Nimeamua kuwa mpinzani Maisha yangu Yote

Zero Hours

JF-Expert Member
Apr 1, 2011
12,943
18,665
Leo nimeamua niweke wazi kile kilicho Rohoni mwangu. Kupanga ni kuchagua. Lakini kwa moyo wangu wote nimeamua na kuchagua kuwa mpinzani mpaka naingia kaburini.

Naomba niweke sawa kabisa maana kuna wale hawatanielewa vizuri. Ni kwamba mimi sina chama. Chama changu ni Upinzani. Yani hata Cuf au chadema leo iwe ndyo chana tawala mimi nitabaki kuwa mpinzani.

Hii ni kwa uzalendo nilionao wa nchi yangu. Watanzania tusidanganyane kuwa kutakuja tokea chama ambacho kitakuwa ni very perfect kutuletea maendelea ya nchi yetu. Kila serikal inahitaji changamoto na ikosolewe pale inapokosea.

Watanzania kama tunakiu ya maendeleo tusifungamane na chama chochote.



Nawakaribisheni wote kwenye chama cha upinzani. "CCU". "Huku ni makavu live."

Mungu ibariki Tanzania.
 
Tukishang'oa dhulumati ccm hakutakuwa na tatizo hata chembe , hiki chama ni mkosi kwa nchi .

Nakushauri futa andiko lako .
 
Tukishang'oa dhulumati ccm hakutakuwa na tatizo hata chembe , hiki chama ni mkosi kwa nchi .

Nakushauri futa andiko lako .
Mkuu kila chama kina mapungufu yake. Watanzania chagueni mtu na si chama. Natamani sikumoja Tanzania ipate hata serikali ya mseto yani Raisi CCM waziri mkuu upinzani. Wabunge 50/50. Yani hapo kutakuwa na maendeleo ya kasi.
 
Halafu baada ya uchaguzi unalalamika kupokwa uchaguzi.Aliwazalo mjinga ndio linamtokea,wewe Chadema,Cuf mbaki upinzani hadi mauti.
 
Back
Top Bottom