Tetesi: Nimeamua Kukisanua: Hii ndiyo sababu ya Jezi za Simba SC kutozinduliwa hadi leo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
46,312
78,133
Mzigo umekuja na Meli na siyo kwa Bung'o ( Ndege ) kama ambavyo Msemaji wa Simba SC Ahmed Ally anavyotudanganya.

Ukweli ni kwamba Kit Supplier wetu Fred Ngajilo 'Vunja Bei' alikuwa na Ukaribu wa Kisamjo Samjo ( Ujanja Ujanja ) na aliyekuwa Boss wa TPA ( aliyeondolewa ) hivi karibuni ( ambaye pia ni mwana Simba SC ) na alipanga Kuingiza Mzigo ( Jezi ) bila kulipa kabisa Kodi au kutoa Kodi Kiduchu tu.

Ukweli ni kwamba Jezi zimekwama Bandarini na Boss Mpya wa TPA 'amekaza' na anataka Kodi ya Serikali ilipwe vinginevyo hazitatoka na huenda Wachezaji wa Simba SC Keshokutwa ( katika Simba Day ) wakacheza Vidali Poo ( Vifua Wazi ) dhidi ya St. George FC ya Ethiopia.

Mmenikera GENTAMYCINE na Kunidanganya kuhusu Usajili wa Mshambuliaji ninayemhitaji zaidi Simba SC Manzoki na kufanya 'Nikeshe' leo kama 'Popo' na sasa 'Nawaanikeni' rasmi.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
46,312
78,133
Duh, hatari sana
Yote ninayoyasema katika NIMEAMUA KUKISANUA zangu za Leo ni kweli 100% na wawe Wapole ru kwani Wakinichefua zaidi nitasema ya ndani zaidi ambayo wengine hata muda huu wanaweza Kukamatwa na TAKUKURU ( PCCB )

Hakuna Kitu GENTAMYCINE nachukia kama KUDANGANYWA na kufanywa Popoma ( Mpumbavu ) na Watu ambao ulikuwa UNAWAHESHIMU japo unajua HAWANA AKILI kama hawa ninaowatolea Uvivu leo.
 

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
46,312
78,133
Acha chuki kwa waliokuzidi mkuu
Kama hizi NIMEAMUA KUKISANUA zangu zote ni za Uwongo waambieni Waitishe Press Conference leo wazikanushe ili niweke nyinginezo Kali Mbili nilizoziweka kama Akiba ili Klabu sasa ichafuke zaidi na baadhi ya Viongozi wenu Wakamatwe.

Hamna Akili.
 

redio

JF-Expert Member
Aug 27, 2016
3,304
5,703
Tuliwaambia kuhusu 20 b ni makaratasi mkabisha, hakuna bank yoyote Kwa apa Tanzania iliyowekwa iyo 20 b. Tukawaambia kuhusu mkataba 26 b ni chupri, mkataba halisi 12.5 b Kwa 5yrs mkabisha, Likaja la Manzoki kuwa Simba ni Chupri mkabisha, limekuja la Jezi mnabisha. Sasa tuendelee kusubiri kwakua uongo unakasi ya kufika Kwa watu na ukweli upo taratibu.
Tuendelee kusubiri ni swala la muda yote yata dhihirika Hadharani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

29 Reactions
Reply
Top Bottom