Nimeamua kuishi kama kijana wa 'Kizanzibari'

Usedcountrynewpipo

JF-Expert Member
Aug 1, 2012
3,636
2,725
Mimi ni kijana (mwanaume) wa Dar!

Nimejaribu kufanya comparison kati ya vijana wengi wa bara na wale wa visiwani nikagundua kuwa vijana wa visiwani wana ishi maisha mazuri sana kuliko sisi wa bara.

Hii inatokana na kwamba sio watu wa kupenda makubwa na hata wanawake wao wako less demanding.

Last time nilipokuwa kisiwani nilimuona kijana mmoja akiwa amempakia mrembo wake kwenye kivespa haoo wakibarizi katika mitaa ya visiwani, and they seemed to be very happy. Kwa kweli niliwatamani sana na nikawaza sie vijana wa bara tumekuwa so westernised na kujazwa ndoto za kuishi kama wazungu, in the end tumekuwa na maisha yasio na raha, mwendo wa kuiga nani ana nini, na wadada wetu ndio wako so demanding, mara mtoto anataka simu ya laki nane n.k Ultimately tumejikuta tukiiishi maisha ya stress na kukosa furaha, ihali wenzetu wa visiwani wanafurahia maisha yao ya wastani.

Sasa ukijumlisha na hii hali ya hapa kazi tu, nimeonelea nibadili life style. Badala ya kuishi kama Westerners, sasa nimeamua nichukue lifestyle ya visiwani na kuishi kama kijana wa 'Kizanziberi'..

I hope it will make me less stressed and much happier...
 
Hahahahaaa
Mimi nadhani ukitaka kuishi hivyo ili upate kile hasa unachokihitaji itabidi ukaishi hukohuko 'Zanziberi',maana huku kila kitu kiko complicated.
Badala ya kupata furaha utaishia kupata stress zaidi.

Nakubaliana na wewe,wakazi wa kule wana maisha ya kawaida sana.
Nimewahi kuishi nao nikawa nastaajabu maana hata mavazi yao ni 'ya kizamani'!
 
Mkuu umesema kweli lakini ata bara unaweza kuishi maisha yako na siyo ya naigizo. Unapotafuta mwenza au mke usioneshe fake life, tafuta marafiki wa tabia unayoitaka, pia ibada kwa dini unayoiamini itakufanya usitetereke na maisha fake ya watu wanaokuzunguka.
 
Nimejaribu kufanya comparison kati ya vijana wengi wa bara na wale wa visiwani nikagundua kuwa vijana wa visiwani wana ishi maisha mazuri sana kuliko sisi wa bara.
Hii inatokana na kwamba sio watu wa kupenda makubwa na hata wanawake wao wako less demanding.
Last time nilipokuwa kisiwani nilimuona kijana mmoja akiwa amempakia mrembo wake kwenye kivespa haoo wakibarizi katika mitaa ya visiwani, and they seemed to be very happy. Kwa kweli niliwatamani sana na nikawaza sie vijana wa bara tumekuwa so westernised na kujazwa ndoto za kuishi kama wazungu, in the end tumekuwa na maisha yasio na raha, mwendo wa kuiga nani ana nini, na wadada wetu ndio wako so demanding, mara mtt anataka simu ya laki nane n.k Ultimately tumejikuta tukiiishi maisha ya stress na kukosa furaha, ihali wenzetu wa visiwani wanafurahia maisha yao ya wastani...
Sasa ukijumlisha na hii hali ya hapa kazi tu, nimeonelea nibadili life style. Badala ya kuishi kama Westerners, sasa nimeamua nichukue lifestyle ya visiwani na kuishi kama kijana wa 'Kizanziberi'...
I hope it will make me less stressed and much happier...
 
Zanzibar vespa ni luxury pia.Bora ungesema kampakia kwenye phoenix ningekuelewa lakin kwa vespa hapana hiyo ni usafir luxury pia.
Alaf tambua maisha ya zanzibar ni ya kawaida sana katika nyanja zote.Ni kawaida kumkuta kijana wa kizanzibar anatembea bila viatu mguun.
Pia tambua ile nchi ina utaratib fulan wa dini ya kiislam.Kama hujaoa itakubid uwe makin sana katika masuala ya mahusiano hapo namasnisha huwez chukua mpenz wako mchana kweupe ukamgegede ghetto kirahis rahis tu.
 
Umenichekesha sanaaa!! chukua mwanamke anaefanana na wewe anekupenda wewe kama wewe hata znz wanapenda walokua navyo ila sema hakuna malezi kama ya watu wa dar, omba mungu akupe mwenye kheir na wewe na mue na maelewano ....
 
Good luck, vitu kama sofa ni anasa, wengi wakalia mazulia sitting room. Kuna jamaa yangu alifikia hatua ya kugeuza Monitor ya Computer ya chogo kuwa TV.

Mavazi mwendo wa msuli vest Na T shirt. Ukibadili kanzu kwa makobazi.

Muruaaah kabisa.
 
Tabia ya kuiga mbaya jamani unataka ufanane na cris brown wkt kwenu mbagala pale dampo mondi aliposhootvideo.wadada sasa eti kim kadashian hehehe hii fake life mbaya umetoka kwenu umeacha watoto wamekula dona asubuhi na kachumbari we eti unajiweka matawi mjini.bongo msijifananishe ni unyamwezini huyo babaake kim kadashian kabadili jinsia awe mwamamke we ht hela y kumtibu babaako tez dume huna hehehe.kuwa real nenda shamba ukishindwa pika mama ntilie fuga kuku sio kufuga mikucha km jini na mawigi.bongo huku ndo fursa hizoo
 
He heee! Una majungu wewe!
 
Back
Top Bottom