Nimeamua kufungua biashara ya mama lishe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nimeamua kufungua biashara ya mama lishe

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by sajosojo, Oct 16, 2012.

 1. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #1
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 774
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Helo wadau naomba ushauri wenu niko hapa dar nina kama mil 1 nataka kufungua biashara ya mama lishe,nimwajili mtu wa kupika,je itanilipa?
   
 2. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #2
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikiwashauri wajasiriamali wengi kwamba furaha yako katika biashara isiwe katika fedha/faida unazopata; lazima kuwe ni jambo la zaidi linalokusukuma kuanzisha biashara. Fursa yeyote ya biashara hutokana na uhitaji wa huduma/bidhaa katika eneo husika, hivyo basi biashara yako inapaswa kulenga au kufikia zaidi jamii inayokuzunguka kulinga na uhitaji wao. Kila biashara inalipa, bali hutegemeana na uhitaji uliopo katika eneo husika, ikiwa umeona uhitaji wa kuwepo kwa huduma hiyo katika eneo husika basi utapata faida tu; bali kama huduma hiyo inapatikana katika eneo husika na unahitaji kuongeza ushindani tu, inabidi ujipange vizuri.
   
 3. E

  ESAM JF-Expert Member

  #3
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Songa mbele na kazi maana biashara ya chakula lazima watu wale tu. Ila kama alivyoshauri Mgombezi angalia uhitaji wa huduma katika eneo husika au soko la bidhaa yako. Lakini pia kumbuka suala la chakula lazima liambatane na usafi wa hali ya juu, yaani mazingira pamoja na vifaa utakavyotumia. Pia usisahau kumwomba Mungu akusaidie na kuibariki biashara yako, ila fungu la KUMI umtolee usimwibie. Baada ya hapo mafanikio ni lazima tu.
   
 4. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #4
  Oct 16, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 555
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Biashara hyo nzuri mtaji ulionao usikupe hofu ili uweze kucompete vizur biashara hyo inahitaji mambo kadha yawe sawasawa.
  1. Usafi unahitajika wa hali ya juu( mazingira ya mgahawa,wahudumu, vyombo,na upishi)
  2. Kauli nzuri
  3. Ubunifu katika upishi
  4. Weka huduma za ziada
   
 5. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 774
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  thanks sana kwa kunipa moyo i really appreciate wadau
   
Loading...