Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!Ofa!!!ofa!!!ofa!!!
Ninauza mayai ya kuku wa kienyeji(Malawi) kwa ajili ya kula na pia ukitaka kwa ajili ya kutotolesha yanapatikana kwa order.

Bei ya tray moja ni elfu kumi tu(10,000tsh) ninapatikana Dar es salaam Tegeta-Madale na ukitaka tray kuanzia kumi unaletewa popote ulipo bure ila ukihitaji pungufu ya hapo utatoa nauli nusu na sisi tutakuchangia nusu..kwa mawasiliano zaidi 0769345032 au 0654250816 karibuni sana.
 
This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.[/QUOTE]
thanks brother kwahii kituu nilikuwa nawaza ntaanzajeee kulimaaa nimepata mwangaa sasa ,.
 
nauliza mbegu nzuri za mahindi kwa kilimo ni zipi na zinapatikana wapi, hasa yale mahindi makubwa na marefu
 
JF

Hali ya uchumi ni ngumu sana kwa watu wote hasa tunategemea mwisho wa mwezi. Weekend nilijaribu kupiga hesabu za mishahara yangu in next 10 years....ooooooooooops hazikufika hata 500millions Tshs.

Kwa maneno mengine kama sintantafuta kitu mbadala mbali na mshahara wangu cha kufanya basi nishakufa maskini na sintakuwa na chochote cha kuwaachia wanangu.

Maisha ni magumu sana kadri siku zinavyoenda mbele, sasa nimeamua kuanza kilimo kwa mara ya pili, awamu hii natumia mshahara wangu kama mtaji, nimewaambia kwa mara ya pili sababu kilimo cha kwanza nilifanya pamoja na wazazi wangu hadi nilipomaliza form four miaka hiyo, hicho hakikuwa na manufaa yeyote sababu ya mtaji na ufahamu.

Kwa sasa nimeanza na heka 50 ( 70m by 70m), nipo morogoro - pale Tuliani. Heka zote zimeshalimwa sasa tunapanda - nita expand my project up to 1,000 in next 3 - 5 years.

Makadirioni kwamba kila hekari average ni gunia 30, nitategemea kupata gunia 1500 za mahindi kutokana na hekari zangu za sasa 50. Kila gunia average selling price ni Tshs 60,000. kwa hiyo nitapata average Tshs 90m by July this year.

Running cost itakuwa approx 5m, so super profit ni 85m by July 2010.

Sasa 85m kwa mtu anayepokea sh 1million kwa mwezi ni mshahara wake wa miaka 7 na ushee-- teh teh teh teh

By next year nitaexpand to 200 hektas, nitalipima shamba langu na nijaribu kutafuta mikopo katika mabenki - or mbia toka SA au Zimbabwe. by 2015 wakati Dr Slaa anakuwa Rais wa nchi nitakuwa millionea. Sasa ole wenu mseme nimefanya ufisadi.

This is a challenge to you JF - hasa mnaopata less than 5m per month - think twice and join me.

Kumbuka shairi la darasa la nne - Kama mkitaka mali mtayapata shambani - huu ni wosia.
Mkuu, napenda kujua gharama za kulima mahindi.
kukodi shamba hekari moja ni shilingi ngapi?
mbegu bora shilingi ngapi?
gharama za mbolea, kupalilia etc
 
Naombeni msaada tafadhali mwenye uzoefu na kilimo cha mahindi Moshi... Naomba kujua formula(umbali mche na mche) itakayonipelekea kuvuna kiwango kikubwa kwa heka moja..
 
Hoja yako ni poa sana mkuu... tatizo umeileta muda kupendana aiseeee....
Mkuu ebu vumilia maana hii mida wakulima wengi ndio wanamalizia kukitupa cha pili kwa shemeji zetu
 
Heshima kwako ELNINO,

Mkuu wangu bei ya mbegu ni tsh 3500/= per kilo,utatakiwa kutumia kilo 10 kwa kila eka. 3500 x 10 x 50 = 1,750,000/=.kulima eka moja si chini ya tsh 20,000/= x 50 = 1,000,000/=.kupanda eka moja si chini ya tsh 5,000/= x 50 = 250,000/=,kupalilia eka moja si chini ya 10,000/= x 50 = 500,000/= kuvuna,kuhifadhi [magunia & dawa],kupukuchua na kusafirisha ni gharama inategemea na umbali wa masoko.Mkuu gharama za chini kabisa weka 8,000,000/= pembeni kwaajili ya hiyo shughuli yako.
mkuu nimekuwa nikilima mahindi kila mwaka toka mwaka 2012 lakini gharama alizoweka mtaalam hapo ni tofauti kabisa na huku kitaa
 
Nipo tanga wakuu naomba kujuzwa ni sina gani ya mbegu inayostawi vizur ukanda huu mana naskia kuna mbegu bora sina nyingine na zna Tija kuliko mbegu za asili.

Naomba wakulima mnijuze
 
Fika uyole kilimo pale au tafuta contact zao
mmhh uyole si iko mbeya mkuu?

Ebu afanye kwenda ofisi ya kilimo katika wilaya anayotaka kulima, ndo jukumu lao watakupa update za kila kitu kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna tunaita seed to seed ( ni imani yangu watasimama na wewe kila hatua ya shamba lako kama kweli una nia ya kulima).
 
Fika uyole kilimo pale au tafuta contact zao
Duuh! hatari kwelikweli. Mtu yupo Tanga halafu aende hadi Uyole kuulizia mbegu inayofaa Tanga! hatari kweli kweli. Mwambie aende TFA pale karibu na Mkwakwani Stadium watamshauri mbegu inayofaa kulingana na lilipo eneo lake maana hata Tanga inahali ya hewa tofauti tofauti kulingana Wilaya alipo.
 
Duuh! hatari kwelikweli. Mtu yupo Tanga halafu aende hadi Uyole kuulizia mbegu inayofaa Tanga! hatari kweli kweli. Mwambie aende TFA pale karibu na Mkwakwani Stadium watamshauri mbegu inayofaa kulingana na lilipo eneo lake maana hata Tanga inahali ya hewa tofauti tofauti kulingana Wilaya alipo.
Asante,mkuu
 
Nachokushauri ndugu yangu usiwe sana optimistic hasa kwenye masuala ya bei.. mfano kwa sasa gunia ni 35,000/= tena na japo serikali imeruhusu mahindi kuuzwa nje lakini bado wakenya wamegoma kununua yetu wananunua ya Zambia.. ila hoepful by March next year things will be different and maize demand itakuwa kubwa tofauti na sasa.. Yangu nimeamua kuhifadhi tu kwa dawa nisubiri.. Siku zote wanasema "Farming looks mighty easy when your plow is a pencil and you're a thousand miles from the corn field." hizo hesabu utaona mamilioni kwenye daftari hapo, ila in real life situation ujiandae kisaikolojia hasa kwa hiki kilimo chetu cha kutegemea mvua..Ningekushauri fanya hivi;
1. Uzuri unalima turiani hapo, na shamba lako ni kubwa.. Nenda pale Tanfeed International kwa Profesa Kekule, huwa kiwanda chake cha kusaga chakula cha kuku anatumia yale mahindi ya njano.. na mara ya mwisho kuongea nae alisema ananunua kilo moja si chini ya shilingi 600.. This was last year when i met him.. sasa unaweza kuingia mkataba nae angalau ukawa na uhakika na soko kabla hata ya kuingia shambani.. si lazma ulime mahindi yote ya njano lakini at least you have that assurance.
2. Kama wewe si mtaalamu wa kilimo basi hapo halmashauri kuna mabwana shamba wamekalia tu mabenchi..nenda onana na crops officer akupe mtaalamu ambae atakuwa consultant wako..uzuri wa kutumia mtaalamu wa eneo husika ni kwamba wamekaa hapo wanaielewa ardhi vizuri, mbolea zipi zinarespond vizuri, mbegu gani nzuri, visumbufu gani vya mazao hasa wadudu na magonjwa na general agronomic practice utakayokupa matokeo chanya kwa kuwa kila agro ecological zone zinatofautiana.. Kwa hiiyo uwe na mtu wako mmoja wa kukupa ushauri.. hata kama una utaalamu, fanya hivyo utajikuta unajifunza kitu.. usiogope vigharama vidogo vidogo kama nauli yake, posho au tips..you are investing and you dont wanna take any risks..Make use of these experts. Pia uzuri mwingine ukimtumia mtaalamu yeye atajivunia kuwa ana mkulima wake wa mfano anaemsimamia, so pia ni credit kwake na hii inaweza kufungua hata opportunities nyingine kwako zinazokuja kwenye idara ya kilimo wilayani kwa ajili ya wakulima wa hayo maeneo.
3. Ni vizuri ukafanya diversification.. wanasema a farmer can not put all his eggs in one basket, kwa hiyo uamue may be kufanya mono cropping au intercropping, na kama utaamua ni mahindi tu usipande mbegu ya aina moja.. In case ya shida yoyote na kwa uwekezaji mkubwa hivyo unaweza kupoteza kila kitu ukajikuta unatembea ukiongea mwenyewe barabarani. kwa hiyo diversify, pia unaweza kutupia mikunde katikati au any other crop ambayo in the process itakuondolea weeds pressure na kurutubisha udongo wako
4. Tafuta njia za kukusaidia kufanya operations mbalimbali kwa wepesi.. mfano kwenye palizi unaweza kutumia herbicides, kuliko kutegemea watu, . hii itasaidia kukuwezesha kumaliza mapema kwani ili kupata tija, hutakiwi mazao yako yawe na visumbufu kama wadudu na magugu..ukitegemea watu hadi wamalize itachukua muda sana na mtasumbuana sana
5. Mwisho MUHIMU WEWE MWENYEWE KUWEPO SHAMBANI WAKATI WA HATUA MUHIMU. MFANO KUPANDA, KUWEKA MBOLEA, NA KUVUNA. USIJE UKAWAAMINI WATU UKATEGEMEA SIMU.. Kanunue mbegu uhakikishe imeishia shambani, mbolea hakikisha imewekwa yote kwa vipimo sahihi... kuvuna pia usipoenda unapigwa.. Angalau palizi unaweza kurelax kidogo mradi utaenda kukagua... Watu hasa vibarua hawaaminiki kabisa... hasa kwa hizo hatua nilizokuambia

Nimeamua kushare experience yangu, i hope utaokota mawili matatu yatakayokusaidia.. Goodluck na usisahau kutupa mrejesho

Bro naomba unitafute my [HASHTAG]#0621073599[/HASHTAG] [HASHTAG]#0738640020[/HASHTAG] i could use ua help...thank u
 
TANGA SEHEMU GANI?TUMIA DK 8031 NDYO MDA WAKE IKISHAFIKA TAR 20 APR TUMIA SHUTKA NI YA MDA MFUPI
 
Mbegu ni Dk 80..90 ila Mvua iwe ya kutosha
Mbegu za DK Zina mazao mengi, shida sasa ni unga wake ni mwepesi sana, hivyo hutumia unga mwingi kupika ugali wa watu WACHACHE.
Kwa Tanga ambapo ni pwani, tumia Seedco 403, mahindi yake ni mazito, na pia ya muda mfupi.
 
120 Reactions
Reply
Back
Top Bottom