Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Katika hatua muhimu za kilimo cha ahindi ni palizi. Palizi huwa linahitajika ili kuondosha ushindani wa mahindi na magugu kwa nutriets na mwanga. Bila palizi kiasi kikubwa cha mazoa hupungua kwani mmea hushindwa kukua vizuri.

Magugu yanaweza kusababisha kupungua kwa mavuno hadi asilimia 90 yasipodhibitiwa. Wataalamu wanabinisha kuwa kipindi muhimu kabisa cha kuzuia magugu katika zao la mahindi ni wiki ya kwanza mpaka ya nane toka kuota.

Zipo namna nne ambazo zinaweza kutumika kuzuia magugu. Moja wapo ni hii maarufu ya kupalilia kwa jembe. Palizi hili huwa likifanyika usahihi linasaidia sana mmea lakini linahitaji nguvu kazi kubwa na linachukua muda mrefu. Kipindi cha palizi vibarua wengi wanakuwa mashambani mwao na changamoto ya kuwapata huwa ni kubwa.

Ili kurahisha palizi kuna njia nyepesi ambayo ni ya kutumia kemikali (herbicides Viuagugu) za kuua magugu. Nitaeleza faida na hasara za hizi viuagugu
 
Asante kwa darasa zuri sisi wakulima tumekuelewa. Mimi niko Tanga mbegu niliyotumia ni seed. co vp unaweza kunisaidia sifa ya hii mbegu?

Mkuu unalima Tanga sehemu gani naona sehemu nyingi bado mvua hazijaanza hapo Tanga. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
 
Habari wandugu, ashukuliwe Mungu kuwa tuwazima na anatupigania kwenye changamoto za maisha.
Kwa hali ya kiuchumi ilivyo kwa sasa inatubidi kutafuta miradi tofauti tofauti ili kumudu hali ya sasa. Kwa mtazamo wangu naona sasa ipo haja ya kuitumia ardhi tulio nayo kutuletea maendeleo na sio kukaa na kulalamikia hali ngumu ya maisha.
Katika hayo naombeni kujuzwa kuhusu kilimo. Cha;

1: maparachichi.
Kilimo hiki kipoje, kinahitaji hali ya hewa ya namna gani?
Ni maeneo yepi hapa nchini yanafaa kwa kilimo hiki.?
Vipi kuhusu masoko yapoje?

2:. Matikiti major:
Hapa pia naomba kujuzwa, nifanye nini ikiwa nataka kulima matikiti maji,
Changamoto zake zikoje?

3: Mahindi:
Kilimo hiki kinaonekana kudharaulika lakini kila uchao unga unapanda bei.
Hivi ni njia zipi Bora za kilimo cha mahindi?
Ni mbegu zipi ni bora zaidi kwa hapa nchini hasa kwa mkoa wa morogoro?

Kwa wale wataalamu wa kilimo naomba mnijuze hayo, naamini itasaidia wengi wenye nia kama yangu.
Natanguliza shukurani zangu kwenu.
Ingia hapa
Kilimo cha Mahindi
 
Salaam wakuu.

Msimu huu nimeandaa shamba nataka kulima mahindi. Mnisaidie maswali yafuatayo:
1. Nini tofauti ya mbegu za muda mfupi na mrefu kuhusu kiasi cha magunia unayopata kwa eka?
2. Ni mbegu gani nzuri kupanda huku kwetu Iringa ili nipate mavuno makubwa.
3. Naitaji kg ngapi za mbegu kwa kila eka?.
4. Ni dawa gani zinafaa kupandia na bei zake zikoje?

Pia nakaribisha ushauri wowote kuhusu kilimo cha mahindi.

Asanteni
Majibu yako hapa

Kilimo cha Mahindi
 
Mkuu BabM

Kwa Dar es Salaam ni mbegu gani ya mahindi inafaa kulima?

Asante.

Kwa Dar mbegu ambazo zinakomaa kwa muda mfupi zinafaa zaidi na ambazo ni za ukanda wa chini. Mbegu ambazo zinakomaa kati ya siku 90 na 120 kama zilivyoanishwa hapo juu. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
 
Hakika, hii ni elimu kamambe.

Kupitia elimu kama hii tunaweza kuondokana na umasikini kwa kupata taarifa sahihi na mahususi juu ya teknolojia za Kilimo na kuzifanyia kazi ipasavyo.

Asante sana mkuu, bila shaka wewe ni mtu unaye husika na mbegu bora za Kilimo.

Kama ni ndivyo ningependa kujua upo taasisi gani au duka gani la pembejeo za Kilimo ili kuweza kupata ushauri wa karibu zaidi?

Asante.
 
Mkuu unalima Tanga sehemu gani naona sehemu nyingi bado mvua hazijaanza hapo Tanga. Mbegu nyingine ambazo waweza otesha zikafanya vizuri ni DK8031,Pannar 4m -19, na hizi Seedco 403 au 513.
Mkuu mimi nalima muheza na kwa sasa niko kwenye palizi
 
Back
Top Bottom