Nimeamua kuwa wazi, siogopi polisi wala CCM na serikali yake

Hakuna cha Slaa wala Mbowe, wao wenyewe ni waoga, au umesahau lile tukio la Arusha. Mbowe na umri wake wote aliweza kuruka ukuta

Hahaha Kama ni kweli basi tuna longway to go na sio 2015 Kama ninavoamini. Swali kwanini polisi hawawaui wao wala kuwafunga? Ina maana kesi zote hizo Kama wanamakosa mbona hawafungwi? Ushauri Kama CDM hawawezi kuitisha maandamano basi waache kazi zao mpaka Iyo 2015-25-35-45 au 2055 ili kupunguza mauaji Haya. Naamini ni uoga na sio busara Kama wanavyotuaminisha.

By JIULIZE KWANZA
Kwi Kwi Kwi Labda aseme slaa au Mbowe ndio ataeleweka wewe unknown user utasubiria sana japo wapo wenye nia ya kukuunga mkono lakini Wana angalia bob we lianzishe ukipata watu 1000 basi Mimi nitachukua namba 1001
 
Acheni kujidanganya nyie, humu wote waoga... Eti muanzishe mapambano!.. Kama kuona utumbo wa David tu hapa mmeanza kuweweseka, mtaweza kuvumilia mabomu ya machozi?

kumbe kipuri chakavu.........looh!
 
SANGAKA,

Kama hujatumwa basi pole kwa hasira uliyonayo.

Ninakushauri tu kwanza ukalale ili uipumzishe akili yako na ukiamuka utakuwa na mawazo mazuri ya kupimika.
 
Haya maneno ndio yale wanayo toa kina Slaa halafu wao wanasepa wengine wanauawa. Watu tuache kuishi na familia zetu tukufate wewe kwenda kufanya fujo ili Slaa awe rais, hivi unajua balaa la uhaini wewe? Rudi kwa wakuu wako uwaambie kuwa huku JF wamekustukia.
Majebere mimi sijazungumzia habari za slaa kuwa rais.Natambua kuwa kama wanajf wazalendo kila mtu ana wajibu wakuifanyia kitu chema nchi yake.Dr slaa ana namna yake aliyochagua kulitumikia taifa.Beside,nafahamu ni nani nabishana nae hivyo hainipi taabu saana.Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida sana.
 
acha kupotosha, hatuja fika hatua hiyo tz ya wananchi kuingia barabarani.
Kelele tunazopiga kupitia vyombo vya habari zinatosha, huku kuifanyia fujo serekali ni kukurupuka.
Waungwana wanazungumza, na wazungumzao hawagombani.
Tuache kukuza mambo na tutumie busara badala ya jazba.
Suala la ulimboka mwenyewe kakaa kimya, unataka tufanyeje?
Yeye ndo angetoa ushahidi wa nini kilichotokea lkn hajataka.
Suala la muandishi iringa kila mmoja anajua lilivyo iyumbisha serekali ndio mana unaona wanalifanyia kazi.
Kelele zetu kupitia media zinatosha, hakuna sababu ya kufanya fujo.
Au ndio unataka nchi isitawalike?
 
SANGAKA,

Kama hujatumwa basi pole kwa hasira uliyonayo.

Ninakushauri tu kwanza ukalale ili uipumzishe akili yako na ukiamuka utakuwa na mawazo mazuri ya kupimika.
Nakushukuru sana kwa ushauri wako,lakini yawezekana huna hisia juu ya mauaji haya ya watu wasiokuwa na hatia,kama hivi ndivyo,ni vigumu mitazamo yetu ika-match.
 
Majebere mimi sijazungumzia habari za slaa kuwa rais.Natambua kuwa kama wanajf wazalendo kila mtu ana wajibu wakuifanyia kitu chema nchi yake.Dr slaa ana namna yake aliyochagua kulitumikia taifa.Beside,nafahamu ni nani nabishana nae hivyo hainipi taabu saana.Kutofautiana kimtazamo ni jambo la kawaida sana.
Fujo ni kitu chema? Kuhamasisha uhaini ni uzalendo? Haya tuiotoe hii serikali halafu wewe ndio uwe kiongozi?
 
acha kupotosha, hatuja fika hatua hiyo tz ya wananchi kuingia barabarani.
Kelele tunazopiga kupitia vyombo vya habari zinatosha, huku kuifanyia fujo serekali ni kukurupuka.
Waungwana wanazungumza, na wazungumzao hawagombani.
Tuache kukuza mambo na tutumie busara badala ya jazba.
Suala la ulimboka mwenyewe kakaa kimya, unataka tufanyeje?
Yeye ndo angetoa ushahidi wa nini kilichotokea lkn hajataka.
Suala la muandishi iringa kila mmoja anajua lilivyo iyumbisha serekali ndio mana unaona wanalifanyia kazi.
Kelele zetu kupitia media zinatosha, hakuna sababu ya kufanya fujo.
Au ndio unataka nchi isitawalike?
Kwani sasa ndugu yangu Peri nchi inatawalika?
 
Tafuta njia nyingine hii hutapata mtu haswa waTZ unaacha maswali kuliko majibu
 
Nakushukuru sana kwa ushauri wako,lakini yawezekana huna hisia juu ya mauaji haya ya watu wasiokuwa na hatia,kama hivi ndivyo,ni vigumu mitazamo yetu ika-match.

Hakuna anaefurahia kifo wala hakuna anaependa mwenzake apate matatizo'lakini haya ya kwetu yanaeleweka chanzo ni kitu gani' waambie viongozi wa cdm waheshimu mamlaka za nchi waone kama nchi haitatawalika
 
Tafuta njia nyingine hii hutapata mtu haswa waTZ unaacha maswali kuliko majibu
Mvumbuzi kaka/dada sijakuelewa vizuri,iwapo hutaniunga mkono si mbaya,kwani nimeendea kuishi hadi leo hii nina miaka 30 bila ya uungwaji mkono kutoka kwako,lakini kama wewe ni gamba siku zako zinahesabika,"sure am telling u"
 
Mh...inaonekana umechoka sana lakini mbona na wewe umejificha nyuma ya keyboard na jina lako lisilo halisi?
 
Hakuna anaefurahia kifo wala hakuna anaependa mwenzake apate matatizo'lakini haya ya kwetu yanaeleweka chanzo ni kitu gani' waambie viongozi wa cdm waheshimu mamlaka za nchi waone kama nchi haitatawalika
Kwani kazi ya mamlaka ya nchi yetu kwa sasa ni kuzuia maandamano na mikutano ya cdm?
 
kuna siku niliandika humu nikiomba wanjf tuungane kupinga huu udhalimu na hata ikibidi tuunde chama cha ukombozi,waliojibu kwa ustaarabu walikuwepo,kama kawaida sikukosa waliotumia viuno kufikiri,lakini mwisho bwana mmoja akasema haiwezekani tukaungana huku tukishuhudia tofauti za kiitikadi ndani ya wanajf wenyewe.partly nakubaliana nae.

Misri walitumia hii mitandao ya kijamii kufanya mapinduzi makubwa yaliyobadilisha mfumo wa kidikteta na walau wakashuhudia hatua muhimu ya kuelekea katika demokrasia kwa kufanya uchaguzi,tunisia nao vivyo hivyo. Nasema wanajf ni watanzania halisi kwani miongoni mwa sifa ya mtz halisi ni kulalamika tu bila kuchukua hatua.

Nchi ikifika hapa basi mungu amjalie kikwete aendelee kupata amani katika uongozi wake.kwa mara nyingine wanajf naomba tutumie mitandao hii hasa kwa wale tuliopata bahati walau ya kubofya,na nadhani kwa kiasi kikubwa uoga si mkubwa sana.matukio ya hivi karibuni(yaani ulimboka,ally zona na david)yanatosha,tusisubiri tukio jingine ili sisi tuendelee ku-comment.

Hivi kweli hii ndo kazi tuliyoichagua,tukatae,tuingie barabarani tupinge mambo haya.aliye tayari kuninga mkono nami niko tayari kutoa namba zangu za simu.hatuwezi kuendelea kuivumilia hii serikali dhalimu,isiyokuwa na tofauti kabisa na serikali zilizo wazi kuwa ni za kidikteta.nitawapa namba zangu ifikapo saa nane na dakika tano mchana ili ikiwezekana tupange pakukutaniaili nasisi tuweze kuona tutafanya nini juu ya mauaji na dhuluma zinazoendelea.

Tahadhali:pandikizi asijidanganye kufika,najua hii ni hatari sana mimi kujiweka wazi,lakini ni hatari zaidi kwa pandikizi atakaedhani anaweza kunipeleka msitu wa pande
.
Karibuni tuunganishe nguvu

Duuh! kaka umetumwa au wewe chizi? Elimu yako kiwango gani?. wana jf hebu someni vizuri mawazo ya huyu chiizi wetu wa jukwaa halafu changanueni, mtaniamini.
How can so serious issues taken so carelessly and so foolishly like that. Au ndio umeshaa andaa vijana wako wa mabwepande. M$%"£$%^%S^*&&*(&%^&N%(*&%&^% MKUBWA kabisa wewe.
 
SAGANKA, ningelikuwa mie, ningelianza KIMYA KIMYA kama Dereva wa train kwenye vivuko vya barabara.

Huko mbeleni ndiyo unaanza kujenga kundi lako kimya kimya kama ROBIN HOOD.

Haya ya kuja hapa na kujitangaza, ni kuwa umeshashindwa hata kabla hujaanza.

Hapa unakuja ukiwa umevaa SUTI kama walivyo CHADEMA.

Wapigania uhuru hata siku moja hawajitangazi kwenye mitandao. Angalia FARC wa Columbia.

Halafu cha muhimu, uende kusomea UJASUSI na UUWAJI vinginevyo basi uwe na bahati sana.

Ila USOMI wako, utakuwa ndiyo adui yako mkuu kwa hii kesi ya pili. Itasaidia kwenye kesi ya kwanza.
 
Wewe sema siku rasmi ya kuanza mafunzo ya kijeshi na namna ya kutengeneza siraha ili mapambano yaendelee kimya kimya!!
 
Back
Top Bottom