Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

JF
Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.
Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF- hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.

Heshima kwako ELNINO,

Wazo lako zuri sana binafsi nimeshalifanyia kazi tangu mwaka 2008, baada ya kugundua mshahara pekee bila kuwa na kipato kingine cha uhakika ni balaa kadri siku zinavyosonga mbele kwasababu majukumu yanazidi kuongezeka eg:watoto na nk.

Nimenunua shamba eka 250 kwa tsh 3.5 mil maeneo ya Kabuku Tanga na kuanza kulima mwaka huo huo(2008).Project yangu nimeigawanya katika sehemu kuu mbili [1] Mazao ya msimu eg;Mahindi,Dengu,Choroko,Mbahazi,Alizeti na Ufuta

[2] Mazao ya kudumu eg Maembe ya kisasa,Machungwa,Mananasi,korosho na Minazi.

Mazao ya msimu yamenisaidia sana kupunguza gharama za uendeshaji ambazo kwa kweli ni kubwa kuliko ulizozitaja hasa ukizingatia kila mwezi naenda shambani mara mbili.

Zipo faida nyingi ambazo tayari nimeshaanza kuziona hata hivyo kitu kilicho wazi kabisa ni kuongezeka kwa kipato mara dufu.

Ushauri wangu kwa wanaJF wote tuchangamkie kilimo kwasababu kinalipa sana,tuache kubweteka mijini au kufanya shughuli ambazo tayari watanzania wengine wameshazianzisha eg saloon,biashara ya taxi au daladala. Ardhi Tanzania bado ni rahisi sana nina uhakika kama unapata mshahara kuanzia 500,000/= na kuendelea unao uwezo wa kumiliki shamba kubwa ambalo litakusaidia wewe na kizazi chako.

Tumekataa wana EAC kumiliki ardhi Tanzania wakati sisi wenyewe tunaiangalia bila kuifanyia kazi itafika siku hatutakuwa na sababu za kuwakatalia. Hongera sana Elnino umeamua jambo jema Mungu akubariki.

Naomba kuwasilisha.
 
Sawa kuna miscellaneous lakini kupita 5m target is vigumu - kwa mafano sasa hivi mpaka upandaji nitakuwa nimetumia 2m tu - palizi nitaweza kutumia 1m nyingine - uvunaji na kuhifadhi ni 3m approx
hata ukisema nipate magunia 20 kwa heka still jumla itakuwa tatal gunia 1000 times 60,000 = 60m ( Kadirio la chini kabisa)
Heshima kwako ELNINO,

Mkuu wangu bei ya mbegu ni tsh 3500/= per kilo,utatakiwa kutumia kilo 10 kwa kila eka. 3500 x 10 x 50 = 1,750,000/=.kulima eka moja si chini ya tsh 20,000/= x 50 = 1,000,000/=.kupanda eka moja si chini ya tsh 5,000/= x 50 = 250,000/=,kupalilia eka moja si chini ya 10,000/= x 50 = 500,000/= kuvuna,kuhifadhi [magunia & dawa],kupukuchua na kusafirisha ni gharama inategemea na umbali wa masoko.Mkuu gharama za chini kabisa weka 8,000,000/= pembeni kwaajili ya hiyo shughuli yako.
 
nikaribishe niwe jirani yako huko Kabuku,
nami nataka kununua ardhi kwa kilimo cha umwagiliaji

thanks
 
Hongera sana mzee,napenda sana lakini tatizo supervision muda unaitajika sana,wabongo ukiwachia lazima wakufanye mbaya.all in all imetulia sana
 
nikaribishe niwe jirani yako huko Kabuku,
nami nataka kununua ardhi kwa kilimo cha umwagiliaji

thanks
Kwa nini usianze wewe na sisi tukufuate? joke. Mkuu kuna mapori mengi sana ambayo sio ya kununua ila kuokota tu basi, Mimi naamini tukiwa pamoja ki-jkt jkt hivi kambi itanoga.
 
Kwa nini usianze wewe na sisi tukufuate? joke. Mkuu kuna mapori mengi sana ambayo sio ya kununua ila kuokota tu basi, Mimi naamini tukiwa pamoja ki-jkt jkt hivi kambi itanoga.
Mkuu Malila
nilekeze how to go about aquiring hilo farm,tuwesote ki-jkt,nipedata by PM,
nataka kulima embe na parachichi
 
KWANGU MIMI NI KATI YA THREAD ZILIZOKWENDA JANDONI(wazungu mtasema shule) KWA WASANII WATASEMA INA VINA NA MIZANI.....!
TUSIISHIE KWENYE MANENO TUFANYE KWA VITENDO....PROBLEM MIMI NA WEWE TUNA MANENO MINGI VITENDO VICHACHE,
mwinyi e-mail ya PM amtumie pm aone WATU WAKE WANAVYOJADILI KILIMO KWANZA ....!
VIVA LA KILIMO....!
 
Mkuu Malila
nilekeze how to go about aquiring hilo farm,tuwesote ki-jkt,nipedata by PM,
nataka kulima embe na parachichi

Unataka shamba la parachichi la ukubwa gani? na embe za muda mrefu au mfupi? Je umesikia Cocoa za kilimo hai?

Baada ya mwezi mmoja nitakuwa na majibu ya maswali yako hasa kuhusu Parachichi. Ukienda Mkuranga pwani ardhi ipo kibao kwa ajili ya embe,kama uko serious ni-pm nikuelekeze utakaponunua ardhi bila dalali wala 10%.
 

Heshima kwako ELNINO,

Mkuu wangu bei ya mbegu ni tsh 3500/= per kilo,utatakiwa kutumia kilo 10 kwa kila eka. 3500 x 10 x 50 = 1,750,000/=.kulima eka moja si chini ya tsh 20,000/= x 50 = 1,000,000/=.kupanda eka moja si chini ya tsh 5,000/= x 50 = 250,000/=,kupalilia eka moja si chini ya 10,000/= x 50 = 500,000/= kuvuna,kuhifadhi [magunia & dawa],kupukuchua na kusafirisha ni gharama inategemea na umbali wa masoko.Mkuu gharama za chini kabisa weka 8,000,000/= pembeni kwaajili ya hiyo shughuli yako.

Heshima kwako Mkuu,

Ama kwa hakika wewe umelima...haya mahesabu yako yako kwenye mstari kabisa. Ila bei ya kulima kwa Trekta mkuu mimi ninavyojua sio chini ya 30,000/= Pia hapo umesahau bei ya Magunia, ambapo kwa mwaka 1996-1999 nilipokuwa nalima gunia moja ilikuwa 180 - 250/=

Mkuu EL NINO

Nakupa hongera sana kwa juhudi zako. Ila nakushauri angalia tena mahesabu yako kama walishauri wadau hapa.

Kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania...huko tuendako bila ya kuwa na Shamba tutakuwa maskini wa kutupwa.
 
Naona at least watanzania kadhaa wana mawazo chanya.

Kumbuka kuna kukosea mwaka pia (sikukatishi tamaa mm mwenyewe ni mkulima, lkn kuna jamaa yangu tulikuwa tukichuuza wote enzi hizo, alichimbia Tsh 50M kibaigwa kwa mategemeo ya kuvuna mabilioni, mwaka huo jua likawaka hakuvuna kitu-alitamani pesa hiyo angenywea bia!!).

Kilimo kinalipa sana jamani ukienda nacho vizuri hauna haja ya kutumikishwa na mtu kwa mshahara wa milioni 20 kwa mwezi
 
Naona at least watanzania kadhaa wana mawazo chanya. Kumbuka kuna kukosea mwaka pia (sikukatishi tamaa mm mwenyewe ni mkulima, lkn kuna jamaa yangu tulikuwa tukichuuza wote enzi hizo, alichimbia Tsh 50M kibaigwa kwa mategemeo ya kuvuna mabilioni, mwaka huo jua likawaka hakuvuna kitu-alitamani pesa hiyo angenywea bia!!). Kilimo kinalipa sana jamani ukienda nacho vizuri hauna haja ya kutumikishwa na mtu kwa mshahara wa milioni 20 kwa mwezi

Kilimo cha kutegemea mvua ni hatari,lakini kunamaeneo yana mito namifereji kiasi kwamba huhitaji nguvu kubwa kupata maji. Nendeni nje ya maeneo yenye majina makubwa mkaone mambo mazuri huko. Halafu yapo ni wewe kujimegea.
 
Kilimo cha kutegemea mvua ni hatari,lakini kunamaeneo yana mito namifereji kiasi kwamba huhitaji nguvu kubwa kupata maji. Nendeni nje ya maeneo yenye majina makubwa mkaone mambo mazuri huko. Halafu yapo ni wewe kujimegea.

ni kweli kabisa mkuu, maeneo yapo mengi sana ya bwerere. mimi nililipa elfu 3o serikali ya kijiji, nikapewa uanachama wa kijiji na kiwanja cha kujenga kibanda changu, kisha nikapelekwa shambani nikajihesabia hekari za bureeeee zikiwa na miwanga ya kumwaga!!!

karibuni vijijini jamanni, ni raha sana, hasa ukijua kuishi na wanavijiji (kutoa landrover ya bure misibani, jenereta na mafuta bure harusini,amini nakwambia pesa iko shambani)
 
Elnino, kwa hili tuko pamoja. Safi sana.

Ntakuandikia email. Tuwasiliane mgosya.
 
Hivi nikisema najitolea kwenda kuishi kijijini kwa makubaliano kwamba nitakuwa MTIIFU kufanya kazi zote za usimamizi wa shamba kuanzia kuandaa
shamba mpaka kuvuna kwa makubaliano ya mimi kutumia nguvu,busara na hekima niliyopewa na Mungu na mtu mwingine ajitolee fedha,
ili kufanikisha hilo zoezi naweza kupata mtu wa kupiga naye kazi?

Makubaliano yanafanyika baada ya kila mmoja kiridhika na mwingine kwa kufahamu nyumbani na wazazi wa mwenziwe kama wapo, kisha sheria na taratibu nyingine kufuatwa.

Hili swala linawezekana?


Ila siyo kilimo cha hekari kumi au ishirini(isiwe chini ya hekari 50), hapa nazungumzia shamba la ukweli maana hiyo ndiyo itakuwa ajira yangu.
Yaana kifupi naachana kabisa na mambao ya mwisho wa mwezi.

Huyo mtu yupo?
 
Back
Top Bottom