Nimeamua kumfuata shetani, kwakuwa Mungu sijawahi kumwona na wafusi wake ni wanafiki sana

Ukitaka ufaidi kua mfuasi wa shetani jiunge Frimanson,utafurahia sana kila lakheli mpinga Kristo
 
Safiri salama usisahau kutuletea mrejesho wa kishetani na mamlaka yake
 
Hayo unasema wewe, onesha maandiko ni wapi Yesu alyhi salaam anasema "Mimi Mungu".

Mimi nakuonesha haya:

Yohana 17.3-4
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

Hapo ni dhahiri shahiri kuwa yeye ni mtume na ametumwa tu.
Unazijua nafsi tatu za Mungu?
Ndiyo maana wakati wa kumuumba Adamu, Mungu alisema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu "hakusema "Na nimfanye mtu kwa mfano wangu " soma kitabu cha mwanzo, manake kuna Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu!

Ndiyo maana Yesu aliwaambia wayahudi yeye alikuwepo kabla ya baba yao Musa wakataka kumpiga mawe, wanadamu hawapendi kuambiwa ukweli,
Nakushauri umkubali huyu Yesu maana njia ya mbinguni ni yeye peke yake,
Mitume wengine hawakufufuka
Lakini yeye alishinda kifo, mauti na kaburi
 
Shetani ni father of deceiver...n fundi wa kudanganya ili akuchote mkafe wote hajawahi kuwa na huruma hata chembe na kiumbe chochote kile.

Ndo maana hata Yesu halijaribiwa na shetani kwa kuaidiwa kupewa Dunia nzima kwa kigezo cha kumtosa mungu, bahati nzuri Yesu anamjua shetani vizuri.

Mleta mada unataka kuwa royal opposition wa master of the people and universe..God...the most high...! Hatari inayokukabili ni zaidi ya hatari. Na pia ni bora kuamini mungu yupo halafu ukamkuta kuliko kuamini hayupo halafu ukamkuta..ist the potential disaster.

Pointless,
1.ufundi wa kudanganya shetani kautoa wapi?sio kwa mungu?
2.kwa nn yesu ajaribiwe na shetani?yesu si mungu pia au?
Think big...
.…........Free ideas............
 
Mungu "mwenye enzi" amekuumba wewe kwa mapenzi yake, ila uamuzi wa kumuamini na kushika amri zake au kumfuata shetani ni wa kwako. Si vyema sana kuchagulia watu maamuzi ila nina amini kutokana na pita pita zako za hapa na pale umeshawahi kufahamu au kujua hatma ya kumfuata shetani na mambo yake na kama bado basi si vibaya ukaperuzi vitabu mbali mbali na machapisho mbali mbali ili upate huo uelewa na ufahamu.
Ikiwa kuamfuata shetani ama mungu ni hiari je,Kwa nini kuna adhabu endapo nitamfuata shetani.
Think big.....
.........…Free ideas.......
 
Shetani ni father of deceiver...n fundi wa kudanganya ili akuchote mkafe wote hajawahi kuwa na huruma hata chembe na kiumbe chochote kile.

Ndo maana hata Yesu halijaribiwa na shetani kwa kuaidiwa kupewa Dunia nzima kwa kigezo cha kumtosa mungu, bahati nzuri Yesu anamjua shetani vizuri.

Mleta mada unataka kuwa royal opposition wa master of the people and universe..God...the most high...! Hatari inayokukabili ni zaidi ya hatari. Na pia ni bora kuamini mungu yupo halafu ukamkuta kuliko kuamini hayupo halafu ukamkuta..ist the potential disaster.
kwa hiyo wewe unaamini Mungu yupo kwa kuwa tu una hofu siku ukienda halafu ukamkuta itakuaje.
Ni hofu ndiyo inayokufanya uamini Mungu yupo..... unadhani mungu anapenda kuogopwa?
 
Walokole wanadai wanamwomba Yesu awapelekee naombi yao kwa Mungu mwenyezi.Na wanapiga kelele na kunena kama vichaa,kiasi cha kuwaombea kifo.
Kwakuwa shetani wanayetwambia yupo na wala hajawai kuonekana na wala hana mafundisho yake naomba niwe mfuasi wake maana hana kelele hajawai kuitisha mikutano.Karibuni tujiunge tutasonga mbele sana.
NIKUPE JIBU KWA HERUFI KUBWA::KAMA HUJAMWONA SHETANI CHUKUA KIOO UJIANGALIE. UTAMWONA.
 
Ikiwa kuamfuata shetani ama mungu ni hiari je,Kwa nini kuna adhabu endapo nitamfuata shetani.
Think big.....
.........…Free ideas.......
Very simple, it is not like a rocket science, nothing needs to think big here, kufuata sheria za nchi au la ni hiari yako, sasa usipozifuata inakuaje?
 
Unazijua nafsi tatu za Mungu?
Ndiyo maana wakati wa kumuumba Adamu, Mungu alisema "na tumfanye mtu kwa mfano wetu "hakusema "Na nimfanye mtu kwa mfano wangu " soma kitabu cha mwanzo, manake kuna Mungu Baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu!

Ndiyo maana Yesu aliwaambia wayahudi yeye alikuwepo kabla ya baba yao Musa wakataka kumpiga mawe, wanadamu hawapendi kuambiwa ukweli,
Nakushauri umkubali huyu Yesu maana njia ya mbinguni ni yeye peke yake,
Mitume wengine hawakufufuka
Lakini yeye alishinda kifo, mauti na kaburi

Usiniletee story za redio za zamani "three in one".

Soma:

Mathayo 27:
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

"Mungu" kaachwa na Mungu?

Hamfikirii japo kiduchu?
 
Kuna kanisa limeanzishwa wiki iliyopita hapa mtaani kwetu jana nimemsikia muhubiri anasema mashuka yaliyoombewa na kubarikiwa yanatolewa kwa laki moja na nusu! ila mkuu huko unakotaka kwenda nikutakie kila la kheri ukifika wasalimie
 
Walokole wanadai wanamwomba Yesu awapelekee naombi yao kwa Mungu mwenyezi.Na wanapiga kelele na kunena kama vichaa,kiasi cha kuwaombea kifo.
Kwakuwa shetani wanayetwambia yupo na wala hajawai kuonekana na wala hana mafundisho yake naomba niwe mfuasi wake maana hana kelele hajawai kuitisha mikutano.Karibuni tujiunge tutasonga mbele sana.
Duu nimecheka kwa kusikitika, ila kwa kuwa umeamua mwenye, hata kurudia MUNGU utamua wewe mwenyewe, na nina uhakika ipo siku utakutana yae kwenye kona moja hivi utalia na kutoa machozi baada ya kugundua shetani ni mnafiki zaidi
 
Shetani ni sifa ewe punguani.

Wakristo wanadai Yesu (ambae mwenyewe anasema yeye ni mtu) kuwa ndiyo Mungu wao, tena wamewekewa picha ya mzungu, basi wengine mpaka wanaiabudu.
unapenda sana ligi za udini, ukiambiwa ya upande Wako unatamani kujilipua we gaidi mkubwa
 
Usiniletee story za redio za zamani "three in one".

Soma:

Mathayo 27:
46 Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?

"Mungu" kaachwa na Mungu?

Hamfikirii japo kiduchu?
Haya mambo hayaendi kimwili kama unavyofikiria,
Jiulize kwa nini mapepo yanatoka kwa jina la Yesu
 
Dini uloiona ni walokole tu?!! Mbona wasabato hawapigi kelele hujahamia huko?!

Na utaendelea kuwa mfuasi wa wafuasi maana Unaishi kwa kuangalia watu huna akili ya kujitegemea wewe! wala huna akili ya kufikiri unategemea kufikiriwa
 
kwa hiyo wewe unaamini Mungu yupo kwa kuwa tu una hofu siku ukienda halafu ukamkuta itakuaje.
Ni hofu ndiyo inayokufanya uamini Mungu yupo..... unadhani mungu anapenda kuogopwa?
Kwanza kwa kutaka kukuthibitishia kwamba mungu yupo angalia the "perfect distance" kati ya dunia na jua vimewekwa kwa umbali sahihi kabisa incase dunia ingesogezwa mbele kwa hatua chache tu kuelekea jua basi isingeweza kuhimili moto mkali unaowaka pale kwenye jua na ingeungua na kuteketea na duniani kusingeweza kuwa na maisha.

At the same time Mungu angeisogeza dunia nyuma kutoka lilipo jua basi dunia nzima ingefreeze kwa Baridi kali kwani inachemshwa na jua.

Hivyo mungu kutaka kuthibitisha how genius he is and he has powers that are limitless..akaiweka jua na dunia at perfect distance ili maisha ya viumbe wote duniani yawezekane.

Point 2.
Mungu anapenda saana kuogopwa na kupewa heshima yake. That's why hata wale watumishi, manabii na mitume wake walitamani kumuona lakini hakawaambia atakaeniona hataishi maana utukufu wangu unatisha. Hata wale Makerubi na maferasi wanaomzunguka na kumsifu na kumtukuza akiwa kwenye kiti cha enzi wana mabawa sita....unajua kazi ya hayo mabawa...tega sikio..mawili ni kwa ajili kufunika nyayo zao, zile mbili ni kwa ajili ya kupaa na kuelea angani wakiwa wanamwimbia mtakatifu mtakatifu awapo kwenye kiti chake cha enzi...Yale mabawa mawili mengine ni kwa ajili ya kufunika nyuso zao wasimwone maana utukufu wake hata hao malaika hawawezi kuhustahimili.

Mungu,God,Jehova, Jah, Allah, Yahwe, Sebbha,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom