Nimefikiria kwa makini sana nimeona ni jambo sahihi kuoa binti wa kisabato, sababu ni zifuatazo;

1. Nitaokoa zaidi ya milioni 2 kwa mwaka kutoka kwenye hela za kuhudumia nywele. Milioni 2 ni kama matofali 2000.

2. Kwenye msosi nitaokoa hela nyingi sana kwa mwaka zaidi ya milioni 3 kwasababu mama wenye nyumba hatataka kula kitimoto, rost nyama, mayai, biriani, pilau, cocacola, majani ya chai, maini, na vitu vingine vitamu yaani rojorojo.

Badala yake mboga za majani, juice ya mwarobaini, maharage, na matunda vitashika hatamu. NB: Kitimoto nitakula kwa siri bila mke kujua.

3. Nitakuwa na utulivu wa nafsi kwasababu wife sharti lake kuu ni kumwacha awe huru na sabato yake.

Isitoshe wachungaji wa kisabato sio kama kina Mwamposa ambao huwafanya mateka wa kiimani wake za watu.

4. Nina uhakika wa watoto wangu kuwa katika maadili mazuri kwasababu kanisa lina mambo mengi kwenye makuzi ya watoto. Kitu kama PF naunga mkono sana.

Ila watoto wakiwa wakubwa nitapiga marufuku kuhudhuria camps za vijana kwasababu ya kashfa ya ngono iliyopo.

5. Nitaimarika sana kiafya kwasababu SDA wako vizuri sana kwenye miongozo kuhusu afya kwa waumini wao. Ikumbukwe vitu vyote wasabato wanavyosema tusitumie vina madhara ambayo yamethibitishwa kisayansi sema ni ubishi wetu.

Kwa mfano kitimoto ni kitu hatari.

Kiukweli nataka nioe binti wakisabato ila kabla ya kuoa lazima nikague vyeti vyake. Kigezo cha ufaulu ni muhimu sana.

Lazima mke wangu kwa O-Level awe na C ya hesabu au zaidi, English kuanzia D.
Sijawahi kufaulu hesabu kwenye maisha yangu Ila nafikiri maisha yanasonga tuu. Ila nafikiri sikuepo kilaza
Screenshot_2021-12-05-21-04-42-13_e2d5b3f32b79de1d45acd1fad96fbb0f.jpg
Screenshot_2021-12-05-21-07-23-12_e2d5b3f32b79de1d45acd1fad96fbb0f.jpg
 
Nadhani unaongelea mabinti wa kisabato wa zamani, zama hizi hasa maeneo ya mijini karibu mabinti wote wanafanana kwenye tabia chafu. Hakuna tofauti kati ya mkatoliki, mlutheri, mpentekoste, msabato na muislamu. Imani imekuwa kama blanketi tu la kufunikia ufuska na uhuni mwingine.
Kuoa na kuolewa zama hizi ni jambo la hatari mnoo.
 
sheria mojawapo ni amri kumi ambayo mojawapo Yesu aliivunja (ikumbuke siku ya Bwana ukaitakase), ndio maana nimesema jiwe la kwanza mlianza kumrushia Yesu, sisi tunafuata tu. kwa kukusaidia, wamwabuduo Mungu halisi huwambudu katika Roho na kweli, Roho lazima awe ndani yako, sheria bila Roho ni upotevu. KESHO KAMUULIZA MCHUNGAJI WAKO KUHUSU HAYA, then lete mrejesho kama atakujibu:-

1. Wakolosai 2:16-17 16 Kwa hiyo msimruhusu mtu awahukumu kuhusu chakula au kiny waji, au juu ya kuadhimisha sherehe za dini, sikukuu ya mwezi mpya au siku ya sabato. 17 Maana hizi zilikuwa ni kanuni za muda tu au vivuli vya yale mambo ambayo yangekuja; lakini hakika ya mambo yenyewe ni Kristo.16 Therefore do not let anyone judge you by what you eat or drink, or with regard to a religious festival, a New Moon celebration or a Sabbath day. 17 These are a shadow of the things that were to come; the reality, however, is found in Christ.

2. Warumi 3:20 20 Kwa hiyo hakuna binadamu hata mmoja atakayehesabiwa kuwa na haki mbele za Mungu kwa kufuata sheria; bali sheria hutufanya tutambue dhambi. 20 Therefore no one will be declared righteous in God’s sight by the works of the law; rather, through the law we become conscious of our sin.

3. Warumi 3:27-28 27 Sasa kujivuna kwetu kuko wapi basi? Hakupo. Je kumeondo lewa kwa msingi gani? Kwa msingi wa kutimiza sheria? La. Kumeon dolewa kwa msingi wa imani. 28 Kwa maana tunasisitiza kwamba mwanadamu anahesabiwa haki kwa njia ya imani na wala si kwa kutenda maagizo ya sheria.27 Where, then, is boasting? It is excluded. Because of what law? The law that requires works? No, because of the law that requires faith. 28 For we maintain that a person is justified by faith apart from the works of the law.

kumbuka hapa audience ilikuwa wamataifa ambao walikuwa hawafuati sharia za Musa tangu zamani sasa wameingia kwenye ukristo na wayahudi wakaanza kuwahukumu kwamba lazima wafuate sheria na kula vyakula kwa mujibu wa sheria. ukimaliza kusoma hii mistari, tafuta sehemu yeney kitimoto tandika kisawasawa na soda baridi ndio urudi tubishane tena.
ciao!
Akizingatia haya umwambiayo atakuwa amepata kitu cha thamani sana maishani mwake. Ashukuriwe Roho akuongozaye kuandika haya.
 
Ukikaa ukatulia ukawaza na kujua kipi ni hitaji la moyo wako matatzo kwenye ndoa yatakuwa kidg pia yakuvumilika kabsa, huo ufaulu cjui connection zake n zpi,
 
Kwa hakika mapenzi yamekuwa kama biashara ,kuna mtu usipompa pesa anaona hapendwi na mwanaume asipopewa penzi anaona hapendwi,ila mimi sipo hivyo,hakika mabinti wanaotoka dhehebu la kisabato wana hofu ya mungu kwanza, hawana makuu ,hawana tamaa,nimepata binti wa kisabato ana kila sifa za kuitwa wife material natarajia ndo atakua mke wangu ndani ya miaka miwili
 
Kama na wewe ni mtakatifu kama huyo binti basi sawa! Lakini kama na wewe ni wale wale hapo kwa namna yoyote ile lazima huyo binti akuache ili upate galasa mwenzio muende sawa usije ukamtesa mtoto wa watu bure!
 
Kama na wewe ni mtakatifu kama huyo binti basi sawa! Lakini kama na wewe ni wale wale hapo kwa namna yoyote ile lazima huyo binti akuache ili upate galasa mwenzio muende sawa usije ukamtesa mtoto wa watu bure!
Me mwenyewe napitia njia zile zile
 
Back
Top Bottom