Nimeamua, sitapiga kura tena!

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,737
5,438
Mimi ni muumini wa vyama vingi ingawa ni mpiga kura huria na sio mwanachama wa chama chochote cha siasa.

Kwa mara ya kwanza nilipiga kura mwaka 1990, tena nikiwa mwanafunzi wa sekondari. Wakati ule nil8mpigia kura Mzee Mwinyi na ulikuwa mfumo wa chama kimoja tu -CCM. Tangu mwaka 1990 hadi leo hii, nimepiga kura katika chaguzi zote kuu bila kuacha. Kwa bahati sijawahi kushiriki kupiga kura kwenye chaguzi ndogo zozote.

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa siasa, iwe hapa nyumbani Tanzania au siasa za kikanda na kimataifa kwa ujumla.

Tangu baada ya uchaguzi wa 2015 ambao ulikuwa na msisimko wa kipekee hadi sasa, nchi yetu imeingia hatua nyingine ya kidemokrasia. Kumekuwa na mbinyo na ukandamizaji wa haki za kidemokrasia kuliko ilivyokuwa 1995-2015.

Kuna mazuri ambayo utawala wa Rais JPM umeyafanya, kupambana na rushwa na ufisadi na kurudisha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma. Hata hivyo Kumekuwa na uminyaji wa haki za kisiasa na kidemokrasia kinyume cha matarajio yangu kuwa demokrasia yetu changa ingesitawi zaidi.

Tumeshuhudia vyombo vya dola vikitumika kukandamiza wapinzani wa CCM na kutovumilia mawazo mbadala. Tumeshudia Tume ya Uchaguzi ikishindwa kutimiza wajibu wake na kwa makusudi ikichangia kuvurugika kwa uchaguzi kama hivi juzi kule Kinondoni na kupelekea kuuwawa kwa mwanafunzi asiyehusika na vurugu za uchaguzi Akwilina Akwiline na kujeruhiwa na risasi kwa wafuasi kadhaa wa Chadema.

Ktk chaguzi hizi ndogo kumekuwa na hamasa sana kwenye kampeni, lkn la kushangaza wapigakura wanaojitokeza ni wachache pengine kuliko wakati wowote kwenye chaguzi! Hili halijawashitua wachambuzi wa mambo ya siasa, Tume ya Uchaguzi wala Serikali. Ktk uchaguzi wenye ushindani wa kweli wa kidemokrasia, mafanikio hupimwa kwa msisimko wa kampeni, ushindani Ktk uchaguzi, na idadi ya wapigakura. Tunachokiona kwenye kampeni ni tofauti kabisa na kinachoonekana kwenye matokeo na hivyo kuleta maswali mengi kuliko majibu.

Sasa, mimi Vyamavingi, kuanzia leo natangaza rasmi kutoshiriki uchaguzi wowote hadi hapo nitakapojiridhisha kuwa vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi, Polisi, na Serikali kwa ujumla vinaweka mazingira yenye kutoa fursa ya uchaguzi wenye kutoa ushindani sawa na wa haki kwa wadau wote wa uchaguzi.

Vv
 
nahisi nami naelekea huko! haina maana kupiga kura kwanye nchi ya demokrasia isiyo na democracy
 
nahisi nami naelekea huko! haina maana kupiga kura kwanye nchi ya demokrasia isiyo na democracy
Mkuu, sioni thamani ya kura yangu, naona nguvu yangu ya maamuzi kuhusu nani awe kiongozi wangu haipo tena.

Vv
 
Ambacho hutaki kukifanya tena ndicho kinachotafutwa usiku na mchana kwa gharama kubwa sana na chama kikuu, kwahiyo utakuwa umewarahisishia kabisa shughuli ya ya uporaji wa "kula".
 
CCM hawahitaji kura ya mtu kushinda bora wafute tu uchaguzi tujue moja tu, uchaguzi kama tulivyoona juzi juzi ni, kupoteza muda na rasilimali bure tu wakati mshindi walishampanga
 
Hata tukikataa kupiga kura mambo yatakuwa yaleyale cha msingi tunatakiwa tudai katiba mpya.
Binafsi naiunga 26/04/2018 kwa vitendo na si kulialia mitandaoni
 
Upige usipige ni haki yako ya kidemokrasia hongera kwa uamuzi wako
Asante mkuu, nimeona siwezi kupoteza muda na kuhatarisha maisha yangu bure kwa chaguzi za chaguzi zetu, yasije kunikuta kama ya binti Akwilina, Daniel na wengineo.

Vv
 
Ambacho hutaki kukifanya tena ndicho kinachotafutwa usiku na mchana kwa gharama kubwa sana na chama kikuu, kwahiyo utakuwa umewarahisishia kabisa shughuli ya ya uporaji wa "kula".
As long macho yangu hayataki kushudia viini macho vya demkrasia na upotevu wa maisha ya watu, acha iwe hivyo.

Vv
 
Me toka 2010....sijawai na sitowai tena kupiga kura.....siku hiyo ya uchaguzi ntanunua maji yangu ya uhai karibu gari zima niweke pembeni nipige ela.....
 
Mimi na familia yangu hatutapiga... Bora siku hiyo tukae tulewage ulanzi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom