Nimeamua kuvunja kisimbuzi cha Azam kwa maana walivyotufanyia ni zaidi ya utapeli

Brand ya Azam kubwa Sana kwa bidhaa nyingine kabla ya kuingia ktk biashara ya media,na brand Yao ilijenga taswira ya uaminifu i'la kwa Mara ya kwanza naona biashara hii mpya ya media /tv inaelekea kuvunja uaminifu wote ambao azam Kama Azam imejingea kwa wateja.

Azam tv ilivyotufanyia ktk maboresho Yao ya vifurushi Ni zaidi ya utapeli,Bora wangetumbia kuanzia mwanzo kuwa wanapndisha Bei za vifurushi kuliko kuleta ujanja ujanja wa kutoa chanel hi kupeleka huku hii kupeleka huku na kuwavuruga watwja.

Mimi kuanzia zamani nilikuwa natumia kifurushi Cha Azam plus Cha elf 23,humo nolikiwa naweza kuangalia chanel zote za michezo maana naangaliaga sana ESPN, Ukitoa Azam sports 1 na 2, pia chanel zote za watoto Kama baby tv n.k,chanel za wanyama,chanel za movies zote nilikuwa nazipata n.k

Juzi wamekuja na ujanja ujanja wao wkatudanganya wameshusha Bei za vifurushi Tena wakawa wanajinadi kabisa cha 23,000 Sasa hivi kitakuwa elf 20,nikajiroga kulipia elf 20,nilichokipata Ni zaidi ya Kero,chanel zote ninazoangaliaga hakuna,watoto chanel zao hakuna zolizopo sizo wanazozitaka wao,Sasa wameshusha Bei ipi?

Mbaya zaidi nikataka nifanye topup niende kifurushi Cha juu kumbe haiwezekani labda ulipie Tena upya,yaani elf 28 nyingine, ikabidi nivumilie mwez uishe,kifurushi kimeisha jana,watoto wanataka kuangalia tamthilia zao na mimi sina hela yote ya kulipia kwa mwezi nikasema nilipe walau kwa wiki nakuja kuangalia Bei ya wiki sijui wameset kwa margin ipi kubwa pasipo mfano kuliko ya mwezi, imagine kifurushi Cha elf 20 kwa mwezi,ambapo ukigawanya kwa wiki 4 unapata elf 5,Basi kwa sabahu za kibiashara wangeweza kiweka hata elf 6 ili au 7,kwa margin ya elf 2 siyo mbaya wao wamekuja kuweka elf 9 kwa wiki yaani ukizidisha Mara 4 unapata almost elf 36,mbona havina mahusiano?

Kwa kweli mm Kama niliyekuwa mteja nimekwazika Sana,na kwa kuwa Sina namna ya kufanya nyingine nimeamua kuvunjilia mbali kisimbuzi hiki,Hawa jamaa hapa nyumbani nawaambia kimeharibika,nifanye mpango niwanunulie walau DSTV wanaonekana hawana Mambo ya kiswahili,watazoea tamthilia na michezo ya kule Kama walivozoea Azam!
Tafuta hela mkuu!
 
Nami nawahama rasmi January hi mwishoni,malipo yakiisha time 18000 goodbye,maana elfu 18 hupati Azam one wall two Wala sinema zao,ambazo wanapenda watoto
 
Nauza ving'amuzi vya startimes... Wako poa kwa tamthilia na channel za watoto.
Screenshot_20210310-191354.jpg
 
Mnazingua mnaiwaza elfu 28 kweli?weka kifurushi cha elf 28 kuepuka kero.kama uwezo unaruhusu weka na dstv hapo kifurushi kikubwa maisha yanakuwa burudani,
 
Back
Top Bottom