Nimeamua kuvuta bangi ili kutatua matatizo haya

Mchimba Chumvi

JF-Expert Member
May 19, 2016
2,060
4,844
Honestly speaking haya matatizo yananitesa sana nayo ni kutokujiamini, sijikubali, upweke na stress kupitiliza.

Ni kijana wa early 20 nimeajiriwa kampuni fulani ambayo inanibidi ni interact sana na watu hasa raia wa kigeni, but tatizo linakuja kuwa sijiamini kabisa kitu ambacho kimepelekea performance kuwa mbovu kabisa.

Hivyo kupelekekea kuwa na stress, mpweke na sijikubali kabisa

Finally nimepata idea kutoka kwa mshikaji wangu ambaye kanipa idea ya kutumia bangi na anenihakikishia 100% inaenda kutatua kabisa shida zangu.

Najua wapo madaktari na wabobezi wa madhara au faida ya bangi humu naomba mnipatie a,b,c tafadhali.

Natanguliza shukrani
 
We umeamua kuvuta bangi tu huna cha zaidi na kuvuta sio kitu kibaya maana hata Mimi natumia kitu kibaya ni kutaka kuvuta kwa ajili ya confidence je bangi ikienda kinyume na unachokitegemea? cha msingi soma makala zinazoweza kukuongezea confidence au tafuta mbinu nyingine ya kukuongezea confidence ila kama unahitaji kwa ajili ya stimu you're welcome.
 
Mchimba Chumvi,
Kama ni kweli uliyoandika mimi nakushauri hivi. Katu katu usitumie ''ulevi'' wa aina yoyote kufidia udhaifu ulionao. Jambo sahihi la kufanya ni kukubali una tatizo na kuamua kulikabili bila masaada wa ''kilevi''. Bangi inaweza kukuletea negative result ambayo hukutegemea. Na hata ikikuletea matokeo chanya, bado siku moja unaweza kujikuta kwenye mazingira ambayo huipati! Mfano mzuri ni ukisafiri nchi za watu.
 
2018 uliomba msaada wa kazi ukisema usipopata kazi unaweza kua stressed na kutumia madawa ya kulevya,umepata kazi unaanza kulia lia ukisema unataka kuvuta bangi tena.

Vuta tu dogo.
Screenshot_2020-01-14-20-07-44-1.jpeg


dodge
 
Suluhisho la kuto jiamini ni kutafuta zaidi nafasi za kufanya kile unachohisi huwezi. Mazoezi pekee ndio sukuhiso, kuongea katika hadhara inataka uzoefu ambao hata uvute nini hutapata.
 
Back
Top Bottom