Nimeamua kujilipua kwenye kilimo, nimeandaa shamba la heka tatu za tikiti na nimepanda

elnyas

Member
Jul 10, 2017
24
56
Habari wana jamvi Mimi nikijana mwenye umri wa miaka 24.

Sasa nimeamua kuanza kilimo baada ya changamoto nilizikumbana nazo baada ya kutoka chuoni.

Nimeandaa shamba la hekar tatu ambalo lina mashimo zaidi ya elf nne 4000, Nimepanda mbegu mbili kila shimo ambapo ntakuwa na miche elf nane 8000, Kila mche uwe na matunda mawili inamaana ntakuwa na matunda elf 16.
kama nikiyatunza vizur ntapata 1500tsh kila tunda kwa hiyo matunda 16000 mara elf moja mia tano ntapata more than 28m.
Hata kama ntauza kwa 1000tsh ntakuwa na 16m ,

Ntaleta mrejesho mwezi wa tisa,

tutakianeni Khmer.

Sent from my HUAWEI P7-L10 using JamiiForums mobile app
 
IMG_20170713_084421.jpg
IMG_20170711_090507.jpg
IMG_20170711_090307.jpg

Sent from my HUAWEI P7-L10 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana,usisahau kuleta mrejesho baada ya mavuno mkuu matokeo yoyote yalete tujifunze, mimi N'yadikwa nakutakia kila la heri...tuleteege na feedback umewekeza kepito ya shingapi

Sent from my SM-T231 using JamiiForums mobile app
 
mrejesho uwe unaendelea kwa kila hatua km hutojali,atleast kila wiki ili wadau wapate kujifunza kupitia kwako mana changamoto ni nyingi kwenye kilimo, nakutakia kila la heri

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Ushafanya utafiti wa soko? Cost of production vepe? Mana naona hesabu zako zimeegemea upande mmoja tu wa mzani a good and clever entrepreneur must know how to balance the sheets! Nakutakia kilimo chema mkuu!

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
 
Kuna uzi upo humu wa matikiti na mwingine wa mboga mboga(angalia kwenye stick treads juu kabisa kwenye jukwaa la kilimo utaiona)!!

Ukipata hizi threads mbili utajifunza mengi sana
 
Una mtaji kiasi gani,?
Kama mtaji ni wa kudunduliza na hujawahi kulima kisha ukaanza na heka tatu, elimu yako ya chuo haijakusaidia, unafanya venture kwa kusukumwa na mizuka biashara ukiziendea kwa mizuka unakula za uso tu
Ungeanza na heka 1 au 2 kujifunzia makosa yako
 
Ushafanya utafiti wa soko? Cost of production vepe? Mana naona hesabu zako zimeegemea upande mmoja tu wa mzani a good and clever entrepreneur must know how to balance the sheets! Nakutakia kilimo chema mkuu!

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app

Naomba Mungu amsaidie aone hii comment ili aanze kujipanga na soko mapema
 
Ushafanya utafiti wa soko? Cost of production vepe? Mana naona hesabu zako zimeegemea upande mmoja tu wa mzani a good and clever entrepreneur must know how to balance the sheets! Nakutakia kilimo chema mkuu!

Sent from my TECNO-J7 using JamiiForums mobile app
Ok mkuu nashukuru sana kwa comment yako hata hivyo cost nineshindwa kuiweka kwa sabab project haijafikia mwisho ,wakat natoa mrejesho ntaweka na cost but mpaka sasa namshukur MUNGU sana maana cost niliyotumia mpaka sasa sio kubwa
Nimekodisha shamba kwa30,000Tshs Kwa kila hekar sasa Kwa heka tatu ni 90,000Tshs. Nimelimiwa Kwa sheli Za ng"ombe Kwa 10,000Tshs per hear,vibarua ni cheap sana hk nilikolimia.Nilinunua mbegu Za kisasa aina ya kingsuger ambayo 500gm nilipanda hekar moja na nusu Kwa hiyo utaona hekar tat nilinunua gram 1000. Gharama ya mafuta kwa maana kumwagilia nime budget lak6 hadi kuvuna na ninaona haitaisha yote, gharama zingine Kama kununua viuatilifu I mean madawa pamoja na mbolea kama NPK sio kubwa unakuta dawa chupa inauzwa elf 5, mbolea kilo moja elf 1. Kuhusu soko lipo la uhakika huku kwet sa iv tikit hazipo za kutosha wauzaj wanalazika kufata mikoa jiran Kwa gharama kubwa hadi sasa ninawateja watatu ambao kila mmoja anajinadi kuyachukua yote. Pia nimeongea na watu wa kiwanda flan ivi wao wanasema nikifikisha angalau tani 10 ambapo Kama hekar mbili zimetuzwa vizur zinafikisha wao wataijia mzigo shamban

Sent from my HUAWEI P7-L10 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom