TIQO
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 13,787
- 2,078
Nimeamua kuhama nyumba niliyo kuwa naishi baada ya mama mwenye nyumba kunizushia ya kunizushia wakati sijawahi hata ingiza binti kwenye ghetto langu, nikaamka saa 3 maneno, nikirudi saa 2 usiku maneno nikirudi saa 5 usiku maneno, nikijipikia ugali na nguru maneno yaani shida tupu huyu mama mwenye nyumba sijui lengo lake nini. Nimehamia mtaa wa 3 toka nilipo kuwa nikiishi.