani anijuze.

Korodani zangu zinatoa sana harufu nimeanza kuogea Omo baada ya sabuni nyingine zote kudunda kuanzia detol, protex na kadhalika.

Korodani langu linatoa sana harufu huu ni mwaka wa 18 harufu haitaki kutoka. Mwanzo nilidhani labda ni fangus ambazo ni chronic lakini hakuna cha fangus wala nini nimepaka sana cream za fangus na kumeza dawa zake moja inaitwa zocon lakini hakuna kitu sio fangus bana..
Sikiliza ndugu. Nenda dukani, nunua deodorants za kupulizia au za kurole mfano; nivea for men, dove men care, men mitchup na nyinginezo. Kila ukimaliza kuoga asubuhi weka sehemu husika. Hii si tiba ila inakulinda dhidi ya harufu hiyo kwa masaa 24 mpaka 48. Fanya hivyo mkuu utanipa mrejesho. Ila jipange vina gharama kidogo. Ni kaunzia tshs 5000 na kuendelea. Unatumia maisha yako yote kama hupendi harufu. Wanaozitumia kutibu kikwapa wataongezea hapa.
 
Ndugu yangu hayo madeodorant ndiyo usiseme ni kama ndiyo yanachochea sasa harufu kuongezeka. Nimeyatumia kwa miaka mingi hola. Pia yanaharibu sana ngozi ya korodani.
 
Sasa hiyo Ommo haikuunguzi mkuu? na je unaona tofauti ya harufu kupungua baada ya kuanza kuitumia?

Pole sana
Kwa kweli inaunguza sana. Leo nitajaribu nione tena. Nikishatumia omo huwa nakaa kwenye beseni kutuliza maumivu ya kuunguzwa. Omo ni kali sana unaweza sema unakatwa na wembe.
 
Fuata huu ushauri Anza kutumia mafuta ya Nazi kujipaka asubhi na usiku ukitaka kulala. Paka sehemu za Siri kote halafu ulete feedback hapa.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom