Nimeamua kujiendeleza kielimu angalau niweze kwenda sawa na mpenzi wangu

Mboka man

JF-Expert Member
Aug 22, 2020
478
1,638
Sijajua kama nakosea au laa ila nimeamua kujiendeleza kielimu angalau niweze kwenda sawa mpenzi wangu kielimu upande wangu niliishia Diploma ila mpenzi wangu ana masters na ana kazi yake nzuli tuu hivyo nimeona na mimi acha nijiendeleze maana Siwezi jua mbeleni kuna nini.

Upande wangu baada ya kupiga jicho la mbali nimeamua kujiendeleza kielimu huku napiga mishe zangu za kutafuta hela kama kawaida lengo la kujiongeza niweze kupanua Wigo wa ufahamu kumiliki fursa hata nisipojiliwa basi kielimu basi tusipishane sana na mpenzi wangu.

Kama nimekosea basi mtaniambia kuhusu hiloo.
 
Kuna Msemo usemao katika kila mwanaume mwenye mafanikio nyuma kuna mwanamke sasa hapo ndo pakujiuliza miaka yote ulikuwa wapi kwanini hukujiendeleza mpka umepata mwanamke

Anyway kuliko kulala ni bora upambane ufike mbali kama mwenzio itakusaidia sana huko mbeleni
 
Ukifuatilia uhalisia wa maisha ya maprof na madokta walio wengi huwezi kutamani kusoma ufikie ngazi zao za kielimu. Wengi wao ni waongo sana, wezi wa kupindukia, ni wanafiki kupita kiasi, wanapropaganda wazuri mno, walevi wa kupindukia, wazinzi mno! hasa hawa wanaofundisha vyuoni hawamuogopi Mungu kiuhalisia

Kasome uelimike sio ulingane na mpenzi wako
 
Elimu ni muhimu sana kasome tu tena utasoma kwa bidii sabab unajua ukicheza ukafeli hutakua sawa kielimu na huyo mwenzio, kwaio kasome.
NB: kulingana kielimu na mpenzi wako haimaniishi hawezi kukuacha/kukudharau
 
Soma uongeze maarifa kwa manufaa yako, acha kushinda na mwanamke...
 
Sijajua kama nakosea au laa ila nimeamua kujiendeleza kielimu angalau niweze kwenda sawa mpenzi wangu kielimu upande wangu niliishia Diploma ila mpenzi wangu ana masters na ana kazi yake nzuli tuu hivyo nimeona na mimi acha nijiendeleze maana Siwezi jua mbeleni kuna nini

Upande wangu baada ya kupiga jicho la mbali nimeamua kujiendeleza kielimu huku napiga mishe zangu za kutafuta hela kama kawaida lengo la kujiongeza niweze kupanua Wigo wa ufahamu kumiliki fursa hata nisipojiliwa basi kielimu basi tusipishane sana na mpenzi wangu

Kama nimekosea basi mtaniambia kuhusu hiloo
Yatakukuta mambo kama yaliyonikuta Mimi nalia na ninajuta kila siku na kumwomba mungu japo tu anifikishe sehemu flani ni inbox tupeane ushauri ndugu usikurupuke
 
We tumia hela kijinga upeleke ada siku mambo ya kikubumia ndio utajua hujui 😂
Wanawake hawakubaligi kusapoti kwa kutoa hela zao bila kelele nyingi!
 
Back
Top Bottom